Ni saa mbili na madakika, salaam ndugu wanajukwaa!
Uswahilini kuna mengi! Kuna kupigana juju, umbea, majungu, na mengine mengi.
Kuna shida moja ambayo huwapata wakazi wa uswahilini, na hii huwapata watu ambao wamejenga kwenye viwanja visivyopimwa!
Yaani hivi ni viwanja vya vipimo vya macho na mashahidi kadhaa, mambo yanaanza kuharibika unapoanza kufanya ujenzi. Jirani wa kushoto analalama akisema umekula kiwanja chake, huyu wa kulia naye anaanza kumega ardhi ya upande wako kidogo kidogo ilimradi taflani!
Ukinunua kiwanja uswahilini kabla ya ujenzi anza kuzungusha uzio kwenye mpaka wako na hapo ndipo uanze kujenga, la sivyo watu wataanza kulilia ardhi huko mbeleni.