Ukiachilia mbali bakery ya Super Loaf, Temeke bakery na Mtoni bakery kuna bakery gani kubwa Dar?

Tatetitotu

Member
Joined
Mar 6, 2018
Posts
58
Reaction score
42
Poleni kwa majukumu wapendwa,kama kichwa cha habari kinavyojieleza kwa yoyote analelewa bakery kubwa ya kutengeneza bidhaa(bite) kama mikate na kuendelea katika jiji la dar tofauti na hizo bakery tajwa hapo juu pliz naomba anijuze
 
Nenda keko magurumbasi pale ipo, na nyingine pale gomz kushoto ya kituo cha polisi
 
Unafanya Market research? Hizi Bekary zinakuwa zinapata Competition kari sana kutoka mtaani kwa wakaanga Vitumbua, mandazi na Chapati hawa ndo wengi sana na ushindani wanao utoa si wa kitoto hata kidogo
 
Ndio changamoto ni kubwa sana kwa toka kwa small Vendors wa bite
 
Unafanya Market research? Hizi Bekary zinakuwa zinapata Competition kari sana kutoka mtaani kwa wakaanga Vitumbua, mandazi na Chapati hawa ndo wengi sana na ushindani wanao utoa si wa kitoto hata kidogo
Tatizo ladha hizo bekary zingekua zinatoa ladha tofauti na tulizo zoea wangeuza sana
 
Kuna mikate huwa imeandikwa Mbezi bread, Bakery yake ipo api?
 
Unafanya Market research? Hizi Bekary zinakuwa zinapata Competition kari sana kutoka mtaani kwa wakaanga Vitumbua, mandazi na Chapati hawa ndo wengi sana na ushindani wanao utoa si wa kitoto hata kidogo
Hawa wa bakeries wana supply hadi huku kwetu mkoani. hao wapika maandazi wanawezaje kushindana nao ?
 
Poleni kwa majukumu wapendwa,kama kichwa cha habari kinavyojieleza kwa yoyote analelewa bakery kubwa ya kutengeneza bidhaa(bite) kama mikate na kuendelea katika jiji la dar tofauti na hizo bakery tajwa hapo juu pliz naomba anijuze
Mapenzi yangu yote na mikate na kutembea kwangu kote,nimejikuta nimetekwa na Mikate toka FURAHA BAKERY,aisee hawa watu viwango vyao si vya nchii wana ladha ya kipekee sana tofauti na bakery nyinginezo nchini,alafu hawa watu wamejitanua sana na bidhaa zao zinatoka na kupendwa sana ,nilienda NJOMBE nikawakuta wametapakaa supermarket zote na madukani,IRINGA ndio kabisa,DODOMA,RUKWA ,niliwakuta pia SINGIDA japo baada ya kuulizia niliambiwa hawafiki kiusambazaji badala yake kuna wafanyabiashara wanaojumulia LUPA au kuagiza,nilijiuliza sana nguvu na uwezo wa kikazi wa hawa watu compared na bakery zilizopo Dar nikashindwa kupata jibu,ila nilipojaribu kuwaulizia walipo nikaambiwa kiwanda kipo JIJINI MBEYA,zamani nilikuwa nashuhidia watu wakisafiri kwenda mikoani wanawanunulia ndugu zao mikate ya Dar kama zawadi pekee na yenye thamani kipindi hicho mimi pia nikiwa mmoja wao,lakini siku hizi naona mambo yameanza kwenda kinyume badala yake nimeanza kuona watu Wanatoka ama kurudi Dar wanakuja na mikate ya mikoani ana kuagiziwa na jamaa zao.
 
Bakery kubwa kabisa dar: Azam bakeries, Mini bakeries, Temeke bakeries, Grand confectionery. Zilizobaki ni ndogondogo kama Gomz, Mtoni, Furaha, Bahari etc..... una swali lingine kuhusu bakery ?
 
Bakery kubwa kabisa dar: Azam bakeries, Mini bakeries, Temeke bakeries, Grand confectionery. Zilizobaki ni ndogondogo kama Gomz, Mtoni, Furaha, Bahari etc..... una swali lingine kuhusu bakery ?
Hii Furaha na Bahari zipo Maeneo gani nisaidie namna ya kupafikia
 
Hawa wa bakeries wana supply hadi huku kwetu mkoani. hao wapika maandazi wanawezaje kushindana nao ?
Mkuu haya mambo kama huyajui uliza, wale ni Indirect competitors. Kuna Direct na Indirect. Sasa kuna wakati Inderect wanakuwa na ushindani mkubwa kuliko Direct. Kusambaza mikoani kwani huko mandazi hayapikwi?au Mandazi na Vitumbua vinapikwa Dar pekee?
 
Mikate Yangu bora ni Brown tu. Hiyo white huwa haipandi kabisa na nakulaga pale kunapo kuwa hakuna namna
 
Nilishaacha kula mikate miaka mingi sasa,siku hizi Mimi nakunywa chai na mihogo ya kukaanga toka kwa mama mwajuma,au chapati za bibi mfuko,nikikisa hizo na kula sambusa za jirani yangu hapa mama mazoea,mambo ya kula chai na mikate ni ya zamani sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…