Ukifiwa na dada yako, Je ushemeji kwa mumewe utaendelea?

Kwa hiyo mkuu utaacha kufuatilia maendeleo ya watoto wa marehemu dada yako?..

Binafsi sina mazoea na mashemeji ila watoto wakishaingia kwenye picha. Hata kama haziivi ni lazma muwe mna hata salamu kwa ajili ya watoto mkuu
Najaribu kuipima kwa mazingira ya kisasa ''kibepari'' baba yao anajiweza na amewapeleka bweni wote, na ameamua kuvuta kitu kipya. Wewe utakuwa unawasiliana nao kwa staili ipi?
 
Najaribu kuipima kwa mazingira ya kisasa ''kibepari'' baba yao anajiweza na amewapeleka bweni wote, na ameamua kuvuta kitu kipya. Wewe utakuwa unawasiliana nao kwa staili ipi?
Uwezo wa baba yao hauhusiani na nafasi yako kwa watoto wa dada yako mkuu.

Imagine watoto wamepoteza mama na uhakika wa care watayopewa katika familia mpya. Hakuna mwenye nayo

Hivyo, watoto watakimbilia wapi kama sio kwenye ndugu wa mama yao?..

Kingine mkuu, kwani kipindi cha likizo huwezi mpigia simu ili ukutane na watoto au la, kama shule inaruhusu visiting. Kwani haiwezekani kwenda kuwatembelea

Mbona ni simple mkuu
 
Ushemeji unaishaje sasa?Kwa hiyo na wapwa wako utabadilisha jina la kuwaita?
 
Naona upande wa mke itabidi watumie nguvu nyingi sana katika kuliweka sawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…