Ukija kuamua kuanza kulima utalima zao gani?

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Nimeona jinsi wakulima wakizungumzia mwenendo mbaya wa mazao yao Shambani mfano wa kulima wa Kanda ya Kati wengi walichelewa kumpanda hivyo jua la mwezi wa tatu limezingua kufanya mimea isinawiri huko kusini mvua zinapiga nyingi TOKa mwaka Jana na Wao athari ni kuharibika Kwa mazao mfano ufuta imewabidi wapande Mara mbili.

Mimi binafsi naona ni heri kujichanganya mwakani nikajipanga nikajitafuta niwe na kama laki Sita nikodishe Shamba heka hata nne nipande karanga au Maharage na sio mazao marefu marefu kama mahindi au ufuta yanayohitaji palizi, Madawa, usimamizi, booster, mbolea n. K.

Karanga hata usipouza sokoni Kwa bei ya jumla bado una uwezo wakuwauzia wajasiriamali wadogo mtaani na ukapiga Hela same to Maharage au kunde yaani hukosi Baraka baraka za ardhi.

Kwa kifupi ni hapa ni mwendo wa kulima mazao mafupi mafupi tu ya kuyamudu mfano mwingine ni mamboga mboga ya bustani ya kumwagilia.
 
Karanga hata mim nawaza Sana kuzilima ukiweza hata heka kumi hukos gunia Mia za debe sita na hazihtaj mbolea kama ilivyo kwa mahind! Tatzo sis tunataka sifa za kulima mahind hata km weng wanayalima! Npo songea mahind yameitika mashamban sio mchezo na kwa hii hali inabd serkali iinglie Kati hakuna Bei mwaka huu! Nnavyoona mim mpunga ndio kila kitu ukipata ardh nzur na kukawa na mvua za kuaminika soko liko Waz watu wanakula wali sanaaaa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…