Ukigundua mke wako ni mshirikina na hampendi mama yako na ndugu zako, suluhisho ni lipi kwa misingi ya kikristo bila sheria za mahakama?

NetMaster

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
1,454
Reaction score
4,925
nataka tujuzane wakristo kwamba ndoa zetu hizi za kikristo zimekaa kinadharia sana kuliko kiuhalisia, sheria hazijajitosheleza na ndio maana watu hukimbilia mahakamani maana wanaona kabisa sheria za kikristo bado haziwezi kutatua hali zao.

Ukristo unaweza kutatua tatizo hili bila kutegemea sheria za mahakamani? Inatokea kwamba kwenye uchumba hata wa zaidi ya mwaka mzima mwanamke alikuwa na adabu ya hali ya juu, anawapenda ndugu zako, na tabia nyingine nzuri kumbe ni kujifanyisha tu ili umuoe.

Baada ya kunasa kwenye mtego wake mambo ya nabadilika.

~ Anaanza kuwa na kiburi.

~ Anaanza kuchukia na kuwatukana wazazi na ndugu zako.

~ Unakuja kupata stori huko kwao ni washirikina, ila kujificha huwa anaenda kanisani (wapo washirikina wengi sana wanatumia hii style)

Hapo mmeshakula kiapo kwamba mtaishi kwenye shida na raha mpaka kifo. Ngoma chambire moto!

Hii hali inatatuliwaje?
 
Kulingana na ukristo itabidi uendelee kuishi na mke anaetukana wazazi wako na ndugu zako, kazi kweli kweli !!

Tunaposema ukristo umepunjwa baadhi ya vitu tuwe tunaelewana,,

Maandiko yapo wazi ila ugumu wa watu kufata sheria za dini badala ya maandiko unawamaliza
 
Hii tunaitatu kwa maombi tu hamna kingine coz hakuna jambo linaloshindikana kwa mungu suluhisho ni kumuombea basi
Tabia hujenga mazoea, sio kitu cha kuvunjika kirahisi,

pia ili maombi yapige kazi inabidi mtu awe tayari ana imani, huwezi kumlazimisha mtu kuamini.
 
Ukristo unaweza kutatua tatizo hili bila kutegemea sheria za mahakamani? Inatokea kwamba kwenye uchumba hata wa zaidi ya mwaka mzima mwanamke alikuwa na adabu ya hali ya juu, anawapenda ndugu zako, na tabia nyingine nzuri kumbe ni kujifanyisha tu ili umuoe.

Baada ya kunasa kwenye mtego wake mambo ya nabadilika.
~ Anaanza kuwa na kiburi.
~ Anaanza kuchukia na kuwatukana wazazi na ndugu zako.
~ Unakuja kugundua ni mshirikina alieficha vifaa vyake juu ya dari

Hapo mmeshakula kiapo kwamba mtaishi kwenye shida na raha mpaka kifo. Ngoma chambire moto!

Hii hali inatatuliwaje?
Imeandikwa usimuache mwanamke mchawi aishi. Temana nae
 
Mambo kama haya yana ngazi katika utatuzi. Kwa kuwa umeshasema ni kiburi basi ni dhahiri umeshaongea naye na ameshindwa kukuelewa.

Moja, washirikishe wasimamizi wa ndoa yenu na kiongozi wa kiroho. Waite, ongeeni kwa pamoja. Washirikishe swala lako na mkanyeni aache ulozi na kiburi. Kama unajua alipoweka vifaa vyake, nenda katoe. Vichomeni moto. Nakusihi kuwa karibu sana na Mungu.

Pili, kama hatawasikiliza mrudishe kwao kisha itisha kikao cha pande zote mbili. Ongeeni kwa uwazi. Aache tabia yake. Walau kiburi kinavumilika ila si uchawi. Mmeshindwa kupata muafaka, abaki kwao huko huko.
 
Imeandikwa usimuache mwanamke mchawi aishi. Temana nae
Kumuacha mwanamke inabidi mpaka iwe kifo ama azini nje ya ndoa tu basiiii !!!

Enhee, na vipi kuhusu yeye kuwa a kiburi + kuwachukia na kuwatukana wazazi na ndugu zako ?
 
Pili, kama hatawasikiliza mrudishe kwao kisha itisha kikao cha pande zote mbili. Ongeeni kwa uwazi. Aache tabia yake. Walau kiburi kinavumilika ila si uchawi. Mmeshindwa kupata muafaka, abaki kwao huko huko.
Hilo sio suluhisho la kikristo, Ukristo ueweka wazi muishi pamoja mpaka kifo..
 
Ukristo umeweka hii misingi ikiwa kuna tatizo kwenye ndoa.
1. Neno la Mungu.
2. Maombi
3. Hekima

Sasa jiulize tu mleta mada, uko tayari kuendelea kuishi naye au huwezi? (HEKIMA)
Kama huwezi sepa zako, lakini huku ukifahamu tu huyo ni mkeo mpaka kifo kije kiwatenganishe.(NENO LA MUNGU)
 
Sasa jiulize tu mleta mada, uko tayari kuendelea kuishi naye au huwezi? (HEKIMA)
Kama huwezi sepa zako,
Imeandikwa muishi pamoja mpaka kifo (sio kumpeleka kijijini ama kumfukuza) , hizo sheria za kusepa umezitoa wapi ?

