Ukiitwa na Rais Ikulu Kwa mazungumzo rasmi ukakataa utafanywa nini?

Tangu mwanzo Chadema walishaomba kuonana na Rais! Kwa bahati nzuri Rais mwenyewe akianza kuonana na Makamu Mwenyekiti Mh. Tundu Lissu kule Ubelgiji, wiki chache zilizopita!

Na jana ameonana na Mwenyekiti mwenyewe wa chama Mh. Mbowe mara tu baada ya kutolewa mahabusu, kutokana na ile kesi yake ya mchongo! Na taarifa rasmu imeshatolewa juu ya mazungumzo yao.

Nadhani katika hili, malengo ya Chadema yametimia kwa 100%.
 
Aseee [emoji2955][emoji2955]
 
Hajaitwa, yeye ndiye alikua akifanya maombi mara kadhaa ya kuonana na Rais, aliongea hata kwenye vyombo vya habari. Maombi yake yamekubaliwa
 
Rais wetu tunampenda. Kwa pamoja tuijenge nchi yetu. Mpango wa kumfunga na kumtesa Mh Mbowe ulisukwa wakati wa utawala wa yule mzee. Mama hahusiki.



Kuitwa na kuongea na Rais wa nchi ni heshima kubwa. Ni jambo lenye maslahi kwa Taifa.


JESUS IS LORD
 
Kwani kuna mtu amesema ukikataa wito wa ikulu utapata matatizo? Inamaana Mbowe katishiwa asipoenda ikulu?
 
Ila usije kua unataka kusema mbowe kaitwa ikulu. Kwa kauli ya samia mwenyewe mbowe ndio kaomba kuonana na samia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…