Ukiagiza bidhaa au gari na ukakwama ushuru ni vyema baada ya gari kufika ukapeleka Bonded Warehouse.

Ukiagiza bidhaa au gari na ukakwama ushuru ni vyema baada ya gari kufika ukapeleka Bonded Warehouse.

Hakuna limit ya kukaa, kukataliwa hakupo labda uwe ujakamilisha vitu au mzigo ukawa na mashaka. Mzigo ukiwa Bonded bado unakuwa upo chini ya TRA kwaiyo hapo kinachofanyika ni kubadili eneo la kutunza mizigo kutoka Bandarini kwenda Bonded Warehouse ambapo gharama za kutunza mizigo (storage charges) zipo chini.

Kwenye kila Bonded Warehouse kuna ofisi rasmi za TRA.
Ok,
Na hizo bonded muda wote tu zinakuaga Open, I mean zina nafasi??. Yaan huwezi kuleta gari labda halaf kipindi hicho bonded zikawa zimejaa zote ukakosa kabisa??
 
Ok,
Na hizo bonded muda wote tu zinakuaga Open, I mean zina nafasi??. Yaan huwezi kuleta gari labda halaf kipindi hicho bonded zikawa zimejaa zote ukakosa kabisa??
Bonded kwa Dar zipo nyingi sana mkuu zaidi ya 800+, nyingine mpaka wana offer ya bei na kutafuta wateja. Labda kama unapitisha bidhaa zako kwenye mipaka isiyochangamka mikoani
 
Kama umeagiza gari au bidhaa na ikawa imefika Kwenye Bandari na wakati huo pesa ya ushuru umepungukiwa,kukwama au hukuwa na taarifa sahihi za ushuru na makadirio ya kodi yamekuja zaidi ya kiwango ulichopanga njia sahihi ni kumwambia wakala wa Forodha(Clearing Agent) afanye maombi (TRA) ya kupeleka gari au mzigo kwenye Bonded Warehouse.

Bonded Warehouse ni ghala au sehemu ambayo mizigo inayosafirishwa nje au iliyotoka nje ya nchi inatunzwa inaposubiri kulipiwa ushuru.Bonded Warehouse zipo ambazo zinamilikiwa na serikali au watu binafsi zipo mikoa yenye bandari na mipakani.

Endapo umeagiza gari au bidhaa yoyote na umekwama pesa kabla au baada ya mzigo kushuka bandarini usipate pressure. Inatakiwa umwambie Clearing Agent atafute Bonded Warehouse kwa ajili ya kuweka gari au mzigo wakikubali kuna nafasi, inabidi ajaze fomu ya TRA kuomba kupeleka mzigo Bonded Warehouse baada ya kupeleka mzigo Bonded utakapo kuwa sawa utalipa kodi hata baada ya mwaka na mzigo wako utatoka.

Faida za kutumia Bonded Warehouses
1. Gharama za kutunza mzigo (storage charges) zipo Chini na zina chajiwa kwa mwezi. Mfano gari ndogo kwa mwezi bei ni usd 80, wakati bandarini kutunza kwa mwezi bei ni kubwa sana na huchajiwa kwa siku na ukubwa (CBM) unaweza ukapewa bill ya usd 1000

2.Inaondoa mzigo kuwekwa kwenye list ya overstayed good na kuja kupigwa mnada. Mzigo ukikaa sana bandarini unaingia kwenye overstayed goods na mmiliki asipo utoa unapigwa mnada. Kwenye Bonded Warehouse mzigo unaweza kutunza zaidi ya mwaka

3. Mmiliki wa mzigo ni rahisi kwenda kuangalia mzigo au gari yake ikiwa Bonded Warehouse. Gari ikiwa bandarini mmiliki hawezi kuingia kuona gari au mzigo, ila ukiweka bonded unaomba kuingia Warehouse na kuona mzigo ila huwezi kutoa. Pia akitaka auze ni rahisi kumuonyesha mteja gari au bidhaa ikiwa Bonded tofauti na ikiwa bandarini inabidi auze kwa kutumia picha za mzigo ulikopakiwa na documents za mzigo.

Bonded Warehouse ina faida kwa waagizaji wa bidhaa na magari, inaepusha mizigo kuuzwa kwa mnada. Kama ulifanikiwa kuagiza gari ya usd 3000 (CIF) bora upeleke Bonded Warehouse ukalipe usd100 per month kuliko kuiacha bandarini ukaja kupewa storage charges za usd 3500 na ushuru unakusubiri. Hapo gari inaingia kwenye mnada unaingia hasara
Nina swali mkuu ,hivi ukilipia gari bei yake na ushuru kwa pamoja kuna shida yoyote?na kipi bora kulipia ushuru bandarin ikishafika au kufanya malipo yote siku ikiwadia ni kuchukua tu gari.
 
Back
Top Bottom