Halafu tuseme mmeachana mkiwa bado hamna mtoto na bado ni vijana, iamaanisha maisha yako yote huwezi kuoa na kupata mtoto mpaka kifo ?
 
Kumuacha mwanamke inabidi mpaka iwe kifo ama azini nje ya ndoa tu basiiii !!!
Biblia imeruhusu kuwa na wake wengi. Kama hutaki kumwacha kwa divorce mwache kwa kumsusa tu, oa mke mwingine.

Kuhusu kiburi na kuchukia nduguzo, huo ni uchawi kabisa sio ushirikina. Ukitaka kumrekebisha kwenye hilo piga mabanzi atanyooka, binadamu anatakiwa kufanya jambo lililo sahihi kwa umma na sio sahihi kwake, kwa hiyo ukimpiga kwa lengo la kumrekebisha, umma utakuona upo sahihi.
 
Imeandikwa muishi pamoja mpaka kifo (sio kumpeleka kijijini ama kumfukuza) , hizo sheria za kusepa umezitoa wapi ?

Halafu tuseme mmeachana mkiwa bado hamna mtoto na bado ni vijana, iamaanisha maisha yako yote huwezi kuoa na kupata mtoto mpaka kifo ?
Oa wake wengine wewe. Au la kama wewe ni askofu endelea kubaki na huyo mke mchawi.
 
Ukristo unaweza kutatua tatizo hili bila kutegemea sheria za mahakamani? Inatokea kwamba kwenye uchumba hata wa zaidi ya mwaka mzima mwanamke alikuwa na adabu ya hali ya juu, anawapenda ndugu zako, na tabia nyingine nzuri kumbe ni kujifanyisha tu ili umuoe.

Baada ya kunasa kwenye mtego wake mambo ya nabadilika.
~ Anaanza kuwa na kiburi.
~ Anaanza kuchukia na kuwatukana wazazi na ndugu zako.
~ Unakuja kugundua ni mshirikina alieficha vifaa vyake juu ya dari

Hapo mmeshakula kiapo kwamba mtaishi kwenye shida na raha mpaka kifo. Ngoma chambire moto!

Hii hali inatatuliwaje?
Neno linasema usimuache mwanamke mchawi aishi.Bs muombe Mungu amchukue.Au?
 
Ukristo unaweza kutatua tatizo hili bila kutegemea sheria za mahakamani? Inatokea kwamba kwenye uchumba hata wa zaidi ya mwaka mzima mwanamke alikuwa na adabu ya hali ya juu, anawapenda ndugu zako, na tabia nyingine nzuri kumbe ni kujifanyisha tu ili umuoe.

Baada ya kunasa kwenye mtego wake mambo ya nabadilika.
~ Anaanza kuwa na kiburi.
~ Anaanza kuchukia na kuwatukana wazazi na ndugu zako.
~ Unakuja kugundua ni mshirikina alieficha vifaa vyake juu ya dari

Hapo mmeshakula kiapo kwamba mtaishi kwenye shida na raha mpaka kifo. Ngoma chambire moto!

Hii hali inatatuliwaje?
Old fashion za ndoa zilikuwa nzuri sana, wazazi wa pande zote wanafanya background check kila upande, kuangalia Kama Kuna uchawi, magonjwa, uvivu, etc. Siku hizi unakutana barabarani unatangaza ndoa. Hayo ndo matokeo wanawake anaweza kula cover kwa miaka hata mitano akiwa na lengo na wewe. Ukishamweka ndani ndo anakunjua makucha yake. Very sad. Kama ni mchawi huna budi kumwacha utaharibu kizazi na generations yako. Maana atarishisha watoto wako Kama alivyorishishwa yeye.
 
Biblia imeruhusu kuwa na wake wengi. Kama hutaki kumwacha kwa divorce mwache kwa kumsusa tu, oa mke mwingine.
Ni kanisa lipi la kikrsto linaruhusu kufungisha ndoa ya mke zaidi ya moja ??
Kuhusu kiburi na kuchukia nduguzo, huo ni uchawi kabisa sio ushirikina. Ukitaka kumrekebisha kwenye hilo piga mabanzi atanyooka, binadamu anatakiwa kufanya jambo lililo sahihi kwa umma na sio sahihi kwake, kwa hiyo ukimpiga kwa lengo la kumrekebisha, umma utakuona upo sahihi.
Hio sheria ya kupiga ni wapi ipo kwenye ukristo ??
 
Ushirikina umepigwa marufuku kwenye biblia na ni moja ya kigezo kikubwa cha kuvunja ndoa endapo mmoja wenu akigundulika ni mshirikina.

Hivyo nenda kwa padri na ishahidi ndoa ivunjwe.
 
Back
Top Bottom