Ukifiria kuhusu kifo chako unapata hisia gani?

Fanya kazi wewe huku ukimtanguliza Mungu kwa kila jambo Mambo mengine mwachie yeye
 
Nikiwaza kifo imani inazidi,inanifanya nijilazimishe kuzidisha unyenyekevu na kutokuwa na kiburi na kuongeza ibada.

Mimi huwa najiuliza yani itafika siku watu watasema wanaenda kumzika safuher,alafu sipati picha nimevaa sanda nyeupe,nafukiwa ardhini pale wanangu wanalia na mke wangu na wazee wangu wote wananililia wakati huo mimi sura yangu ipo kawaida tu umeshafumba macho.

Kiukweli kifo ni mawaida tosha kwa waumini kama alivyosema Mtume muhammad sala na salamu ziwe juu yake.

Ninachoamini kuwa siwezi kwenda kuteseka huko kwa kuwa nilikuwa nasali msikitini na kufanya mema sidhani kama nitaadhibiwa kwa hilo,ila ninachoogopa na kuamini ni kuwa nikifanya mabaya hapa duniani nitaenda kuadhibiwa huko kwa Mungu.

Kwa hiyo nikijikita na ibada za kumcha Mungu basi huu upande wa uchamingu ndo nakuwa nipo salama zaidi pale endapo nikifa kuliko upande wa kutakuamini Mungu.

Wakati Mwingine natamani kufa mapema nikaone hayo mazuri ya huko lakini nikifikiria kuwa nina mema machache naona Acha mungu aendelee kunipa uhai wa kufanya mema zaidi
 
kifo hakikuhusu mkuu,kinawahusu waliobaki.ukifa umekufa nothing else
 

Duniani kuna mambo.! [emoji1430][emoji1430][emoji1430][emoji1430]
 
Enjoy to die
 
Fanya kazi wewe huku ukimtanguliza Mungu kwa kila jambo Mambo mengine mwachie yeye
Mzee baba anamtanguliza Mungu na kila siku anatuambia hivyo lakini unaona anachotufanyia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…