- Source #1
- View Source #1
Eti ukikanyaga mifupa ya mnyama au mdudu mwenye sumu na ikakuchoma inaweza kukupelekea madhara kupitia kwa ile sumu ya mdudu au mnyama uliekanyaga mifupa yake iliyokuchoma? Mfano mzuri kwa mifupa ya nyoka mwenye sumu aliyekufa.
- Tunachokijua
- Mfupa ni tishu ngumu katika mwili mwa binadamu na wanyama wenye uti wa mgongo. Mifupa inahimili ogani nyingine mwilini na kuuwezesha mwili kusimama na kuupa umbo. Mifupa pia kinga kwa sehemu muhimu sana kama vile mifupa ya fuvu inakinga ubongo na ubavu wa kifua unaokinga moyo na mapafu.
Sumu ni dutu yoyote inayoweza kuharibu shughuli za seli au inayoweza kudhuru muundo wa seli au kiumbehai.
Kuna wadudu ambao wana sumu na ambao hawana sumu, miongoni mwa wadudu wenye sumu ni kama nyuki, nyigu, honi, jackets za manjano, mchwa wa moto, nairobu fly nk. Wadudu hawa, huingiza dutu iitwayo sumu pale wanapong'ata au kutembelea ngozi ya binadamu. Watu wengi wanaoumwa na wadudu hawa hupona ndani ya masaa au siku. Kwa wengine, sumu hii inaweza kusababisha athari ya kutishia maisha au kuondoa uhai.
Nyoka ni reptilia wasio na miguu. Kuna takriban spishi 3,000 duniani, wako kwenye mabara yote nje ya Antaktiki na Aktiki.
Kama ilivyo reptilia wengine nyoka nao wana damu baridi na ngozi ya magamba. Wote ni wala nyama na spishi mbalimbali hutumia sumu kwa kuwinda lakini nyoka walio wengi hawana sumu wanashika windo kwa miili yao au kwa mdomo tu.
Je, Ukikanyaga mifupa ya wanyama, wadudu hasa nyoka aliyekufa utapata madhara kutokana na sumu waliyokuwa nayo kipindi wako hai?
JamiiCheck imefuatilia suala hili kwa kuzungumza na Afisa Habari wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Beatus Maganja pamoja na Mkufunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka, Tito Lanoy ambao wanaeleza kuwa:-
Hakuna madhara ya sumu ya mdudu au mnyama aliyekufa ambayo mtu anaweza kupata iwapo atachomwa na mfupa wa kiumbe hicho baada ya kufa, madhara pekee mtu anayoweza kupata ni jeraha au maambukizi ya magonjwa iwapo mfupa wa mnyama huyo aliyekufa alikufa kwa magonjwa kama kimeta na ya kufanana na hayo au tayari mfupa huo umeshapata maambukizi ya vimelea vya magonjwa kama bakteria.
Kuhusu kuchomwa na mfupa wa nyoka aliyekufa, Afisa Habari wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Beatus Maganja anaeleza kuwa:-
"Sumu ya nyoka inakaa kichwani kwenye mfuko wa sumu (venom gland) na hutoka kichwani kupitia kwenye mrija unao unganisha mfuko wa sumu na jino la nyoka (venom duct). Hivyo basi ukikanyaga mifupa ya nyoka tofauti na jino la nyoka huwezi pata sumu, Sana sana utapata bacteria infection".
Ukikanyaga mifupa ya nyoka tofauti na jino la nyoka huwezi pata madhara, Sana sana utapata bacteria infection au tetanus. Nyoka akifa sumu yake iliyopo kichwani na kwenye jino hukauka na endapo mtu atachomwa na jino la nyoka mwenye sumu aliye kufa, anaweza kupata madhara ila siyo mifupa. Ni vyema kwenda hospitali mara tu upatapo hiyo ajali ili uweze kupata tiba sahihi
Pia, Mkufunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka, Tito Lanoy ameleeza kuwa:-
Ikumbukwe kwamba ni 15% ya nyoka wanaopatikana Tanzania ndio wana sumu (venom) nyoka wengi hawana sumu.
Kwa hao wachache wenye sumu, 15% wakifa meno yao yanakuwa na sumu pia na likikuchoma utadhurika japo siyo sawa na mtu aliyeumwa na nyoka.
Sumu ya nyoka inatengenezwa na kuhifadhiwa kichwani kwenye mfuko wa sumu na siyo mkiani kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakisema.
Kuhusu kukanyaga mfupa wa wanyama na wadudu waliokufa, Mkufunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka, Tito Lanoy ameleeza kuwa:-
Tofauti na baadhi ya nyoka, nge, buibui na tandu ambao ni wadudu, hakuna wanyama wengine wenye sumu. Ila wanyama wanaweza kuambukizwa magonjwa kama rabies ambayo aking’ata mtu anaweza kumwambukiza Mtu akila au akishika mzoga wa mnyama aliye kufa kwa kimeta pia atadhurika
Ni vyema kwenda hospitali mara tu unapochomwa na mifupa ya mnyama aliye kufa, Pia tusishike wala kula nyama ya mnyama aliyekufa.