Magical power
JF-Expert Member
- Sep 27, 2022
- 2,158
- 5,626
Ukibaini umekosea chaguo/njia basi usiogope kuanza upya, maana hata watu sahihi au wema hukosea chaguo kwasababu ya ubinadamu walioumbwa nao au wamesababishiwa na mtu
Mahusiano yanatakiwa yawe daraja la maisha yako wala si ukuta wa kufupisha au kuharibu maisha yako. Ukiona mahusiano uliyonayo hayawi daraja la ukuaji wako wa kiroho, kiakili na kiafya basi si mahusiano ila hilo ni tatizo
Mateso na maumivu ya kuishi na mtu asiye sahihi hayana msaidizi kuwa utawagawia mtu akusaidie utaathirika nayo wewe mwenyewe wala si baba, dada, mama yako unayemuogopa utamtia aibu ukiyachilia mahusiano yakuseyo
Wewe ndiye unajua unapitia nini. Wewe ndiye unapaswa kuwa mwenye maamuzi. Mapenzi yamebeba hatma yako usikubali mtu fulani kwa ujinga wake akuharibie maisha yako ukaishilia
Si kila mtu anafaa kuwa mume/mke wengine wanatakiwa wabaki kama mapambo na mifano
Usikubali kuishi kwenye majuto au makosa yanayosahihishika na kubadilishika kwa ajili ya kesho yako njema. Tamani kumalizia kipande cha maisha yako kilichosalia hapa duniani kwa amani na tabasamu kuliko kuendelea kuishilia.
Rafiki linda moyo wako kuliko chochote kile ulindacho. Elewa neno KULIKO CHOCHOTE ina maana moyo wako ndio kila kitu kwenye roho, mwili na nafsi. Moyo ni kitu chanye thamani na ndio maisha yako yameshikamanishwa ndani
Sina cha kukufundisha ila nakutafakarisha. Unaweza kunipuuza ila usiyadharau maneno yangu. Yatakusaidia mahala hata kama sio leo.