POTOSHI Ukijenga kabla ya ndoa, ukioa nyumba ni ya wote mke na mume?

POTOSHI Ukijenga kabla ya ndoa, ukioa nyumba ni ya wote mke na mume?

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
Wakuu haka kavideo kanashtua kidogo.

Uhalisia ni upi?

1792139738988.png
 
Tunachokijua
Oktoba 15, 2026 kupitia mitandao ya kijamii kumekuwa na video inayosambaa iliyochapishwa na chombo cha habari cha Nuru FM ambapo mgeni wao Mwanasheria, Flora Shija alikuwa akieleza kuwa ukijenga nyumba kabla ya ndoa, ukioa nyumba inakuwa ya wote.

JamiiCheck imewasiliana na wakkili kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), William Maduhu ambaye amefafanua kwa kueleza kuwa;

Hiyo si kweli, kuna watu wengi wanapotosha sana kuhusu jambo hilo, Sheria ya Ndoa ipo wazi.

Mali ulizozikuta zinabaki kuwa za mwenza isipokuwa kama Mwanandoa ambaye hakuhusika awali awe alifanya maendelezo kwenye mali hiyo au hizo.

Mfano ni kesi ya Bi. Hawa Mohamed ambayo Mahakama ya Rufaa ndiyo iliweka huu msingi Mwaka 1985.

Sheria ya ndoa inaeleza

The Law of Marriage Act, Sura ya 29, Toleo Lililorekebishwa la 2023

Kifungu​

(1) Mahakama ina mamlaka, wakati wa kutoa au baada ya kutoa amri ya kutengana kwa wanandoa au talaka, kuamuru mali yoyote iliyopatikana na wanandoa wakati wa ndoa kupitia juhudi zao za pamoja igawanywe kati yao. Mahakama inaweza pia kuamuru mali hiyo iuzwe na mapato yatokanayo na mauzo yagawanywe kati yao.

(2) Katika kutumia mamlaka hayo, Mahakama itazingatia mambo yafuatayo:

(a) Mila na desturi za jamii ambayo wanandoa wanatoka.

(b) Kiwango cha mchango wa kila mmoja katika kupata mali hizo, iwe kwa fedha, mali nyingine au kazi.

(c) Madeni yoyote ya mmoja wa wanandoa yaliyokopwa kwa manufaa yao ya pamoja.

(d) Mahitaji ya watoto wa ndoa hiyo, ikiwa wapo.

Kwa kuzingatia mambo hayo, Mahakama itaelekea katika kugawa mali kwa usawa kati ya wanandoa.

(3) Kwa madhumuni ya kifungu hiki, mali zinazochukuliwa kuwa zimepatikana wakati wa ndoa zinajumuisha pia mali iliyokuwa inamilikiwa na mmoja wa wanandoa kabla ya ndoa, lakini ambayo iliboreshwa kwa kiwango kikubwa wakati wa ndoa na mwenzi mwingine au kupitia juhudi zao za pamoja.
Je? Iwapo mke ndio alijenga kabla ya kuoana napo itakuwa ya wote?
 
Back
Top Bottom