Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 1,679
- 2,123
Hakuna mtu asiyependa kufanikiwa kikazi, kielimu, kibiashara, kiafya, katika ndoa nk. Mwaka unapoanza watu wengi huwa wanajiwekea mipango na mikakati ili wapate mafanikio. Hapa nakuorodheshea mambo 50 yatakayokuwezesha kuona amani, baraka na mafanikio ukiyafanya. Mwishoni nitakueleza kwanini ukiyafanya haya utafanikiwa:
Ukiyafanya hayo na mengine yote aliyoyaagiza Mungu, hakika utaona baraka na mafanikio tele. Nasema hivyo kwa sababu ndivyo Mungu alivyoahidi katika Walawi 26:3-13 na Kumbukumbu 7:12-24. Mungu hasemi uongo.
"Ukimtii Bwana Mungu wako kwa bidii na kufuata amri zake zote...Baraka hizi zote zitakuja juu yako...Utabarikiwa mjini na utabarikiwa mashambani. Utabarikiwa uzao wa tumbo lako na mazao ya nchi yako na wanyama wako wachanga wa kufugwa, yaani ndama wa makundi yako ya ngʼombe, na wana-kondoo wa makundi yako. Kapu lako na vyombo vyako vya kukandia vitabarikiwa. Utabarikiwa uingiapo na utabarikiwa utokapo. Bwana atasababisha adui wainukao dhidi yako kushindwa mbele yako. Watakujia kwa njia moja lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba. Bwana ataagiza baraka juu ya ghala zako na juu ya kila kitu utakachogusa kwa mkono wako...Bwana atakupa kustawi kwa wingi...Bwana atafungua mbingu, ghala zake za baraka na kukupa mvua kwa majira yake na kubariki kazi zako zote za mikono yako. Utakopesha mataifa mengi lakini hutakopa kwa yeyote. Bwana atakufanya kichwa, wala si mkia. Kama utazingatia maagizo ya Bwana Mungu wako ninayokupa siku hii ya leo na kuyafuata kwa bidii, daima utakuwa juu, kamwe hutakuwa chini. Usihalifu amri zangu zozote ninazokupa leo, kwa kwenda kuume au kushoto, kwa kufuata miungu mingine na kuitumikia."
=====================================
Tafadhali ongezea mambo mengine niliyoyasahau katika orodha hiyo. Itapendeza yakifika 100.
- Ndugu yako akikukosea msamehe hata saba mara sabini – Mathayo 18:21-22
- Usipende usingizi. Lala tu masaa unayopaswa kulala kiafya, usipitilize – Mithali 6:9-11
- Ukikopa, lipa deni – Zaburi 37:21
- Ukipatana na mtu jambo fulani usivunje maagano – Mhubiri 5:4-5
- Usijivunie akili yako – Mithali 3:5-7
- Mpende adui yako. Ukipata fursa, mlishe na kumnywesha – Warumi 12:20
- Ukiweza, watembelee maskini na wajane uwasaidie kuondokana na dhiki zao – Yakobo 1:27
- Ishi kwa unyenyekevu mbele ya wenzako. Usijikweze – Mithali 29:23
- Usimtukane mtu – Mathayo 5:22
- Waheshimu baba na mama yako sio tu kwa kusema “shkamoo” bali hata kwa kuwasaidia kifedha iwapo wana mahitaji – Marko 7:10-13
- Ukiugua, ukaenda hospitali, madaktari wakakupima na kusema hawaoni ugonjwa, ukaenda hospitali ya pili na ya tatu yenye viwango vya juu zaidi, ukaambiwa vivyo hivyo kuwa ugonjwa hauonekani, kemea ugonjwa huo kwa Jina la Yesu – Marko 16:17-18. Baadhi ya magonjwa na udhaifu husababishwa na pepo. Pepo wakitoka, mtu anapona – Mathayo 9:32-33
