RIGHT MARKER
Senior Member
- Apr 30, 2018
- 129
- 473
📖Mhadhara (58)✍️
Leo ni Novemba 8, 2024. Mwaka 2024 unaelekea kwisha, ile mipango yako yote uliyopanga kuifanya na kuikamilisha mwaka huu imebuma, tena imebuma kweli kweli.
• Unadhani ni kwanini?
Shida ilianza hapa;- Wewe kabla hujaanza safari yako tayari ushawaambia ndugu, jamaa na marafiki kuwa unataka kusafiri. Tena uliwatambia kwenye status kuwa; "Mwaka huu ni lazima wakuite bosi" - Thubutu!
Kila ukitaka kufanya jambo zuri unaomba ushauri kwa marafiki, hujiamini, utafikiri ulizaliwa na marafiki. Mbaya zaidi ushauri wao huchanganyi na akili zako.
Siku hizi wachawi, wanafiki, na adui ni wengi sana mtaani, hivyo punguza au acha kabisa kupost mipango yako kwenye mitandao ya kijamii. Hata kama unapost utani wenzako hawajui hilo.
Wapo watu ambao wana nguvu za kichawi za kuchelewesha fungu lako bila hata kufunga safari kwenda nyumbani kwa mchawi/mganga wake. Yaani yeye akitamka tu, fungu lako linachelewa kukufikia. Kuwa makini.
Right Marker
Dar es salaam