KAULI ZA HASSAN NASOR MOYO KUHUSU UCHAGUZI 2010
MWAGA UGALI, NAMWAGA MBOGA
DUKU DUKU LA KATIBA LAZIZIMA TARATIBU VISIWANI
WAPO WAZITO NYUMA YAKE, MWANZO WA HALI TETE VISIWANI
Hivi karibuni mzee Hassan Moyo ameeleza matukio ya uchaguzi 2010.
Habari alizosema hazikanushwa na chombo chochote na inabaki kuwa ndivyo.
Kauli za Hassan Nasor Moyo,mmoja wa wazee waliobaki wenye heshima visiwani haziwezi kupuuzwa.
Ni kauli nzito zinazoashiri mtafaruku mbele ya safari.
Mzee Moyo ni mwenyekiti wa kamati ya maridhiano kule visiwani.
Katika mambo anayosimimia kwa maoni yake, ni msimamo wa serikali 3 na znz yenye mamlaka kamili.
Siku za karibuni amekuwa karibu na viongozi wa tume ya Warioba na wznz wanaopenda mfumo mbadala wa muungano.
Moyo pia anatajwa kuhusika na uandikaji wa katiba ya znz ya 2010 kwa ushawishi ingawa si kiongozi.
Kauli zake za majuzi kuhusu uchaguzi wa CCM na jinsi CCM walivyoshindwa hadi kuombwa Maalim akubali matokeo ni nzito. Amewataja akina Riyami na Karume katika maelezo yake.
Kuwataja kuna maana moja, kwamba walitoa ridhaa ya yeye kusema lolote kuhusiana na uchaguzi kwa kutaja majina yao. Tunakumbuka Aman Karume ndiye aliyesaini katiba ya znz 2010, katiba inayokinzana na ya JMT na pengine ni chagizo la kufanyia mabadiliko katiba ya JMT yaliyokwama.
Kauli ya Mzee Moyo inakuja katika hali mbali mbali
- Kuchukizwa na jinsi mchakato wa kihuni wa Sitta/Chenge ulivyomalizika kwa kuungwa mkono na baadhi ya wawakilishi wa znz.
- Kutoridhishwa na kitendo cha Mansour Himid ambaye ni mshirika wake kuwa na kesi mahakamani ambayo inamfunga mdomo wa kutetea kile wanachokion sahihi
- Kuona ile znz waliyoitaka sasa haitakuwepo tena kwa mkono wa wazanzibar wenyewe
Ni kwa mantiki hiyo, Mzee Moyo ameamua ''mwaga mboga namwaga ugali'' kwamba hana cha kuficha na haielekei siku za usoni atakuwa msuluhishi katika mazingira tata kama yale ya 2010.
Yote hayo yanatokana na uhuni wa mchakato uliomalizika Dodoma kwa CCM kufanya mambo yao ili yawe mambo ya taifa.
Kwa mtazamo mwingine, Moyo anaonyesha jinsi gani hali itakavyokuwa tete mwakani huko znz.
Na alichokisema ni ujumbe kuwa hamkani si shwari tena.
Kauli za Moyo zisichukuliwe kwa wepesi kama ''loser'' bali kwa weledi na uangalifu.
Wazee wenye ushawishi wanapojitokeza hadharani na kumwaga siri zilizokuwa hazijulikani ni jambo la kufikirisha.
Pamoja na hayo, Moyo anaungwa mkono na wazito ambao kwa namna moja au nyingine hawakuridhishwa na uhuni uliokamilika Dodoma. Hivyo si Moyo peke yake nyuma yake kuna wazito.
Wazito hao wana duku duku na pengine wanachelea kujitokeza yasije wakuta yaliyomkuta Manosur Himid.
Moyo ni kigingi ambacho CCM haikiwezi hata kidogo. Ingalikuwa CCM wana uwezo, basi wangeshamuondoa uanachama.
Hivyo katika duku duku la katiba, Mzee Moyo ni kipaza sauti cha wazito wengi walio nyuma ya znz na duku duku.
Hilo tu limeshawagawa wazanzibar na mwakani au kabla ya hapo lazima yatatokea mambo mazito.
Mambo kama yale ya siku za nyuma.
Uhasama miongoni mwao sasa unafikia hatua ya juu. Ni hali inayozimama kichini chini, ni suala la muda kutalipuka tena.
Kama JK alidhani anaweza kuwafurhisha wznz kwa namna anavyofanya, basi anaweza kujikuta anamaliza muda wake akiwa na madoa kama yale ya Mkapa.
Tusemezane
CCM WAMJIBU NASOR MOYO KIMYA KIMYA
DALILI YA MANENO MAZITO KUWAINGIA
RAIS WA ZNZ ATAMBA HADHARANI, TUMEPATA FURSA ZAIDI TANGANYIKA
WATANGANYIKA KUENDELEA KUBEBA MZIGO WA MUUNGANO, FARAJA NI ZANZIBAR
Bandiko hapo juu tumeeleza jinsi Moyo alivyo na ushawishi wa siasa za znz.
Katika mkutano wa Kibanda maiti, Rais Shein amemualika mwanapinduzi mzee Himid Ameir ili azungumze kuhusu mapinduzi.
Hii ilikuwa katika kampeni za kura za maoni za CCM ingawa haijulikani katika CCM ni utaratibu gani unaotumika.
Kinachoweza kukubalika ni kuwa CCM wana uhuru wa kufanya jambo bila ridhaa ya wananchi wa itikadi zingine za kisiasa au wasio na itikadi.
