Ukigundua mke wako ni mshirikina na hampendi mama yako na ndugu zako, suluhisho ni lipi kwa misingi ya kikristo bila sheria za mahakama?

Ushirikina umepigwa marufuku kwenye biblia na ni moja ya kigezo kikubwa cha kuvunja ndoa endapo mmoja wenu akigundulika ni mshirikina.
Kitu cha kuvunja ndoa ni kifo na uzinzi nje ya ndoa, Ni vitu viwili tu!!
 
Sawa Mkuu.

Dawa yako wewe kulogwa tu.
Sio Tatizo langu, nataka tujuzane wakristo kwamba ndoa zetu hizi za kikristo zimekaa kimchongo sana, sheria hazijajitosheleza.

Hivi kweli uishi na mke anawatukana na kuwadharau ndugu na wazazi wako halafu mnasisitizwa muendelee kuishi pamoja,, kuna tofauti kati ya uvumilivu na upumbavu
 
Ukristo hauruhusu
1 Timotheo 4:3
wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli.
1 Tim 4:3 SUV

Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha; Mashemasi na wawe waume wa mke mmoja, wakiwasimamia watoto wao vizuri, na nyumba zao.
1 Tim 3:2‭, ‬12 SUV

Mashemasi na wawe waume wa mke mmoja, wakiwasimamia watoto wao vizuri, na nyumba zao.
1 Tim 3:12 SUV

Kama unasoma Biblia, hayo ndiyo maandiko, wake wengi wameruhusiwa. Usisikilize maneno ya manabii wa uongo wanaokukataza usio mke mwingine
 
Maandiko yanaruhusu na hili wengi tunalijua.

Ishu inapokuja ni kwmba, Je kuna kanisa lolote la kiksristo linayafata haya maandiko ??
 
Hata sheria ya nchi inatambua ndoa za wake wengi zitazofungwa kwa imani ya dini ya kikristo. Mchawi wako ni kipengele ulichokata kwenye cheti cha ndoa, kama ulisema ndoa itakuwa ya mke mmoja ndio ujilaumu hapo. Biblia imesema ishi nao kwa akili, mnyooshe kisaikolojia na kifizikia
 
Hata sheria ya nchi inatambua ndoa za wake wengi zitazofungwa kwa imani ya dini ya kikristo.
Nenda kasome upya sheria ya ndoa ya Tanzania..( Marriage act)

Ndoa za kikristo ni mke mmoja tu
 
Maandiko yanaruhusu na hili wengi tunalijua.

Ishu inapokuja ni kwmba, Je kuna kanisa lolote la kiksristo linayafata haya maandiko ??
Sasa kama mnalijua mnasita sita nini kufuata maandiko? Yaani unaacha kufuata biblia na unaanza kufuata katiba za kanisa?? Hivi ni vichekesho

Kuhusu uwepo wa makanisa ya kikristo yanayotekeleza hilo, yapo. Moja lipo kihesa kilolo iringa na lingine lipo makabe mbezi, yana waumini wasiozidi 10
 
Uwe unaongea kwa ushahidi tafadhali, Ni makanisa yapi hayo ??
 
Nenda kasome upya sheria ya ndoa ya Tanzania..( Marriage act)

Ndoa za kikristo ni mke mmoja tu
Tatizo ni kuwa unataka ligi na sio msaada. Anyways, kama upo tayari kujifunza ili unapoweka ligi kwingine uwe konki, nakufunza

Ukisoma kifungu husika kwenye sheria ya ndoa kinasema kuwa
S. 10 (2) (b) in any other case, be presumed to be monogamous, unless the contrary is proved

Kwa tafsiri ya kuwa wakati wa kuoana, hata kama ilikuwa ni ndoa ya kikristo ila parties wakaamua kuwa itakuwa ya wake wengi, kwa kukata zile zisizohusika, basi ndoa itakuwa ya wake wengi na kutambulika kisheria.

Kaangalie hicho kifungu na ueleze wewe hiyo ya kuwa ukristo unataka mke mmoja imeandikwa wapi.
 

