Ukijaza gesi ya Tsh. 6,000 kwenye Bajaji unapata faida ya Tsh. 50,000, ila kupata faida hiyo kwa Mafuta inabidi ujaze ya Tsh. 20,000

Ukijaza gesi ya Tsh. 6,000 kwenye Bajaji unapata faida ya Tsh. 50,000, ila kupata faida hiyo kwa Mafuta inabidi ujaze ya Tsh. 20,000

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
7,899
Reaction score
10,415
Huenda umekuwa ukitumia usafiri wa Bajaji (pikipiki ya matairi matatu) na kudhani kuwa zote zinatumia mafuta ya petroli pekee.

Hata hivyo, hali imebadilika! Sasa kuna Bajaji zinazotumia Gesi Asilia Iliyoshindiliwa (CNG), ambayo ni nafuu na yenye faida kubwa kwa madereva na wamiliki wa vyombo vya moto.

Matumizi ya gesi asilia katika vyombo vya moto, hususan Bajaji, yameongezeka kwa kasi sana, hasa katika Mkoa wa Dar es Salaam. Hii ni kwa sababu gesi inapatikana kwa gharama nafuu ukilinganisha na petroli, hali inayosaidia madereva na wamiliki wa Bajaji kupunguza gharama za uendeshaji na kuongeza faida zao.

Kwa mfano, ukijaza gesi ya Tsh 6,000 kwenye Bajaji, unaweza kupata faida ya Tsh 50,000, ilhali dereva anayejaza petroli anahitaji Tsh 20,000 ili kufikia faida hiyo na bado kuna uwezekano asifikie kiwango hicho cha faida.

Miongoni mwa sababu zinazochochea ongezeko la Bajaji za gesi asilia ni:
  1. Gharama Nafuu ya Nishati – Gesi ni rahisi zaidi ukilinganisha na petroli, hivyo inapunguza gharama za uendeshaji.
  2. Faida Kubwa kwa Madereva – Kwa matumizi sawa ya mafuta, dereva wa Bajaji inayotumia gesi hupata faida kubwa zaidi kuliko yule wa petroli. Awali, Bajaji iliyotumia petroli kwa lita moja ilitembea kilomita 25, lakini kwa gesi asilia, kilo moja inaweza kutembea kilomita 45. Hii inawasaidia madereva kupunguza matumizi ya mafuta na kuongeza faida. Bajaji zinazotumia gesi asilia zinaweza kuongeza mapato kwa asilimia 20.
  3. Kampuni za Kifedha Zinakopesha Bajaji za Gesi – Kampuni zinazotoa mikopo kwa Bajaji sasa zimeanza kukopesha Bajaji zinazotumia gesi, jambo linalochochea matumizi yake zaidi.
Kutokana na faida kubwa za gesi, baadhi ya wamiliki wa Bajaji zinazotumia petroli wameamua kubadili mifumo ya vyombo vyao ili viweze kutumia Gesi Asilia Iliyoshindiliwa (CNG). Ubadilishaji huu unafanywa katika karakana maalum za mafundi wazawa maarufu kama ‘conversion centers’.

Lakini pia wazalishaji wa Bajaji wameitikia wito wa kuhamasisha matumizi ya nishati safi kwa kuzalisha Bajaji zinazotumia mfumo wa nishati mbili (dual fuel system) – Gesi asilia na Petroli.

Kampuni ya Bajaji Auto Tanzania imeanza kuzalisha Bajaji zenye uwezo wa kutumia gesi asilia na petroli kwa wakati mmoja, tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

Kampuni ya Cars & General Trading Ltd, pia imeamua kujikita zaidi katika kuuza Bajaji za gesi kutokana na faida kubwa wanayopata wateja wao.

Imeandaliwa na Bright and Genius Editors:
🌐 Wasiliana nasi kupitia
☎️ Whatsapp kwa namba +255687746471 / +255612607426 au
📧 Kupitia barua pepe bandg.editors@gmail.com.
 
Mbona ujaweka na garama ya kubadili bajaji ya petrol kutumia gas
Unaweka faida bira kuweka garama za kupata faida iyo

Tofauti na izo bajaji zilizotengenezwa maalum kutumia gesi je kuna madhara gan ya kubadili kitu kinachotumia petrol kutumia gas
 
Ni kweli kuna jamaa yangu ndio kazi yake, aliniambia hivyo pia. Changamoto zake;
1. Spark plugs zinakufa sana, yaani wanabadilisha sana plugs.
2. Hazina nguvu hasa kwenye miinuko.
3. Waki-switch kwenye petrol carburettor zinashindwa kufanya kazi kwa ufanisi(kumbuka hawawezi kutumia gas mda wote coz availability ni ndogo).
 
Je mpk sasa kuna vituo vingapi vya kujaza gas ⛽ station nchi nzima?
KAZI ni kipimo cha UTU
 
Back
Top Bottom