Ukienda kwenye guest au lodge yoyote usilale bila kuomba

Ukienda kwenye guest au lodge yoyote usilale bila kuomba

Ndugu zile Lodge zina mambo mengi sana na kabla ujalala kuna mtu alitoka hapo,na pengine mfanya usafi angekwambia akiyokutana nayoo hata chumbani usingelala.
Umenena

Mbali na uzinzi, hizo nyumba zina mazindiko ya kutisha na kuna mambo mengi ya kiganga
 
Haijalishi uko kikazi ama unaenda kusalimia familia, ndugu ,jamaa au marafikii.Nakujuza tu ukienda Lodge guest zozote kabla ya kulala sali.

Ndugu zile Lodge zina mambo mengi sana na kabla ujalala kuna mtu alitoka hapo,na pengine mfanya usafi angekwambia akiyokutana nayoo hata chumbani usingelala.

Humohumo yanafanyika uzinzi na uchafu kama wote.

Asubuhi njema
Hata kama unaenda kufanya uzinzi uombe pia?
 
Anapaswa kuwa na Imani ya MUUMBA wako wakitaka kukuua wanatangulia wao

Siyo guest tu hata nyumba za kupanga, hata chakula, hata nyumbani kwako cha msingi uwe na Imani na uwezo wa kuwasiliana na MUUMBA wako
 
Unaomba kwa Mungu maovu yasikupate at the same time huyo huyo Mungu ndio kaumba maovu-kuna mambo yanafikirisha sana.
 
Nakubaliana na wewe kabisa.

Niliwahi kwenda Katavi kikazi na ilibidi kulala lodge.

Nilipoingia chumbani tu kwenye hiyo lodge nilihisi kama kusisimkwa na mwili ambapo kiuhalisia sikuweza kuelewa ni kwa nini lakini pia nafsi yangu ilikataa kabisa kulala mule ndani. Nilimuita muhudumu nikamwambia anibadilishie chumba. Kuuliza sababu nikamwambia sijakipenda tu kile chumba. Nikapewa chumba kingine.

Baada ya siku mbili nilipokuwa naondoka niikuwa napiga stori na yule muhudumu wakati nasubiria usafiri. Yule dada akaniambia kaka inaelekea una imani kubwa sana na Mungu wako, nikamuuliza sababu ya kusema hivyo; Jibu lake ndio lilinichosha kabisa. Akasema mwenye lodge huwa kila baada ya muda anakuja kufanya matambiko hapo lodge kwake na kile chumba nilichokikataa ndio huwa anakitumia zaidi.

Yule dada aliniambia kuwa ilishatokea mara mbili kwa wateja kukutwa wamefariki kwenye chumba hicho bila ya sababu za msingi na wakiwa peke yao.
Na sharti kubwa la mwenye lodge ni kuwa hicho kiwe ndio chumba cha kwanza kupewa mteja akija hata kama vingine vipo vitupu.

Binadamu huwa tunajisahau sana ila kuna mambo Mungu anatuepusha nayo bila hata ya sisi wenyewe kujua. Pengine ningeishia kuwa kafara kama ningelala humo.
Aisee 🤔
 
Haijalishi uko kikazi ama unaenda kusalimia familia, ndugu ,jamaa au marafikii.Nakujuza tu ukienda Lodge guest zozote kabla ya kulala sali.

Ndugu zile Lodge zina mambo mengi sana na kabla ujalala kuna mtu alitoka hapo,na pengine mfanya usafi angekwambia akiyokutana nayoo hata chumbani usingelala.

Humohumo yanafanyika uzinzi na uchafu kama wote.

Asubuhi njema
Kuna nyumba za watu unalala kama mgeni kwenye vitanda ambavyo uzinzi umefanyika, na makochi pia unakalia.
 
Siyo Lodge tu, chochote unachotarajia kufanya tanguliza maombi, tumezungukwa na hatari pande zote
 
Back
Top Bottom