Hebu jibu swali hili...
1. Je, mtuhumiwa alikutana na mlalamikaji tarehe na saa tajwa huko jijini Mwanza, mahali tajwa (Rock City Mall-Ilemela), wakaingia kwenye gari ya mtuhumiwa na kubaki humo wakiwa wawili kwa muda?
2. Je, mtuhumiwa kwa jina na nafasi yake katika tarehe tajwa alisafiri kwenda Mwanza kutoka Bariadi Simiyu?
3. Je, anamtambua mlalamikaji kwamba ni mpenzi wake na kwamba walishawahi kutofautiana namna ya kuendesha mahusiano yao?
4. Je, Mtuhumiwa alipofika jijini Mwanza alielekea katika hotel iliyokaribu na Rocky City Mall na kumpigia simu mlalamikaji?
5. Je, ni kweli mlalamikaji ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha SAUT kilichoko huko Malimbe-Nyegezi?
6. Je, kama mtuhumiwa anathibisha alisafiri kutoka Bariadi-Simiyu hadi jijini Mwanza, alipokutana na msichana ambaye ni mlalamikaji kwa kudhalilishwa kingono kwa fedheha wakati akiwa hapo Rocky City Mall ndani ya gari lake binafsi alikuwa nafanya nini naye ndani ya hilo gari?