Hivyo mkutano wa Dr ni halali na wala hauna shaka kwavile ameenda kunadi katiba ya CCM iliyoandikwa na Chenge/Sitta
Mzee Ameir hajulikani katika siasa za znz. Katika hali ya kuogopa maneno mazito ya Mzee Moyo na hali tete ya kisiasa, CCM wameamua kutafuta watu wa umri ili kuja kuzungumzia mapinduzi na katiba yao.
Mzee Ameri ameitwa ili kumjibu Mzee Moyo kwasababu ndani ya CCM hakuna anayeweza kumgusa achilia mbali kumjadili.
Hawa akina Nape na Mwanadiwani, walikuwa hawajazaliwa wakati Moyo akiwa madarakani.
Hawana ubavu wa kumwita na kwa kuzingatia sana ushawishi wake. Kumtisha kama walivyofanya kwa Mansour Himid haiwezekani.
Ni kwa muktadha huo, wameamua kumjibu kwa kumtumia wazee wengine.
Katika mkutano huo, Rais SHein amesema znz imeshiriki kikamilifu kuandika katiba ya Chenge na Sitta.
Hapa ndipo tunasema kuna unafiki na kigeugeu au uongo.
Ilikuwaje wakati wanabadili katiba ya znz 2010, Rais Shein hajalizungumzia hilo.
Inakuwaje wadai kushiriki katika maamuzi ya mambo ya Tanganyika ikiwa wao hawaitambui katiba ya JMT tena kwa dharau.
Lakini pia kauli zake zinashangaza sana. Rais Shein anasema wananchi wa znz waamue.
Katika mkutano huo ulikokuwa wa CCM ni jambo la kushangaza Rais wa znz akiongelea suala la wananchi wote wakati anaongea na wana CCM.Hizo zote ni jitihada za kuipa shamra shamra katiba ya Chenge na Sitta iliyo dorora na kukosa mashiko.
Miongoni mwa mambo aliyosema Shein ni suala la mafuta na gesi kuondolewa katika muungano.
Hapa ndipo anapowaambia Watanganyika jambo wasilojua.
Mafuta na gesi ya Tanganyika itatumika katika muungano. Kwamba, badala ya kuwanufaisha Watanganyika, rasilimali hiyo itakwenda znz kuziba pengo la bajeti, kulipa mishahara ya SMZ na kulipia gharama za Rais na makamu lukuki wa kisiwa chenye uchumi wa bilioni 400 kwa mwaka.
Watanganyika wangeuliza, endapo wznz wameondoa gesi na mafuta ili wajinufaishe, kwanini gesi na mafuta ya Tanganyika itumike kubeba muungano? Kwanini liwe jambo la muungano ikiwa upande wa znz jhawataki.
Jibu la swali hilo ni rahisi sana, kama huna Tanganyika basi una Tanzania ambayo znz imo na hivyo wao kuja kuchukua chako ni halali. Wewe si mzanzibar ni Mtanzania hivyo huwezi kudai chao.
Ni kwa muktadha huo, kila siku tunawakumbusha Watanganyika kuwa wznz huja katika muungano kwa jina na pale penye masilahi.Mumemsikia Rais wa zanzibar akitamba jinsi wanavyonufaika na fursa akimaanisha rasilimali za Tanganyika.
Bila Tanganyika, wznz wataendelea kwafanya Watanganyika shamba la bili.
Hili ndilo Watanganyika wanapaswa kujiuliza na kufikiri na si kufikiri kura za maoni za CCM.
Kura ya maoni inawekewa shamara shamra kuwasahulisha Watanganyika kuwa suala zima halina uhalali.
Ni uhuni uliofanywa kuchukua rasimu iliyoandikwa na Chenge ambaye si tu maadili yake yanatia shaka bali pia ameshiriki kuiba hata kura za CCM wenzake akishirikaiana na Sitta(Megji na wengine)
Wananchi lazima watafute majibu ya maswali magumu kuhusu muungano na wala waasifikirie kuhusu katiba ya CCM na Chenge/Sitta. Hiyo ni katiba yao hivyo waachwe waendelee na katiba yao.
Wananchi waulize
1. Matatizo ya miaka 50 yamepatiwa ufumbuzi gani
2. Suala la gharama kwa mujibu wa rasimu ya CCM inayotaka kufanywa ya taifa limepungua ukilinganisha na Warioba?
3. Muundo wa muungano unatoa haki kwa pande moja, je pande ya pili ambayoni Tanganyika ipo wapi?
4. Kwanini Mtanganyika alipe kodi, atumie raislimali zake kwa ajili ya nchi jirani ya znz?
5. Utegemezi wa znz na uwekezaji wa Tanganyika una manufaa gani kwa walipa kodi wa Tanganyika
6. Je, suala la znz kuwajibika katika muungano limepatiwa majibu?
Bila kujiuliza maswali hayo, tutaendelea kuwasikia wznz wakitamba na fursa kama alivyotamba Shein.
Kwamba mdudu kupe yupo mgongoni na bado anadai fursa za kumnyonya ng'ombe tena kama haki yake.
Bila kuamka, Watanganyika wataamka kila asubuhi kung'ang'ania dala dala ili kwenda kulipa kodi zaidi kwa nchi jirani ya znz.
Wakati huo huo wznz wanatoa misamaha ya ndugu zao, wanaacha kukusanya kodi wakijua shamba la bibi ni Tanganyika.
Huko Tanganyika wanapata 4.5% ya kodi ya Mtanganyika, wanasoma bure, wametengewa fursa kama ajira zao peke yao bila formula. Wao kila jambo wameliwekea uzio tena mahususi kukabiliana na Mtanganyika.
Tusemezane