Ukihitaji usingizi mzuri, fanya yafuatayo...

Ukihitaji usingizi mzuri, fanya yafuatayo...

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
a) Jiwekee msimamo ratiba yako ya kulala kama hakuna dharura nyingine iwe saa fulani Mpaka saa fulani. Hili ndo jambo kubwa la kwanza.

b) Mchana usichoke choke kizembe fanya fanya mazoezi mapema tu kabla haijaingia usiku sana.

c) Punguza au jiepushe na pombe, caffeine, energy drink, sigara sigara.

d) Kitanda kitumie kwa ajili ya kulala tu au mambo ya faragha yale na si vinginevyo usizoee sana kuchart, game, movie, kula ufanyie kitandani labda kama hali ya hewa nje haisomeki... Toka outdoor huko ndo kwenye afya.

e) Kula kiasi tu sio lazima umalize sahani la wali usiku kama ni greens Sawa unaweza kumaliza.

f) Chumba ukiweza kukiweka Safi hakina mambo mengi itakuwa vizuri yaani room ya kulala ina taa za giza na mziki na kitanda tu na kabati moja tu

e) Usijiegeshe kitandani ukiwa hulali. Kama huna usingizi ni bora kakae au katembee.

Hii ni itawasaidia wale tu ambao wanahitaji kujua ni vipi usingizi mzuri ambao ni dawa pia unaweza kupatikana Kwa kujaribu njia Hizo tajwa.
 
Mimi nafanyanga hivi napata usingizi mzuri
FB_IMG_1718908506735.jpg
 
Usingizi mzuri unaletwa na afya njema ya mwili na akili. Ule ushibe vizuri vyakula vyenye virubisho vinavyohitajika mwilini. Cha mwisho ni shoo nzuri ya adabu uliyopiga kwa mwenza wako inaleta usingizi mzuri sana
 
siku hizi usingizi umekuwa adimu sana kwa watu wengi hususani wachakarikaji
 
Back
Top Bottom