Ukiitwa fursa jua mara nyingi fursa ni wewe! Aina 15 za Scam unazopaswa kuzijua

Ukiitwa fursa jua mara nyingi fursa ni wewe! Aina 15 za Scam unazopaswa kuzijua

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
25,030
Reaction score
61,298
Online Scam
1. Phishing
unapata email Dear Customer account yako itafungwa ndani ya dakika 30. Wewe unaogopa, unaingiza password... dakika mbili baadaye akaunti si yako tena.

2. Fake Giveaway
Hongera! Umeshinda iPhone 17 Pro Max na hukushiriki shindano lolote. Mwisho unaambiwa lipa delivery kwanza. ukilipa tu Simu huioni, hela huioni.

3. Fake Shopping
Unaona iPhone ya milioni 4 inauzwa laki 3. Unasema Leo Mungu amenikumbuka.Kumbe aliyekukumbuka ni tapeli.

4. Romance Scam
unaanzisha mahusiano facebook au instagram baada ya wiki anakwambia Baby I love you.Wiki ya pili Baby, nitumie laki moja, mama anaumwa.Ukituma, mama anapona... lakini mpenzi anakula kona..

5. QR Code Scam
Unaambiwa Scan hii upate ofa. Unaiscan... ofa pekee unayopata ni balance yako kuwa sifuri.

6. Tech Support Scam
inakuja alert Kompyuta yako ina virus Wewe unaikabidhi kwa fundi wa mtandaoni. Baada ya dakika chache virus vimetoka na hela benki zimeondoka.

phone na sms scam
7. Fake Bank Call
Sisi ni kutoka benki tupe OTP tu kulinda akaunti yako. Ukimpa OTP kweli akaunti inalindwa... ila inalindwa na wao.

8. Fake Delivery
Mzigo wako umefika lipa delivery.Wewe hujaagiza chochote lakini unalipa kwa matumaini. Mzigo hauji, stress ndiyo inakuja

9. One Ring Scam
Simu inaita namba ngeni ya ajabu ajabu sekunde moja halafu inakata. Wewe unaipigia tena Dakika tano baadaye unajiuliza salio limeenda wapi.

10. Prize Call
Hongera! Umeshinda milioni 50. Halafu wanakuambia Tuma elfu 50 za processing Ukituma wanakuzawadia block.


Money scam
11. Pyramid Scheme
Unaambiwa Utajiri ni kuingiza watu wawili, wao waingize wawili..Mwishowe unaishia kuwa motivational speaker bila hela.

12. Ponzi Scheme
Mwanzo watu wanalipwa kweli. Wewe unaona na kusema Hii ndiyo deal.Baada ya kuwekeza, kampuni nayo inatoweka.

13. Fake Investment
Wekeza leo, ndani ya mwezi utapata faida 300%. Hata benki, migodi na mafuta hayawezi kuahidi hiko kiasi. tamaa ikikuzidi, pesa zinaenda.

14. Fake Crypto Platform
Unaona kwenye app umeingiza milioni 1 zinaonekana zimekuwa milioni 20. Ukitaka kutoa wanaomba withdraw fee. Ukilipa kwaheri..

15. Advance Fee Scam
Umepata kazi dubai lipa registration kwanza. Ukishalipa kazi pekee unayopata ni kutafuta wa kukukopesha hela ya kula.


ukiona umeitiwa fursa jua fursa ni wewe


​

 
Tajiro namba 16, ingekaa Forex trading ingekua poa zaidi. 😊
 
Back
Top Bottom