KWELI Ukikutana na Simba silika ya kushambulia huongezeka ikiwa umewageuzia mgongo

KWELI Ukikutana na Simba silika ya kushambulia huongezeka ikiwa umewageuzia mgongo

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1



1776164121959.png
 
Tunachokijua
Simba ni wanyama wa pekee ambao kishindo cha mngurumo wao ambao huweza kusikika hadi umbali wa kilomita nane, huku wakiwa wakiwa ndiyo jamii ya paka pekee wanaoishi kwenye makundi (pride) na kula wastani wa mara mbili tu kwa wiki.

Licha ya kupatikana zaidi Afrika, idadi ndogo ya simba wa Asia bado wanaishi nchini India, na wenzao wa Uganda wanajulikana kwa kipaji cha kipekee cha kupanda miti ili kukwepa joto. Kwa bahati mbaya, wanyama hawa ambao zamani waliishi hadi Ulaya, kwa sasa wanakabiliwa na tishio kubwa la ujangili, huku takriban simba 600 wakiuawa kila mwaka kwa ajili ya biashara haramu ya viungo vyao au uwindaji wa kitalii.

Beatus Maganja, ni Afisa Habari wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) anaeleza kuwa Simba kwa kawaida, ni mnyama ambaye anawinda kwa kuvizia. Yaani 'ambush predator'. Yeye mara nyingi anapenda kushambulia akiwa amejificha au akiwa hajagundulika. Kwa watu ambao wamekuwa wakifuatilia filamu mbalimbali zinazoonyesha matukio ya simba, utaona ni wanyama ambao wanawinda kimkakati. Wakiwa wamejificha, wanamweka mnyama kwenye target.

Wanapoanza kufukuza, hasa masimba majike ndiyo wawindaji wazuri, maana yake huku mbele mnyama anapoelekea tayari kunakuwa kuna target ya simba wengine ambao wanamsubiri huyo mnyama anayekurupushwa. Akifika tu pale wanamshambulia na kumgeuza kuwa kitoweo. Kwa hiyo wanawinda kimkakati.

Na ni kwa nini wanafanya hivi? Wanafanya hivi ni kwa sababu simba si mnyama anayekimbia sana akilinganishwa na mnyama mwingine kama Duma. Kwa hiyo ndiyo maana simba kwa sababu hapendi kutumia, kwa sababu hana uwezo wa kukimbia muda mrefu kama anavyofanya duma, basi wanafanya mbinu hizi za ambush.

Wanaweka ambush, akitokea mnyama basi wanamshambulia. Na ikitokea mnyama amefanikiwa kutoroka watamkimbiza lakini si kwa umbali mrefu, basi watasurrender na kumwacha. Kwa hiyo huyu ni mnyama ambaye tunasema ni ambush predator.


Madai

Kumekuwapo na madai kuwa binadamu akikutana na Simba hushambulia tu ikiwa umewageuzia mgongo?

Je, ni upi uhalisia?

Kupitia utafutaji wa maneno muhimu (Key words search) JamiiCheck imebaini maoni ya watu mbali ambao wanaeleza uzoefu wao kuhusu Simba.

Mtumiaji mmoja wa Quora anaeleza kuwa wanyama wengi wanapomwona simba hukimbia. Kwa hiyo, njia ya kawaida na ya vitendo ambayo simba hutumia kuwinda ni kuwashambulia kutoka nyuma. Wanyama kama pundamilia, nyumbu, twiga, paa (impala) na wengine mara nyingi hujaribu kwanza kutoroka wanapomwona simba.

Hata hivyo, wakati mwingine simba wanaweza kushambulia kutoka pembeni au mbele, hasa kama sehemu ya mbinu ya kuwazunguka na kuwafukuzia mawindo kwenye mtego. Hii huonekana zaidi kwenye uwindaji wa makundi, ambapo wanajaribu kuongoza mnyama kuelekea sehemu ambako washirika wao wanangoja.

Lakini kwa ujumla, ni suala la silika ya kuwinda mnyama anapokimbia, simba hujaribu kumfuatilia na kumshambulia kutoka mahali penye nafasi nzuri ya kumkamata.

Aidha Beatus Maganja, ni Afisa Habari wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) anaongeza kuwa kuna ukweli mkubwa kwamba mnyama simba unapomgeuzia mgongo unachochea zaidi silika ya kuwinda.

