Ukichoka na Mishe za Mjini Dar, Kajipumzishe Pugu “Ushoroba”

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
26,961
Reaction score
77,890
Mambo vipi wazee?
Your browser is not able to display this video.

Kuna pahala panaitwa Pugu Kazimzumbwi alhamarufu Ushoroba.
Ni pazuri sana kwa mkazi wa Dar au Pwani anaetaka kupumzika siku moja au weekend kuzipisha kelele za bodaboda, bajaji, magari, wauza sumu ya mende, etc. Nimeenda mara kadhaa na weekend hii pia nilienda.

Utangulizi

Pugu Kazimzumbwi ni safu ya misitu iliyo chini ya TFS (Tanzania Forestly Service) inayopatikana Wilaya ya Kisarawe, mwanzoni kabisa ukitokeq Dar es Salaam. Kwa wenyeji kidogo, ni opposite na shule ya sekondari Minaki.


Unafikaje?

Kama unatumia usafiri binafsi, ukitoka Gongo la Mboto, unaendelea na safari hadi mataa ya Pugu, unaacha njia ya Chanika we unaendelea na ya Kisarawe. Mwanzoni ukivuka kibao cha Karibu Wilaya ya Pwani, mbele kidogo Kushoto utaziona ofisi zao.


Ukifika Ofisini


Watakupokea, watakupa introduction kidogo ya utalii uliopo na activities zilizopo na gharama zake.


Gharama

Kuna gharama za aina mbili hapa, mosi ni gharama za kuingia. Hapa mkiwa wawili mtalipa elfu 19 pamoja na gharama ya tourguide hapo hapo na gharama za gari kuingia na gari hapo hapo.

Malipo ni kwa control no. Kuna 5% inalipwa cash pale inaenda serikalini ila ni kama buku tu. Unapewa risiti. Na malipo ya pili ni options za activities utakazo amua kufanya ukiwa uko ndani, tutazidiscuss kidogo.


Utalii na Activities zilizopo

Usitegemee makubwa kwasababu hii sio national park wala game reserve, huu ni msitu wa asili, kwahiyo baadhi ya vitu ambavyo utaviona maybe kwako ni vya kawaida, mfano:

Hiking/Kupanda mlima

Hapa utapanda mlima karibia 1.5km utatumia kama dk 30-50 kutokana na stamina yenu. Ukiwa na maji 1L na mavazi sahihi itapendeza zaidi.

Ukifika juu kileleni kuna view point nzuri utafanikiwa kuona msitu mzima pamoja na kuona shehemu kubwa sana ya Dar es Salaam.

Ukiwa juu utaona ni jinsi gani Dar hatujafanikiwa kujenga mji wetu kwa kuzingatia mipango miji.

Kayaking /Kuendesha viboat flani

Hii ni option, utalipia elfu 10 na mnakaa wawili wawili au watatu au unaweza endeshwa.

Ukiwa mjanja vizia muda hakuna watu wengi kwenye foreni uta spend muda mwingi zaidi majini.

Camping

Wazee wa kulala msituni inawahusu. Hii ni package kwa mtu anaetaka kuspend usiku pahala tulivu huku akiotea moto, kuchoma nyama, kunywa bia na kua karibu zaidi na nature na mpenzi wake.

Gharama itategemea na size ya tent ila
Kwa tent la watu wawili ni elfu 25 na kama una tent lako gharama inazidi kua ndogo.

Sport Fishing

Kwa wanaopenda kuvua samaki, ukilipia utaazimishwa ndoana uweze kuvua. Ila hautaondoka na samaki. Just for fun.

Unaweza kuomba moto though uweze kuwachoma au kuwala. Samaki wanaopatikana ni perege na kambare.

Location za Picha
(Hiyo Jordan Showoff tu)



Kuna baadhi ya watu wanaenda kwaajili ya kupiga picha za kumbukumbu mfano harusi, birthday au vikao binafsi.

Ila kuingia na camera au drone kuna gharama yake itabidi ulipie.

Kuona Mzimu wa Mavoga

Kuna pahala ambapo mzimu wa Mavoga ambapo wenyeji wa Kisarawe Wazaramo walikua wanaenda kuombea dua. Utaona ayo mapango na kujifunza.

Sikwenda kwasababu masharti moja wapo usiwe umelewa, mwanamke asiwe MP na jana yake usitoke kufanya tendo, katika ayo matatu mawili nishafeli. Nikaona isiwe shida.

Lake View

Kuna ilo ziwa ndio laitwa Ushoroba au Minaki Dam ambalo lazamani kabla DAWASA haijafika Kisarawe lilikua linasupply maji wilayani na vijijini vya jirani.

Utaona miundombinu iliobakia mfano pumphouse na mabomba.

Kuendesha baiskeli

Ukienda na bike yako kuna trail za kuendesha kama utakua interested. Ila hawana baiki za kukodisha.

Kuna Batman caves

Ingawa lipo nje ya huu msitu ila nashauri nenda kalitembelee.

Viumbe waliopo je?

Kusema kweli hawana viumbe uko zaidi ya kobe wachache, kenge, komba, nyani, na viumbe wadogo wadogo ambao sio issue.

Kiumbe pekee special ni Pazi mwenye bendera ya Tanzania, nadhani ndio aliowekwa kwenye round about ya Mlimani City pale.

Uoto wa Asili

Kuna uoto wa aina nyingi ila special sana ni mti wa Mpugupugu ambao ndionumezaa jina Pugu. Inasemekana hadi leo huu mti unapatikana Tanzania pekee na katika ilo eneo la Pugu tu. Mti huu ni dawa na wataalamu mbalimbali uwa wanakuja kuchukua sample ya mti kwa tafiti za Kibotania.



Huduma za ziada

Hadi sasa, wameboresha sana huduma za vyoo na mabafu yamekua ya kisasa zaidi.

Vile vile kuna muwekezaji amefungua restaurant anauza vinywaji na vyakula vya aina mbali mbali ingawa kidogo ni overpriced kama upo na tight budget nashauri beba takeaway au kula kabisa. Mfano Chips kavu kwa Buku 3 so kadiria mfuko wako.


Vitu vya kuzingatia

Kama unaenda daytrip beba maji vinywaji na vyakula ukiweza.

Zingatia usafi, usitupe tupe takataka ovyo, maana lile eneo ni safi na limewapa ajira vijana wengi sana.

Ukienda kucamp kumbuka mashuka, mito na taa (unaweza kutumia simu yako), usiogope umeme wa kuchajia upo.

Bwawa hawaruhusu kuogelea ila watajenga swimming pool wamesema.

Mi nimeona tushee hayo, mwingine aongezee.
 

Attachments

  • PXL_20240525_110804811.MP.jpg
    7.3 MB · Views: 14
Alieweka hii habari, amesema ukichoka na mishe za Dar, zikhusisha na kelele za maspika za wauza na za mende. Wauza viwanja.

Yesu anatafutwa wapi wakati ukienda kwa hao wauza dawa za mende yupo.

Akina Masimo na wenzie wapo kila sehemu zenye mishe Dar.

Asante ulieleta hii habari, kuna siku nitaenda kulala huko, ila je nyama choma zinapatikana ndani ya msitu ama inabidi uende na nazo, pili ule msitu hauna nyoka, maana nilipita hivi karibuni, naona umefunga sana, ila sikujua kama kuna mapunziko ndani.
 
Kuhusu nyama choma, unaongea na tour guide uliekabidhiwa atakutafutia nje bucha. Au kama unaweza kwenda nayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…