Ukikamua tunda ili kupata juice unapoteza nyuzinyuzi zake ( Fibers)

Ukikamua tunda ili kupata juice unapoteza nyuzinyuzi zake ( Fibers)

Baba Vladmir

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2021
Posts
373
Reaction score
627
Ukikamua tunda ili kupata juice unapoteza nyuzinyuzi zake ( Fibers).

FAIDA ZA KULA FIBERS;
Mosi
, Fibers ni chakula cha chembe hai za utumbo mpana. Utumbo mpana huzibadili fibers kuwa mafuta yajulikanayo kama BUTYRIC ACID. Mafuta haya ndo chanzo cha nishati kwa chembe hai za utumbo mpana ( Fibers undergo fermentation into butyric acid , which is metabolised by colonocytes for their energy source).Hivyo basi fibers hupunguza risk ya saratani ya utumbo na uwezekano wa kupata ugonjwa wa bawasiri.

Pili
: Fibers huongeza ujazo wa mabaki kwenye tumbo na kuufanya utumbo ujikamue( Peristalsis) hivyo kusaidia kupata choo.Njia nzuri ya kuepuka kukosa choo katika tiba ni pamoja na ulaji wa chakula chenye fiber nyingi.Kwa sasa kuna vidonge pia vya fibers.

Je, UNYWAJI WA JUICE NI HATARI?

Jibu ni hapana( hapa ninamaanisha juice ya asili siyo ya kusindikwa kiwandani)
Kwenye Juice kuna kiwango kikubwa cha vutamin C kuliko ukila tunda. Ingawa una miss fibers( nyuzi)
Vitamin C hu huondoa sumu mwilini ( neutralizes free radicals which are generated in mitochondria)

Kwa hiyo, aliyekunywa juice nyingi kapata vitamin C nyingi lakini pia anaweza kuvuka kiwango cha matumizi ya sukari kwa siku.

Matumizi ya sukari hutegemea umri , jinsia , level ya mazoezi na hata utimamu wa mwili( metabolic state)

NOTE Pigania afya yako. Jishughulishe. Watu wanaorejea katika afya bora ni wale wanaofanya juhudi za dhati katika kuleta mabadiliko chanya na ya kudumu katika mitindo yao ya maisha.
🙏🙏🙏
 
Back
Top Bottom