Ukiachana na bei za Saruji, bei ya kupata Kibali cha ujenzi wa nyumba ya vyumba vitatu huko Halmashauri ya Kigamboni ni Tshs 250,000

Ukiachana na bei za Saruji, bei ya kupata Kibali cha ujenzi wa nyumba ya vyumba vitatu huko Halmashauri ya Kigamboni ni Tshs 250,000

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Wakati tukiendelea kumtafta mchawi aliyepandisha Cement!
Shida kubwa ya halmashauri nyingi ni kugeuza sheria kuwa vyanzo vya mapato.

Tutafakali gharama zifuatazo za kibali cha ujenzi huko halmashauri ya Kigamboni.
Bei hizi zinasimamiwa na ofisi ya Mkurugenzi kwa ajili ya kutunisha mfuko wa manispaa/halmashauri!

Bei ya kibali cha ujenzi wa nyumba ndogo kabisa ya vyumba vitatu na sebule kwenye kiwanja cha upana (12m kwa 13m) ambapo ni sawa mita za mraba 156 ni TSh 200,000 (laki mbili) na ada ya maombi ni Tsh 50,000 JUMLA NI 250,000/=

Ikumbukwe hapo hujajumlisha gharama za michoro ya ujenzi na Nauli za saveyi ambapo ukiongeza na hiyo 250k zaweka fikia laki Saba jumla!

250,000 ni sawa na mifuko 17 ya cement inatosha kabisa kujenga msingi!

Kwanza kwanini msitoze Square mita moja hata tsh 200? Ili watu wengi watamani kuja kuomba kibali? Kwanini gharama ya vibali isiwe chini ya elfu hamsini ili kila mtanzania atamani kuja kuomba kibali!?

Screenshot_20201121-092455.png
 
Nani alikutuma kununua kiwanja huko?. Uza mara moja shikisha mtu kwa bei poa nenda huko mapolini kajenge muda si mrefu huduma zote zitakufikia. Hapo paendelee kuwa pori. Pole kwa usumbufu uliojitokeza. Kwa hisani ya mitano tena.
Watu kama wewe ndiyo wale wapangaji wankuwaga wasumbufu hata kulipa kodi ya nyumba
 
Kihere here chako kimekuponza. Kwa nini uombe kibali? We anza kujenga mpaka uandikiwe kwenye nyumba yako 'Simamisha ushenzi' ndipo uwatafute.
Zamani tulikuwa tunaambiwa, soma mpaka ukute kibao kimeandikwa, 'there is no school for you' ndipo uache.
Wanasema ukikutwa unajenga bila kibari faini ni KUBWA karibu 3m na unabomoleshwa hadi upate kibali.
 
Wakati tukiendelea kumtafta mchawi aliyepandisha Cement!!

Tutafakari gharama za kibari cha ujenzi huko halmashauri ya Kigamboni zilivyokubwa zilizo tiwa baraka na ofisi ya Mkurugenzi kwa ajili ya kutunisha mfuko wa manispaa!

Bei ya kibari cha ujenzi wa nyumba ndogo kabisa ya vyumba vitatu na sebule kwenye kiwanja cha upana (12m kwa 13m) ambapo ni sawa mita za mraba 156 ni TSh 200000 (laki mbili) na ada ya maombi ni Tsh 50000 JUMLA NI 250000/=

Ikumbukwe hapo hujajumlisha gharama za michoro ya ujenzi na Nauli za saveyi ambapo ukiongeza na huyo 250k zaweka fikia laki Saba jumla!

250000 ni sawa na mifuko 17 ya cement inatosha kabisa kujenga msingi!

Kwanza kwanini msitoze Square mita moja hata tsh 200? Ili watu wengi watamani kuja kuomba kibari?
View attachment 1631309
Lipeni tu, si uliipigia kura CCM? u alia nini ? hukujua hilo , si umeipenda mwenyewe?

Hii miaka 5 nakwambia utaona kama miaka 30
 
Yaani hizi gharama zinachochea ujenzi holela, haziko rafiki na badala ya kuongeza pato la Halmashauri, zinafanya wanaojenga wazikwepe na kuinyima Halmashauri mapato. Kuliko kutoa laki 250,000/ mtu ataona heri ampe afisa wa Halmashauri 100,000/= ili amlinde na apotezee.

Vv
 
Yaani hizi gharama zinachochea ujenzi holela, haziko rafiki na badala ya kuongeza pato la Halmashauri, zinafanya wanaojenga wazikwepe na kuinyima Halmashauri mapato. Kuliko kutoa laki 250,000/ mtu ataona heri ampe afisa wa Halmashauri 100,000/= ili amlinde na apotezee.

Vv
Mkurugenzi yupo kimya, Waziri wa ujenzi yupo kimya, waziri wa ardhi yupo kimya pia
 
mi naona hata ikiwa bure, wajenge tu maana hilo pato la halmashauri linaingia Hazina mtu anaenda kununulia jogoo kwa laki moja.waiiii
Yes! Wangefanya hata bure lakini wakakomaa kwenye kukusanya elfu kumi kumi za kodi ya jengo kila mwaka! Kutokana na udogo wake, kila mtu atalipa, Tena wanaweza Fanya vizuri zoez likihusha serikali ya mtaa na wajumbe ili kuhamasisha malipo
 
Ni kila mahali (Tz) UKitaka kujenga lazim upate kibali au Ni kitamboni tu?
Kila mahala, lazima upate building permit but hii kitu ilikuwa bure tuu, nashangaa sasa unalipia. Nadhani ni kwa sababu halmashauri na manispaa zimeporwa sources of income na kwenda serikali kuu so kila mtu anapambana kivyake...
 
Back
Top Bottom