Ukikonda nyama zinaenda wapi?

Ziroseventytwo

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2011
Posts
8,581
Reaction score
15,618
Nimemaliza kula muda mfupi uliopita. Nipo na kijana wangu ni mvulana wa miaka kumi. Ni mnene sana, na anakula kweli kweli. Jina lake la utani ni kibakuli kwa sababu ya unene wake. Ref (kibakuli wa kaole) yupo darasa la tatu. Nimemwambia mwakani ntampeleka akakae boarding school kwa ajili ya kujiandaa na mitihani ya darasa la nne.
Kaniuliza swali la kipuuzi lakini kwangu ni gumu. Kaniuliza hivi baba mimi nikikonda hizi nyama mwilini zinaenda wapi? Kwa kweli sikuwa na jibu zuri la kumpa. Nikaishia kujiuma uma.

Nyama kwenye mwili wa mtu kibobge/mnene zinaenda wapi ikiwa mtu anakonda?
 
Kunenepa chakula ulacho hakitumiki chote na hutunzwa mwilini kama mafuta. Kukonda mwili haupati chakula cha kutosha km kushindwa kula kwa ugonjwa, mahitaji makubwa ya nishati mwilini kwa mazoezi nk. Hivyo mwili hutumia akiba uliojiwekea kutimiza majukumu ya ww kuishi kipindi una pata lishe ndogo.
 
Mwilini kuna Sukari mafuta na protein.Vyote vinaweza kusagwa ili kutoa energy kwa matumizi ya mwili.

Mwili unaanza kusaga sukari, kama hakuna sukari itasaga mafuta na kama hayapo basi itasaga protein.

Ikifika hatua ya kusaga mafuta na/au protein ndipo mtu anaanza kupungua.

NB:Kiswahili ni kigumu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…