Ukifa leo nani atatoa lock kwenye simu yako?

Ukifa leo nani atatoa lock kwenye simu yako?

Kamwene kamwene

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2019
Posts
1,159
Reaction score
2,601
photo-1504203700686-f21e703e5f1c.jpeg


??
 
Umenikumbusha wimbo wa kitabu cha shule ya msingi miaka hiyoo nilikuwa namuona mtoto wa kaka yangu wangu akiimba kila akitoka shuleni....

Saa ya Babu mzee yaenda miaka tisini hivi sasa.
Saa ya Babu mzee yaenda miaka tisini hivi sasa..
Siku ile azaliwa ile saa yanunuliwa ikamfura hisha daimaaa
Tisini miaka weeh tikitakatikitaka
Haichoki kulia weeh tikitakatikitaka
Ila tuu baasii haiendi tenaa aakifaa mzeee....

Hivyohivyo na simu ya mkononi mtu akifa haitakiwi kufanya kazi tena, ikiwezekana mnamzika nayo tuu. Sana sana ndugu chomoeni line muende kampuni husika na nyaraka za mirathi kuona kama mtu ameacha hela kwenye simu.

Mnaweza mchukia marshaling buree kwa kufukunyua simu yake, simu ina siri nyingi sana za mtu binafsi mziache age nazo kama hajaziweka wazi hata kwa mkewe au mumewe.
#uhuruwakujimwambafy...
 
Simu yangu haina lock [emoji359] ila ni marufuku kuishika na ukiishika usiniulize kitu
 
Kwanini waitoe? Yaani atakae jifanya anapekenyua simu yangu nitamrudia kama ghost nitamuwinda maisha yake yote.

Kuna magemu mengi sana nimeishia level za juu sitaki mtu ayaendeleze kisha aniaribie..
Speaking of game za kwenye simu yaani huwa nashindana na watu online very addictive najikuta napanda level hadi naambiwa first to reach this level halafu napumua naangalia wengine nilipowaacha, napotea kama wiki kisha nikirudi nimepitwa napambana tena hadi nafika level ya juu...

Ila umenichekesha hiyo ya kumtokea atayechukua simu yako aahahahahhaaaa looh.
 
Back
Top Bottom