Ukikuta ofisi imebandikwa hivi, "Hatupokei Rushwa" Usirogwe ukajichanganya

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Tembea popote, ingia ofisi yoyote lakini ikitokea umeingia katika ofisi iliyobandikwa maneno ya (Hatupokei Rushwa) Usirogwe kabisa ukajichanganya ukayaamini!

Hata Ukienda kituo cha polisi ukakuta bandiko kubwaa la HAKI ZA RAIA usipoteze muda kusoma!

We shughulika na kilichokupeleka!

Siku moja nilitembelea kituo cha polisi nikamkuta jamaa anasoma bango la HAKI ZA RAIA!

Nikamwambia BRO! "Ukimaliza kusoma ingia ndani wakakunyooshe" Akasema kivipi!?

Nikamwambia Soma hapo palipo andikwa kwamba "Afisa wa polisi anaweza kutumia nguvu ya kadri"

Hii nguvu ya kadri inayotamkwa inategemea na misuli ya mpigaji!

"Nguvu ya kadri ya baunsa ni kiama kwa mnyonge"

Usiyaamini hayo maneno! Ondoka!
 
Jeshi la wananchi halipokei rushwa nina uhakika

Watu waliopo ndio hupokea maana Jeshi sio kitu tangible.

Alafu ujue tu huoni wakichafuka kwa sababu hawana intereaction ya moja kwa moja na jamii.

Otherwise ni wale wale tu uliza waliowahi kushiriki au kufatilia operations zinazohusisha wanajeshi hata kuondoa wafugaji kwenye hifadhi tu then urudi hapa uje kufuta sentensi yako na uombe radhi kwa kutudanganya usiku wa leo.
 
Kuna ofisi moja kwenye mlango wameandika hakuna nafasi za kazi wa internship,ila na jamaa yangu alipata internship kwa michongo tu.

Bongo nyoso
 
Kuna ofisi moja kwenye mlango wameandika hakuna nafasi za kazi wa internship,ila na jamaa yangu alipata internship kwa michongo tu.

Bongo nyoso
Ndo ukiona bandiko lisome kinyume nyume
 
UKIONA BANGO limewekwa kwamba HATUPOKEI RUSHWA Jiulize kwanini wasingebandika kwamba tunatoa huduma haraka?
Kitendo cha kubandika neno HATUPOKEI RUSHWA Ni ishara ya Kutowajibika!
Sheria zipo ili zivunjwe
 
UKIONA BANGO limewekwa kwamba HATUPOKEI RUSHWA Jiulize kwanini wasingebandika kwamba tunatoa huduma haraka?
Kitendo cha kubandika neno HATUPOKEI RUSHWA Ni ishara ya Kutowajibika!
Sawaaa
 
tutofautishe RUSHWA na TAKRIMA ,pengine TAKRIMA inawachonganisha jeshi la polisi na raia

Inapotolewa elimu kuhusu rushwa na TAKRIMA isiachwe itolewe...
 
tutofautishe RUSHWA na TAKRIMA ,pengine TAKRIMA inawachonganisha jeshi la polisi na raia

Inapotolewa elimu kuhusu rushwa na TAKRIMA isiachwe itolewe...
Rushwa ni RUSHWA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…