UKAWA mtakuwa wehu

Maramla

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2014
Posts
588
Reaction score
648
Hivi hawa jamaa vipi...wanaikataa katiba inayopendekezwa halafu wanataka vitu vilivyo kwenye katiba inayopendekezwa vitumike kwenye uchaguzi mwezi octoba

1:tume huru ya uchaguzi
2:matokeo ya rais kupingwa mahakamani
3:rais ashinde kwa zaid ya asilimia 50 yaani 50+1
4:mgombea huru

Kwa akili za kawaida mtu unatakiwa uone ni kiasi gani wanaikubali katiba hii inayopendekezwa...me nashukuru kwa wao kuuonesha unafki wao kwa kuwarubuni wananchi kuikataa ili wakose kile kilicho bora ndani ya katiba inayopendekezwa....watanzania tusiwe wajinga kurubuniwa na kundi hili na compani yao
 

Tena borfa we umesema maana wanaikataa halafu wakati huohuo wanahityaji hivyo vitu viwepo, wehu kweli hao watu.
 
Keep up kwa mtizamo yakinifu
 
Sijui mmekula maharage ya wapi mkavimbiwa?? Katiba inaweza ikaahirishwa mpaka mwakani. Lakini mwaka huu ni wa uchaguzi. Ili ufanyike uchaguzi bora, huru na haki sio ukawa peke yake ni vyama vyote chini ya TCD viliazimia hayo yafanyike Jk ikiwa mmoja wao. Sasa inachekesha mnavyotumia hivyo vifungu ili eti mbariki likatiba lenu bovu.. hiyo katiba haitapita.

Naona wiki imekuwa ndefu hakuna posho... Vijana wa lumumba njaa zitawaua..buku saba inawatoa ufahamu
 

Mpuuzi wewe na hao walokutuma, kama huna hela ya sikukuu useme watu wakupe, kojoa ukalalwe huko unaongea ujinga ujinga tu humu ndani au umetumwa, buku 7 huyo alokuzaaa mchumia tumbo wewe.
 

sio kwamba ni mbaya yote kuna baadhi ya mambo hayapo sawa kuna baadhi ya vipengele vipo kiujanja kila kundi limewakilishwa ila hizo haki hawez kuzidai kisheria.
 

Hakuna serikali 3 pia wanadai et masuala ya uwajibikaji yameondolewa
 
Mpuuzi wewe na hao walokutuma, kama huna hela ya sikukuu useme watu wakupe, kojoa ukalalwe huko unaongea ujinga ujinga tu humu ndani au umetumwa, buku 7 huyo alokuzaaa mchumia tumbo wewe.

Matusi hayo
 
Mpuuzi wewe na hao walokutuma, kama huna hela ya sikukuu useme watu wakupe, kojoa ukalalwe huko unaongea ujinga ujinga tu humu ndani au umetumwa, buku 7 huyo alokuzaaa mchumia tumbo wewe.

Tulia dawa iingie.. jibu hoja sio kukurupuka na kuvimbiwa kwako na pilau la pasaka. Nimewaambia hayo mliyoorodhesha ni maazimio ya kikao cha mwisho cha TCD chini ya mwenyekiti John Cheyo kilichofanyika Ikulu ya Dodoma.. Jk na CCM n wajumbe halali na walishiriki.

Sasa unatakiwa upinge kwa hoja... Kwamba hayo maazimio sio ya TCD.

Sasa wewe mpuuz mmoja, mjinga mmoja unajiita Ebola Hatari cjui umekula maharage ya wapi, unawayawaya kama mtoto uliyevishwa nepi..

Jibu hojaaa!! Sio maneno
 
Hv mmelipwa ujira gani unaomfanya kudharau hata wazazi wenu.....
Kinachopongwa na UKAWA ni hii katiba pendekezwa sawa....na wanachokubali UKAWA ni ile rasimu ya pili ya Mh. Warioba.

Sawli: Je hayo uliyoyaandika yapo kwenye rasimu ya pili ama hayapo?

Je katika vitu hinavyopingwa na UKAWA hivyo ulivyovitaja vipo?

Acha ushabiki tu eti kwakuwa umepewa fulana na kofia kaa chini tafakari maisha anayoishi babu yako au bibi yako kule kijijini amestahili kuishi maisha hayo? Usifungwe akili na kutegemea za mwenzako....ZINDUKA.
 

Inaonekana kwenu mmeshindia maharage hahahahaha maana unayapenda kuyataja taja weka namba nkutumie hela mule pilau leo maana mtaendelea kuharisha harisha ovyo, waswahili wanasema AISIFIAE MVUA UJUE IMEMNYEA ndo wewe unatajataja sana maharage humu ndani, jana juzi mmeshindia hayo hayo hapo kwenu eeenh!! pole sana HAPA KUKU TUUU, DAGAA HAMU!!
 

Hizi ID mpya zina mambo kweli
 

Khee kumbe na hii hoja nayo!!!
 
Mtoa mada naomba ufahamu kuwa katiba ni zaidi ya hayo uliyoyataja ambayo ni matakwa ya kisiasa, bado kuna matakwa ya kijamii, kiuchumi, kiuongozi na utawala bora. Sasa wewe unapoangalia tu matakwa ya kisiasa na kuanza kuhalalisha katiba pendekezwa na kuharamisha malalamiko ya ukawa unakuwa umejikita saana kiitikadi zaidi kuliko uhalisia. Jenga hoja vizuri kisha urudi ili tuchangie vizuri badala ya kutufanya wote wana siasa.
 

We unawaambia wenzio na wewe huoni yanakuhusu hayo? kama umetumwa pole sana humu hatuhitaji wachumia matumbo, uzalendo kwanza mengine baadae, kama uliahidiwa cheo huko ujue kibarua unacho cha kukosoa mambo mazuri.
 

Bora umejipambanua.. Tumeelewa kichwani kwako ni kamasi tupu zimejaa.. hufikifii chochote zaidi ya kula.. Ukinijua nadhan utazimia!!.. sina shida ya hela ya kula wala mahala pa kulala, in fact najitosheleza.. Ninachopigania ni ubora wa Tanzania
yetu.

Kijana usiruhusu tumbo ndiyo likufanyie maamuzi.. matokeo yake ndiyo haya... Hoja unashindwa kujibu unabaki unawayawaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…