Kwanza pale anaona kabisa kwamba ume-withdraw, pale kwamba umeingia uoga dhidi yake. Kwa hiyo kama lengo lake ni kutaka kukushambulia, pale ndipo atakufuata na kuhakikisha kwamba anakushambulia.

Lakini pia katika hili, ijulikane kwamba wanyama hawa hawakuumbwa kwa ajili ya kula binadamu. Chakula chake kikuu ni hawa wanyama walao nyasi. Inapotokea binadamu ameingia kati pale mara nyingi huwa wanapenda tu kuwaletea madhara, kuwashambulia.

Je, ni mambo gani unatakiwa kufanya ukikutana na Simba wakati wa kutembea porini au safari ya watembea kwa miguu?

Tovuti ya Head to Africa inaeleza kuwa endapo unatembea porini au sehemu yoyote na ghafla ukakutana uso kwa uso na Simba, yafuatayo ni muhimu kuyazingatia.
​
  • Usikimbie kamwe. Hili ni jambo la msingi zaidi, ukikimbia, unaweza kuchochea silika ya kufukuzwa na kushambuliwa.​
  • Angalia tabia ya mnyama. Simba akiwa amekasirika au anahisi kutishiwa, huweza kuzungusha mkia wake kutoka upande mmoja kwenda mwingine. Akiwa anawinda, huweka mkia wake wima na kuutikisa kidogo kidogo. Ikiwa anakuwinda, unaweza kuona kichwa kimeinama na ishara za kumvizia.​
​
  • Simama tuli. Hata kama simba anakuja kwa kasi, usikimbie. Anaweza kukimbia kwa zaidi ya kilomita 80 kwa saa na mngurumo wake ni mkubwa sana na wa kutisha. Ukikaa kimya na bado hakusogelei wala haondoki, anza kurudi nyuma polepole sana.​
​
  • Usiketi wala kuinama. Unapaswa kuonesha kuwa wewe si windo wala tishio. Lengo ni kujifanya mkubwa zaidi na mwenye kujiamini. Wanyama walao nyama mara nyingi hawawaoni wanadamu kama chakula cha kawaida. Mara nyingi hutaka kuepuka binadamu, lakini wana silika ya kuwinda ikiwa wataona kitu kikikimbia.​
​
  • Rudi nyuma polepole sana huku ukijitahidi kujifanya mkubwa na mwenye mwonekano wa kutisha kidogo, bila kufanya harakati za ghafla. Kwa kawaida, uwezekano wa mnyama kushambulia binadamu ukiwa porini ni mdogo sana, kwani wanyama wengi hujihami na huepuka watu. Hata hivyo, bado ni muhimu kuwa makini na kuheshimu wanyama wa porini.​

Muhimu zaidi usikaribie wanyama wa porini kupita kiasi ni wanyama wa mwituni na wanapaswa kuheshimiwa kila wakati.​
Sio kweli Mkuu, Simba Wa Mbugani mara nyingi hua hawashambulii watu, Na ni kama washazoea kuona binadamu sio kitoweo, kwa sababu wanapishana na watalii, tour guide nk kwenye magari yao.

Sasa ukikutana nae bahati mbaya live, Kwanza yeye atabaki kushangaa kwanza akusome kama wewe ni threat(Tishio) au friendly.

Hapo ndo jukumu lako kumuonyesha kua wewe huna issue nae, kwa kusimama na kutulia ukimuangalia na yeye, then unaanza kurudi nyuma taratibu kuelekea sehemu salama.

Akishaona hivo, anajua huyu jamaa fala yu hana issue, na kuna distance ukikaa anajua kabisa hapa sio threat, ila ukimsogelea distance fupi hata kama ni kwa mbele mbele ana kuattack not for food ila for defence.

Simba wa baya ni wale walio toka mbugani, na kuingia Mitaani mmoja mmoja hao wanakua kama wamevuruga wanaanza kuwinda watu na mifugo.
 
Ni kweli, hiyo ndiyo kanuni namba moja ya usalama unapokutana na simba porini. Ukimpa kisogo au ukikimbia, unamfanya akuone kama kitoweo (conformation of prey), jambo linalochochea silika yake ya kukulinda au kukufukuza.

Hata ukimpa kisogo asilimia 60 simba wa porini hashambulii watu for food, Mostly wanashambulia for defence, na ni pale umemsogelea sana, au ukutane na simba amejeruhiwa na watu.
 
Back
Top Bottom