Ukikuta meseji ya kimapenzi kwenye simu ya mpenzi wako, kipi cha kwanza cha kufanya?

Ukikuta meseji ya kimapenzi kwenye simu ya mpenzi wako, kipi cha kwanza cha kufanya?

kilamba lamba

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2020
Posts
427
Reaction score
738
Natumai mu wazima sana.

Utafanya nini cha kwanza unapokuta meseji ya kimapenzi ya mtu mwingine kwenye simu ya mpenzi wako .je utafatilia kimya kimya ujue ukweli, au utaamua kumkalisha chini mpenzi wako na kumwambia ukweli?
 
Ngoja wenye wivu n mali zao waje kutoa muongozo, binafsi sishiki simu ya mpenz wangu nae yangu hashiki fullstop,Ila kama naiona huwaga sina mambo mingi
 
Cha kwanza ntafuatilia ukweli kimya kimya mpaka niujue ukweli wote. Pili nikishajua ukweli ntamtumia hiyo conversation nikiwa nae nione atareact vipi.. hapo ndio ntajua zaid cha kufanya.

NB: usupekua simu ya mwenza wako labda kama unatafuta sababu ya kumwacha na ni hatari kwa afya yako.
 
Huo ukimya kimya ndo unawaua nakuwapa magonjwa ya moyo.

WEWE UKISHAJUA , BASI HAKIKISHA UMEFANYA AJUE KUA UMEJUA ANACHEPUKA.

baada ya hapo, usimpe hata muda wa kujitetea, fanya mambo yako kimya kimya


MWANAMKE AKISHAAMUA KUCHEPUKA, AMINI NAKUANBIA, HATA UMPE KIPIGO VIPI, HATA UMGOMBEZE VIPI, HATA UFANYEJEE, KAMA HAJAAMUA MWENYEWE, ATALIWA TU.

Zaidi [emoji116]
 
Nampa Hongera naendelea na yangu!!!!!

Dunia ina binadamu wengi sana unaweza kupata sehemu za siri kwingine ukafurahia maisha sasa ya nini ujitie presha uishie kupata vidonda vya tumbo ????
 
Natumai mu wazima sana.

Utafanya nini cha kwanza unapokuta meseji ya kimapenzi ya mtu mwingine kwenye simu ya mpenzi wako .je utafatilia kimya kimya ujue ukweli, au utaamua kumkalisha chini mpenzi wako na kumwambia ukweli .?
Kuwa makini na chat za wanawake, ukae ukijuwa wanawake walioshibana wanaitana mpenzi.

Sasa usikurupuke kukuta neno mpenzi ukalipuka kumbe mwenzako anachat na shoga yake.

Cha msingi achana na simu ya mwenza wako.

Simu siyo sharing device.
 
Natumai mu wazima sana.

Utafanya nini cha kwanza unapokuta meseji ya kimapenzi ya mtu mwingine kwenye simu ya mpenzi wako .je utafatilia kimya kimya ujue ukweli, au utaamua kumkalisha chini mpenzi wako na kumwambia ukweli .?
Unatafuta nini kwenye simu ya mtu mkuu utakufa siku sio zako
 
Ulipaswa uandike where have you been?

Samahamani lakini sina nia mbaya ya kukukwaza.
Wala usijali kabisa mkuu! It's ok kurekebishana mistakes and i take it in a positive way. Sasa mimi nilitaka kumuuliza "anaendeleaje" and not where he has been as you said, so how it was supposed to be?
 
Back
Top Bottom