Kuna bibi kule mahome alizeeka sana karb miaka kwenye 95 hivi, sasa nasikia enzi zake alikuwa mchawi kweli mpk tukawa tunaambiwa nyinyi mna bahati yani mmekua wote kwenye familia yetu mana wengine walikuwa wanapoteza watoto sanaaa.
Sasa kipindi anaelekea kufa bwana, ilikuwa kimbembe yan mchana kutwa anashinda kulala, anaropoka ovyoovyo mara watoto wananifinya wale aliowauaga kipindi hicho, tena wengine alikuwa anawataja kwa majina kabisa kuwa wanamfinya, hadi kuku kumbe alikuwa analoga kuku za watu ko nazenyewe eti zilianza kumdonoa[emoji848][emoji848]
Yule bibi kiufupi aliteseka sana walianza kumweka kwenye msege wanaondoka wanaenda shambani wakirudi wanakuta funza zimemtoka za kutosha lakini mtu bado yupo hai hafiii,
Nakumbuka familia ilivochoka waliitaga mganga fulani, mweee jamn yule mganga alivyofika tu machale yalimcheza akasema tangulieni kumbe ameona ngoma ilivo nzito akachochora. Badae akawapigia cm akasema ngoma hiyo ni nzito mana huyo bibi kazuiwa na watoto aliowaua huko anakotaka kwenda pamoja na kuku ndo mana analalamika kung'atwa na kufinywa.
Aliwashauri wamnyonge ila atakayemnyonga akubali kuteseka kama hivo ck ya mwisho wake. Wakakataa wote.
Akawaagiza kumshikisha vitu mbali mbali huyo bibi ikiwemo uwele, ulezi mtama na mahindi kisha watafte mtot mdg wamshikishe kuku aingie naye chumbani walikomlaza mgonjwa. Na aliwambia mkisikia kuku amelia mjue mgonjwa wenu amefariki. Ni kweli walifanya hivo na baada ya dak tano mtot yule kutoka nje walisikia kuku akihangaika ndani kwa kilio na badae kukawa kimya, walivyoingia ndani kweli walikuta bibi tayari kafariki. Ule msiba watu hata hawakulia ilikuwa kama sherehe tu. Vijana walichimba kabuli hadi wakayakuta maji. Alafu enzi hizo hakuna jeneza kule kijijini. Bibi alizikwa ila kesho yake walikuta kabuli limebomoka na kuna shimo lefu. Wazee wakubwa wakasema huyu hajafa ila kasepa ataenda kuishi sehemu nyingne. Kumbe mganga aliwaficha kutakachotokea kwa mtoto mana angewambia wasingekubali. So hiyo hiyo siku ya msiba mtot alipandisha mashetani na dak kadhaa tu akafariki. Mganga alipoulizwa aliongea tu kuwa nilitaka kuwatolea mateso ya huyo bibi tu na kiukweli huyo bibi hajafa kaenda kwingine na alisema hao watu hawafagi bila zindiko malumu.
Mwisho niseme tu. Tuishi vzr na wenzetu mana tuendako hatukujui na hatujui kifo kina maumivu gani, mana yote tunayoambiwa ni nadharia, hakuna anayejua ukweli.