Ukiamua kumfanyia wema mwanamke basi mfanyie wema Huo kwa kiasi

Ukiamua kumfanyia wema mwanamke basi mfanyie wema Huo kwa kiasi

Mwizukulu mgikuru

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2021
Posts
5,715
Reaction score
13,739
Unapoamua kumfanyia wema kiumbe mwanamke basi jitahidi sana umfanyie kwa kiasi, usijitoe saaana .utakapoamua kumnunulia gauni la laki mbili basi hakikisha wewe unavaa kiatu au saa yenye thamani zaidi ya laki mbili ya gauni ulilomnunulia. Kufanya hivi kutakusaidia kukuepusha na mambo makuu matatu pale mwanamke huyo mtakapokuwa mmeachana au amekusaliti.

(1) Kukuepusha na maumivu makali ya moyo hasa kwa kuona ulipoteza muda kumhudumia mtu ambaye hakukuthamini au kukupenda kiukweli.

( 2) Kuua au kumdhuru mwanamke. Hii imekithiri sana kipindi hiki na moja ya sababu kubwa za mauwaji au vitendo vya ukatiri ukimuhoji zaidi mwanaume aliefanya tukio hilo atakuambia "huyu mwanamke nilimpa kila kitu lakini alikuwa hatulii sijui alikuwa anataka nini!".

( 3) huwezi kuyumba kiuchumi au kuharibikiwa kimaisha. Siku zote mwanamke akiachana na mwanaume huyo huwa hapendi kumuona akiendelea kiuchumi anatamani kumuona mwanaume anaharibikiwa kabisa kimaisha au anapoteza ramani kabisa kama sio kuwa chizi au kufa kabisa😁
IMG_20250305_115401.JPG
 
Kuna Jamaa hapo juu kafuta comment yake ila aliandika anasema we msomeshe mtoto wa singo Mama iko siku mtoto wake atakuja kukuuliza kwani nilikuomba? who asked for your help? Si ni kiherehere chako.

Sasa sijui mada inahusiana vipi na singo Mama.
 
"mwanamke ni kiumbe anayesahau haraka Sana "
Kuna member hapa ana comment nitafute type yangu 😁😁😁 mpaka Mimi kuandika Haya nimejiridhisha vya kutosha. Mimi ni miongoni mwa wanaume walioowa mwanamke wa kiwango Cha chini sana..Mpaka leo mama yangu huwa ananiambia ilikuwaje wewe Mwizukulu mgikuru ukaowa mwanamke mbaya hivi? Mfupi mnene mweusii, kidato Cha nne aliferi Mimi mme wake Nina degree mbili, hata kuhesabu saa ya ukutani hajui yaani ni mbumbumbu mzungu wa reli..
 
Kuna Jamaa hapo juu kafuta comment yake ila aliandika anasema we msomeshe mtoto wa singo Mama iko siku mtoto wake atakuja kukuuliza kwani nilikuomba? who asked for your help? Si ni kiherehere chako.

Sasa sijui mada inahusiana vipi na singo Mama.
Inaonekana anawachukia sana singo mama😁😁😁
 
Kuna member hapa ana comment nitafute type yangu 😁😁😁 mpaka Mimi kuandika Haya nimejiridhisha vya kutosha. Mimi ni miongoni mwa wanaume walioowa mwanamke wa kiwango Cha chini sana..Mpaka leo mama yangu huwa ananiambia ilikuwaje wewe Mwizukulu mgikuru ukaowa mwanamke mbaya hivi? Mfupi mnene mweusii, kidato Cha nne aliferi Mimi mme wake Nina degree mbili, hata kuhesabu saa ya ukutani hajui yaani ni mbumbumbu mzungu wa reli..
Kwani umuite mkeo mbumbumbu mkuu
 
Kuna stori ya yule jamaa wa kigamboni alimchenja mkewe nilisoma sehemu inahuzunisha sana
Yule jamaa alikuwa yupo vizuri sana kiuchumi na alijitahidi sana kumpa mwanamke kila alichokitaka, lakini mwanamke ni kiumbe kisicholidhika, tamaa nyingi na ameumbwa kusahau kwa haraka.
 
Back
Top Bottom