Ukiacha ufundi, Benchikha inabidi awafundishe wachezaji ujanja wa kimpira

Ukiacha ufundi, Benchikha inabidi awafundishe wachezaji ujanja wa kimpira

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
Moja ya jambo kubwa ambalo Benchikha anaweza kuisaidia Simba na hilo jambo likaisaidia kwa miaka mingi ni kuwapa wachezaji ujanja wa mbinu za kisaikolojia ya jinsi ya kucheza na waarabu wenzake.

Simba imesogea pakubwa sana katika mpira wa Afrika. Leo hii hakuna anayeshangaa tena Simba akimfunga Al Ahly au Wydad na kwa siku zinavyokwenda inaonyesha Simba inaweza kuanza kuzifunga hizi timu hata huko ugenini na lisiwe jambo la ajabu sana.

Katika mechi ya juzi dhidi ya Wydad, Benchikha alijua katika dakika zile za mwisho Wydad atapush sana kupata goli maana sare haikuwa inawapeleka popote. Akaamua kuongeza nguvu safu ya mbele ili Wydad wakiongeza juhudi za kupata goli, nyuma wakiacha mianya itatumiwa na Simba kupata goli. Na kweli ile strategy ilionyesha dalili za kuzaa matunda maana ukiangalia kuanzia dakika ya 80 hivi, Simba ilikuwa inapata nafasi nyingi za counter attack ila shida ilikuwa wanakuwa slow sana kufika kwenye goli la Wydad. Laiti Kibu angekuwepo kwenye zile counter, nadhani Simba ingepata chochote kitu.

Kosa moja ambalo Simba walifanya dakika za mwisho ni kutojaribu kupoteza muda. Mtu pekee aliyeonekana kufanya hivyo ni golikipa Ayoub. Kuna faulo alifanyiwa Phiri, angeweza kabisa kuua dakika 1 nzima pale lakini hakufanya hivyo. Ile faulo ya mwisho ambayo kwa kweli ilifanywa kimakosa na Zimbwe, wangekuwa ndiyo waarabu wanahitaji sare na wanajua hata dakika za nyongeza zimeisha, kwanza wangeanza kulalamika muda umeisha na kuna mchezaji angejiangusha pale golini kabla faulo haijapigwa ili kuzua zogo.

Hilo lingefanywa nina uhakika lingewatoa mchezoni Wydad na kumpa pressure refa kumaliza mpira ingawa ile faulo bado ingelazimika kupigwa maana mpira hauwezi kumalizwa katikati ya mazingira yale ila ile faulo isingekuwa na madhara kama ambavyo yalitokea. Badala yake kutokana na kutofanya vurumai lolote wakati ile faulo inapigwa, Simba ndiyo walikuwa hawako mchezoni.

Najua kuna maeneo nengine zaidi ya haya ya kupoteza muda ambayo wanatuzidi ujanja ila kwa kiasi kikubwa Waarabu karibu wote wanatumia mbinu zinazofanana katika mpira. Ningetamani Benchikha awape madini ya mbinu hizi na ingependeza zaidi kama Simba ingekuwa na wachezaji vijana zaidi na baadhi ya wataalamu wa kitanzania kwenye benchi la ufundi ili mbinu hizi ziweze kubaki na timu kwa muda mrefu.
 
Huyo Benchikha na vijana wake usm algers waliwafanyia yanga
 
Simba ina timu mbovu tu. Hata kocha atumie mbinu gani, hakuna kitakacho badilika. Na mkumbuke safari yenu msimu huu inaishia kwenye hatua hii ya makundi.
 
Acha ujinga hakuna mbinu zaidi ya uwekezaji na kuwa na wachezaji wenye quality kubwa zaidi yao!
 
Simba ina timu mbovu tu. Hata kocha atumie mbinu gani, hakuna kitakacho badilika. Na mkumbuke safari yenu msimu huu inaishia kwenye hatua hii ya makundi.
Kweli ujinga kipaji.

Hongera.
 
Back
Top Bottom