Ukianza kuona dalili hizi kwenye uchumi ni muda wa kuchukua tahadhari

Ukianza kuona dalili hizi kwenye uchumi ni muda wa kuchukua tahadhari

Kama mtaalamu mdogo sana katika maswala ya uchumi kuna vitu nilikuwa navingojea ili niweze kutoa mtazamo wangu na nilikuwa nafuatilia kidogo kwa mbali nikawa napata feedback kuanzia mwezi wa tisa tutaanza kuona viashiria ya kushuka bei ya vitu ambavyo katika maisha yetu katika nchi yetu hatujawahi kuona.
Kwa kuwa nilijua kwa undani sana nini kulichotokea kwenye nchi za Amarika na Ulaya kwenye miaka ya 2008. Nikawa naikisubiri nikione hicho hapa ni kaanza kuona dalili ndogo ndogo za nyumba za kupanga kuanza kuteremka bei, muda wa vacancy kujaa ukawa mkubwa zaidi, nikaanza kuona taasisi za fedha kuoanza kusitisha kukopesha na hii mara zote hutokea baada ya kuona huenda risk ni kubwa kuliko walivyoiangalia mwanzo. Sasa kwenye repoti za nusu mwaka za financial institutions mwaka huu inaonyesha kuwa pamoja na taasisi nyingi kuwa vyema ila swala la provision for bad debt imekula faida ya taasisi nyingi kiasi kwamba sijui katika nusu ya mwaka inayokuwa itakuwajeje ni jambo la kusubiria tuone.

Ila sasa nyumba zinazouzwa kutokana na watu kushidwa kufanya marejesho ndio ambazo zinanikumbusha history hiyo ya 2008 katika nchi za nyingine zilizokumbwa na uchumi kuwa doroo.
Kikawaida watu wote wanaowekeza kwenye Real estate industry wanajua kuwa kitu kinachopandisha bei ndio hicho hicho kinashusha yaani kwa mfano mtaani mwako ikiwepo nyumba inauzwa ukasikia nyumba ile imeuzwa shilingi 500m ukaona ilikuwa imechoka moja kwa moja ukitaka kuuza ya kwako iliyo nzuri zaidi utaweka Shilingi 800m na ikinunuliwa basi kila mmoja anajua nyumba mitaa hiyo ni range ya 500 to 800 na kinyume chake ni kweli.

Kwa viashiria hivi ni ni muda mzuri wa kuchukua taadhari na uwekezaji wako na risk yoyote unayochukua ni lazima ufikirie vizuri na uwe na plan B kwa kila jambo la kiuichumi ni muda ambao tunajua kwamba ili uchumi upanuke ni lazima usinyae kidogo halafu unapanuka huwa hapanuki tuu ukipanuka sanaa unapasuka then unasinyaa kidogo halafu unakuwa tena ni muhimu kwa level ya mtu bianafsi kujua uko wapi katika mzungumko mzima wa uchumi na kama taifa tufanye nini ili madhara yake yasiwe makubwa kwa Taifa.
Na kwa kumalizia hapo ndipo utaalamu uliotukuka unahitajika ili tusonge mbele tuweze kufika malengo yetu kama nchi na kwa watu wetu. Nawatakia jioni njema na tafakari yenye maana katika ujenzi wa taifa letu hili zuri.
Kipindi hiki ndio stimulus package ya kuuchangamsha uchumi inatakiwa, sio wakati ule wa awamu iliyopita zikatolewa na kama sifa ya awamu ile, zikatafunwa na waliopata fursa, wakati hakukuwa na mdororo wowote Tz.
 
Kipindi hiki ndio stimulus package ya kuuchangamsha uchumi inatakiwa, sio wakati ule wa awamu iliyopita zikatolewa na kama sifa ya awamu ile, zikatafunwa na waliopata fursa, wakati hakukuwa na mdororo wowote Tz.
Hutakiwi kutoa stimulus package katika uchumi unaoanguka kutokana na shortsighted near term government policy.

Stimulus package inatolewa kwenye recessionary crisis.

Muanguko wa sasa wa uchumi kwa kiasi kikubwa unatokana na serikali ya awamu ya tano kukataa kusikiliza ushauri wa wataaalam.

Sasa ukiweka stimulus package mara baada ya kufungia hela zote BOT kinyume na ushauri wa wataalam, utakuwa unaweka conflicting policies.

Hizo hela kuwekwa nje ya BOT tu ni stimulus package, ambayo umeiondoa kinyume na ushauri wa wataalam.

Sasa umeondoa stimulus package halafu ulete tena stimulus package, unarudi nyuma hatua moja, unaenda mbele hatua moja.

Utakuwa unajua kwamba unataka kurudi nyuma au kuenda mbele?
 
Siku zote kabla sijasoma kilichomo naangalia Nature ya paragraph napata jibu halaf naamua nionekane mvivu au nisome
 
Back
Top Bottom