- Kabla hujaamka, kabla hujalala, usisahau kumshukuru Mungu na kuomba ulinzi wake – 1 Wathesalonike 5:16-18
- Epuka kabisa kufanya uzinzi na uasherati – 1 Wakorintho 6:18
- Usiibe kitu chochote cha mtu – Kutoka 20:15
- Unapoongea na wenzako, usiseme uongo – Waefeso 4:25
- Usiwadharau wasio na pesa au wenye elimu ndogo – Yakobo 2:1-4
- Mtu akikuudhi usikasirike na wala usipange kulipa kisasi – Warumi 12:19
- Maisha yakiwa magumu, usiwaze kujiua – Zaburi 34:18
- Kama umeoa, mpende sana mke wako. Na kama umeolewa usiache kumtii mme wako – Waefeso 5:22-25
- Kama una watoto, fanya bidii kuwatunza, kuwalisha, kuwasomesha na kuwalea katika maadili safi – Mithali 22:6
- Usithubutu kumkufuru Mungu – Mathayo 12:31
- Waepuke malaya wanapokubembeleza ukumbatie vifua vyao – Mithali 5:3-8
- Usipende pesa kupita kiasi, bali uishi kwa kiasi – 1 Timotheo 6:10
- Usiwaonee maskini na pia usiwapendelee matajiri – Mambo ya Walawi 19:15
- Usijihusishe kamwe na mambo ya uchawi au ushirikina – Kumbukumbu la Torati 18:10-12
- Utunze mwili wako kwa kuzingatia kanuni zote za kiafya – 1 Wakorintho 6:19-20
- Epuka kuongea maneno machafu; ongea yaliyo safi na ya kujenga – Waefeso 4:29
- Usiache kusoma Biblia(Neno la Mungu). Isome kila siku na kutafakari usomayo – Zaburi 1:2
- Wapende jirani zako kama unavyojipenda mwenyewe – Mathayo 22:39
- Usipende mabishano; tafuta kuwa na amani na kila mtu – Warumi 12:18
- Fanya kazi halali kwa bidii, epuka uvivu – Mithali 10:4
- Epuka kula rushwa – Kutoka 23:8
- Epuka uchoyo; washirikishe wengine baraka ulizopewa – Waebrania 13:16
- Uwe mkarimu kwa wageni – Waebrania 13:2
- Usikae na chuki moyoni mwako, suluhisha ugomvi haraka – Mathayo 5:23-24
- Usivunje ndoa za watu – Mathayo 19:6
- Usitoe sadaka ili watu wakuone au kukusifu kuwa umetoa – Mathayo 6:1
- Usishirikiane na wengine kutenda dhambi – 2 Wakorintho 6:14
- Usikae na hasira moyoni mwako usiku kucha – Waefeso 4:26
- Jifunze kushukuru kwa kila jambo na kila hali – 1 Wathesalonike 5:18
- Waheshimu wenye umri mkubwa kuliko wewe – Walawi 19:32
- Epuka masengenyo na kuongea maneno ya umbeya – Mithali 20:19
- Usijisifu kwa kuwa una mali nyingi au uwezo mkubwa – Yeremia 9:23-24
- Fanya kazi yako kwa uaminifu, hata kama haina mshahara mkubwa – Luka 16:10
- Usifanye haraka kutoa majibu kabla ya kufikiri – Mithali 18:13
- Usilalamike kila mara; jifunze kuridhika – Wafilipi 2:14-15
- Usiige tabia mbaya za ulimwengu – Warumi 12:2
- Usiache kumuabudu Mungu kwa roho na kweli – Yohana 4:24
- Maisha yetu duniani ni mafupi; tenda mema kadri uwezavyo – Yakobo 4:14
- Kumbuka Yesu Kristo atarudi kuwachukua wale tu wanaomwamini na kuwapeleka mbinguni; kama hujaokoka tubu dhambi zako leo, amini na ukiri kuwa Yesu ni Bwana na umpokee katika moyo wako kwa imani ayatawale maisha yako – Warumi 10:9.