Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nikiwaza kifo imani inazidi,inanifanya nijilazimishe kuzidisha unyenyekevu na kutokuwa na kiburi na kuongeza ibada.Mimi nawazaga Sana hivi unakuaje inafikia mpaka point macho yanafumba na husikii Tena na moyo kufungwa acheni jamani kifo Ni fumbo kubwa sana.wale wanaosema kuwa kufa Ni Kama usingizi wa ghafla sidhani Kama wapo sahihi.ila me nahisi ukiwa huna dhambi ukawa mtu wa Mungu Basi kifo chako kitakuchukua ukiwa huna mawazo Wala stress ila ukiwa Na Mambo mengi na madhambi ya nyuma ukiyafikiria ndo utahisi maumivu.
Jazia jazia nyama kidogokifo hakikuhusu mkuu,kinawahusu waliobaki.ukifa umekufa nothing else
Kuna bibi kule mahome alizeeka sana karb miaka kwenye 95 hivi, sasa nasikia enzi zake alikuwa mchawi kweli mpk tukawa tunaambiwa nyinyi mna bahati yani mmekua wote kwenye familia yenuu (mana wengine walikuwa wanapoteza watoto sanaaa.)
Sasa kipindi anaelekea kufa bwana, ilikuwa kimbembe yan mchana kutwa anashinda kulala, anaropoka ovyoovyo mara watoto wananifinya wale aliowauaga kipindi hicho, tena wengine alikuwa anawataja kwa majina kabisa kuwa wanamfinya, hadi kuku kumbe alikuwa analoga kuku za watu ko nazenyewe eti zilianza kumdonoa[emoji848][emoji848]
Yule bibi kiufupi aliteseka sana walianza kumweka kwenye msege wanaondoka wanaenda shambani wakirudi wanakuta funza zimemtoka za kutosha lakini mtu bado yupo hai hafiii,
Familia ilivochoka walimtafta mganga fulani, yule mganga alivyofika tu machale yalimcheza akasema tangulieni kumbe ameona ngoma ilivo nzito akachochora. Badae akawapigia cm akasema ngoma hiyo ni nzito mana huyo bibi kazuiwa na watoto aliowaua huko anakotaka kwenda pia na kuku ndo mana analalamika kung'atwa na kufinywa.
Aliwashauri wamnyonge ila atakayemnyonga akubali kuteseka kama hivo ck ya mwisho wake. Wakakataa wote. Akawaagiza kumshikisha vitu mbali mbali huyo bibi ikiwemo uwele, ulezi mtama na mahindi kisha watafte mtot mdg wamshikishe kuku aingie naye chumbani walikomlaza mgonjwa.
Na aliwambia mkisikia kuku amelia mjue mgonjwa wenu amefariki. Ni kweli walifanya hivo na baada ya dak tano mtot yule kutoka nje walisikia kuku akihangaika ndani kwa kilio na badae kukawa kimya, walivyoingia ndani kweli walikuta kuku kafa na bibi tayari kafariki. Ule msiba watu hata hawakulia ilikuwa kama sherehe tu. Vijana walichimba kabuli hadi wakayakuta maji. Alafu enzi hizo hakuna jeneza kule kijijini. Mwili wake uliviringishwa tu ukafungwa na kamba kisha kushushwa.
Bibi alizikwa ila kesho yake walikuta kabuli limebomoka na kuna shimo lefu. Wazee wakubwa wakasema huyu hajafa ila kasepa ataenda kuishi sehemu nyingne. Kumbe mganga aliwaficha kutakachotokea kwa mtoto mana angewambia wasingekubali. So hiyo hiyo siku ya msiba mtot alipandisha mashetani na dak kadhaa tu akafariki. Mganga alipoulizwa aliongea tu kuwa nilitaka kuwatolea mateso ya huyo bibi tu na kiukweli huyo bibi hajafa kaenda kwingine na alisema hao watu hawafagi bila zindiko malumu.
Mwisho niseme tu. Tuishi vzr na wenzetu mana tuendako hatukujui na hatujui kifo kina maumivu gani, mana yote tunayoambiwa ni nadharia, hakuna anayejua ukweli.
Enjoy to dieNikiwaza kifo imani inazidi,inanifanya nijilazimishe kuzidisha unyenyekevu na kutokuwa na kiburi na kuongeza ibada.
Mimi huwa najiuliza yani itafika siku watu watasema wanaenda kumzika safuher,alafu sipati picha nimevaa sanda nyeupe,nafukiwa ardhini pale wanangu wanalia na mke wangu na wazee wangu wote wananililia wakati huo mimi sura yangu ipo kawaida tu umeshafumba macho.
Kiukweli kifo ni mawaida tosha kwa waumini kama alivyosema Mtume muhammad sala na salamu ziwe juu yake.
Ninachoamini kuwa siwezi kwenda kuteseka huko kwa kuwa nilikuwa nasali msikitini na kufanya mema sidhani kama nitaadhibiwa kwa hilo,ila ninachoogopa na kuamini ni kuwa nikifanya mabaya hapa duniani nitaenda kuadhibiwa huko kwa Mungu.
Kwa hiyo nikijikita na ibada za kumcha Mungu basi huu upande wa uchamingu ndo nakuwa nipo salama zaidi pale endapo nikifa kuliko upande wa kutakuamini Mungu.
Wakati Mwingine natamani kufa mapema nikaone hayo mazuri ya huko lakini nikifikiria kuwa nina mema machache naona Acha mungu aendelee kunipa uhai wa kufanya mema zaidi
Mzee baba anamtanguliza Mungu na kila siku anatuambia hivyo lakini unaona anachotufanyia?Fanya kazi wewe huku ukimtanguliza Mungu kwa kila jambo Mambo mengine mwachie yeye