Attachments

  • Screenshot_2022-11-30-17-57-36-306_cn.wps.xiaomi.abroad.lite.jpg
    107 KB · Views: 2
Mkuu umechanganya kiingereza tu

Tafsiri sahihi ya hapo ni kwamba,

Ndoa yoyote iliyofungwa Tanzania kabla au baada ya sheria ya ndoa kutungwa.

a. kama ni ya kiislamu au ya mila za Tanzania, itachukuliwa ni ndoa inayomruhusu mwanaume kuongeza mke

b.kwa ndoa za aina nyingine (ikiwemo ya ukristo), itachkuliwa kwamba ni ya mwanaume kutoruhusiwa kuongeza mke hadi kuwe na ushahidi ithibitishwe sivyo, hapa zipo ndoa za kimila za wakenya, waganda, n.k. hawa inabidi wapeleke vyeti vya ndoa zao ama nyaraka zozote zinazowapa ruhusa kuongeza mke.

Kwa lugha nyepesi ndoa ya kikristo inachukuliwa ni ya mke moja na mme moja, FULLSTOP!!


(2) A marriage contracted in Tanzania whether contracted before or after the commencement of this Act, shall–
(a) if contracted in Islamic form or according to rites recognised by customary law in Tanzania, be presumed, unless the contrary is proved, to be polygamous or potentially polygamous; and
(b) in any other case, be presumed to be monogamous, unless the contrary is proved.
 
Kwenye a na b kote kuna neno PRESUMED, lakini kwenye tafsiri ya Kiswahili uliyoweka, hilo neno umelitumia kwenye (a) tu, kuwa 'ITACHUKULIWA' halafu kwenye (b) ukaamua kutoliweka hilo neno, na hilo ndio msingi wa TAFSIRI NZIMA, liweke halafu uone maana yake kama inabaki hiyo unayoamini.
 
Kwenye a na b kote kuna neno PRESUMED, lakini kwenye tafsiri ya Kiswahili uliyoweka, hilo neno umelitumia kwenye (a) tu, kuwa 'ITACHUKULIWA' halafu kwenye (b) ukaamua kutoliweka hilo neno, na hilo ndio msingi wa TAFSIRI NZIMA.
Kifungu a kinahusisha ndoa za kiislamu na zile za mila za Tanzania, Sheria inapresume hizi ndoa mwanaume anaweza kuongeza mke

kifungu b kinahusisha ndoa ambazo sio za mila za kitanzania au kiislamu, Sheria ina presume hizi ndoa (ikiwemo ya kikristo) mwanaume hawezi kuongeza mke mpaka kuwe na ushahidi kwamba sheria za ndoa zao zinaruhusu mwanaume kuongeza mke, mfano kama mtu ndoa yake haijtajwa kwenye kifungu (a) ila anaruhusiwa kuongeza mke, hapa anaweza kwenda kupeleka ushahidi mahakamani ili aongeze mke wa zoada, mfano kuna watu wa nje wana dini zao ambazo si uislamu lakini wanaruhusiwa kuongeza mke.
 
Ukristo ni zaidi ya kujulikana wewe unaamini nini, ukristo ni maisha. Ukristo unamfundisha mtu kuwa na mahusiano kibinafsi na Mungu, Kama mtu alikuwa anajifanyisha kuwa ana tabia nzuri kumbe sio, maana yake kabla ya kuingia kwenye ndoa inatakiwa Mungu awe amekuonesha hicho kitu.

Nakuhakikishia Mungu anaongea na watu katika dunia hii hii iliyojaa uovu, na hata ukiwa na mahusiano naye hata kidogo tu, kama ukimpa nafasi anaweza kuzuia usiingie kwenye huo mtego.

Shida ni kwamba wengi hawana mahusiano na Mungu lakini wakiingia kwenye matatizo ndo wanataka Mungu awajibike.
Ila ikitokea huyo mtu hakuwa amejifanyisha na kwamba Mungu kwa mapenzi yake kamili aliruhusu uingie na huyo mtu kwenye ndoa, basi hakika jua tu kwamba Mungu mwenyewe atalimaliza hilo muda si muda. Ni suala la kuwa mwombaji, kuwa mstahimilivu na kukaa karibu na uwepo wake kila wakati.

1Wakorintho 10:13 "Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili."
 
Maneno haya mengi hayatatui matatizo ya kwenye ndoa za kikristo,

Sikiaga tu mtu fulani ana matatizo, usiombee yakukute!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…