Ukikutana naye........UTAMUULIZA?


Mkuu ndio hali halisi
Haya ni masomo ambayo huwa kwa sisi hatuoni kama masomo ila tunaona kama ni shida fulani ila kila hatua unayopitia ujue ni mtihani katika maisha yako na ni funzo lisije likatokea tena
 
mkuu naamini nia ya mleta mada ilikuwa hiyo
sasa huku Ally anakoelekea kunapelekea zaidi kuingia kwenye lile jukwaa la stress ambalo naamini pia sio lengo la mleta mada hapa

Mnakosea kabisa kudhani kuwa nataka niipeleke mada huko kwenye mastress. Maswali yote ambayo nimeuliza hapa ni halali na mleta mada hakuweka vikomo vya maswali ya kuulizwa. Au aliweka? Sasa sijui haya yote ya kusema mimi nataka sijui kuipeleka hii mada kwenye mastress yanatoka wapi?

Haya bana naona kuna maswali mengine kumbe ni kufuru hata kuuliza. Nawaachia mada yenu mfurahie bila mastress. Mimi nasepa zangu kule kwenye kutongozana na kina Lizzy na Ma Jerry.
 
Upendo na amani na vitawale katika hii sredi. Na Husninyo popote pale ulipo, nakuhitaji huku PM.
 
Ningekutana nae uso kwa uso ningemwambia .
Eeh mungu Nashukuru kwa matendo yako makuu Kwangu
Nashukuru kwa kunipa familia Njema na yenye upendo
Nashukuru kwa kunipa wazazi wenye hekina na busara za kutusikilia watoto wao
na kutuongoza katika maisha haya yaliyojaa tabu
Nashukuru kwa kunipa dada na wadogo zangu wenye upendo wa agape
Ningemuomba anipe mapito yaliyo mema siku zote
Ningemuomba anipe hekima kama za mfalme Suleiman ,
Pia ningemwambia nakushukuru kwa yote yaliyotokea katika maisha yangu
kwani najua ni moja ya mapito yangu
.
 

Ally afu wewe acha mambo bana hapa ni MMU stress free
 
Mie nisingemwuliza kitu zaidi ya kumshukuru tu, yote nimwombayo anayatekeleza
 
Nitaongea mpaka aseme baaasi

Swali:
Lini mafisadi wa Tz wataisha au
wataadabiswa na nchi iwe nzuri
wananchi wafaidi?

Nitashukuru:
kwa yote aliyonitendea mimi na familia yangu
ikiwa ni pamoja na kuniwezesha kuwa hivi nilivyo,

Nitaomba:
abariki uzao wangu wote
aniepushe na vishawishi vya kuiibia nchi yangu
anibariki niwe na utajiri wa kutisha
anizuie nisiingie ktk siasa
 


Hii post nimeisoma na kunifanya nisikie imani na huruma....
BUT kusoma kwangu hii thread badala ya kusikitika nimecheka mno... Dah!
(i hope nimesamehewa...)... Saizi tupo very comfy.. for Kumtaja Mungu
in vain ilikua issue hapo kati...

On a serious note.

Nikipata nafasi ya kuonana na Mwenyezi Mungu na kupata nafasi ya kumuuliza
suali ama kumuambia lolote... Naamini nitakua Speechless na kuishia kumshukuru
kwa Neema zoote alizo nijalia, familia alonipatia, watu alonijalia, na Maisha niloishi....
 
<br />
<br />
nimesusa, sikupm wala siquote posts zako hadi sikukuu ipite.
Nitakufuata hukohuko uliko!

Mie nisingemwuliza kitu zaidi ya kumshukuru tu, yote nimwombayo anayatekeleza
Una bahati sana ndugu yangu, Mshike sana Mungu wako, usimwache kamwe!

Hahahahaha..... unafikiri atakuwa na muda mrefu hivyo? Mungu ana watu wengi sana!
 

Nyie wasichana wawili hapo juu
Mna bahati sana....
Mshikeni sana Mungu wenu
Msimuache kwa kuwa anawapenda sana.

Kuna wengine wanamwomba mpaka wanafikia hatua ya kukufuru kwa kuwa hawajibiwi maombi yao.
 
Nyie wasichana wawili hapo juu
Mna bahati sana....
Mshikeni sana Mungu wenu
Msimuache kwa kuwa anawapenda sana.

Kuna wengine wanamwomba mpaka wanafikia hatua ya kukufuru kwa kuwa hawajibiwi maombi yao.

Babu nani kakwambia mie ni msichana ???shikamoo babu
 
mie naogopa kukufuru babu odm. kwa sababu,mh! ngoja tu nijifunze kuhesabu baraka zangu! mama yangu alipofariki miaka 7 iliyopita, dadangu alisema "muacheni Mungu aitwe Mungu. kama alisema Yesu ni mwanae mpendwa, tumsikilize, na akamuacha aangikwe msalabani!basi bana, imeshakua!''. tuliishia kumshukuru Mungu kwa muda aliompa mama kuwa nasi, na kutuandaa kuwa wanawake ambao tuko hivi leo! na kutupa ujuzi na mtazamo huu! wakati mwingine unaweza kujiuliza, why bother with God? lakini Mungu atusaidie.
 
Babu nani kakwambia mie ni msichana ???shikamoo babu
Oh.... avatar ilinidanganya, samahani mvulana.

Kweli mwacheni Mungu akae hukohuko mbinguni aliko, kumbe akijitokeza atakuwa na maswali mengi sana ya kuulizwa..... Pole sana rafiki, kwa kumpoteza mama yako mpendwa......

una hamu ya kukosa nguo mpya eeh? shauri yako!
babu; shkamoooo! naomba sh buku eeh..
Acha kuchakachua sredi, hii ni sredi ya Mungu.
 
haaah haah mkuu then ungemuuliza kwa nn alimchukua sokoine halafu Lowassa anamuacha!
Au kama ni kisiasa zaidi utamuuliza kwanini umekubali Pinda adhalilike namna hii kwa Jairo kurudishwa kwenye ulaji?
 
Au kama ni kisiasa zaidi utamuuliza kwanini umekubali Pinda adhalilike namna hii kwa Jairo kurudishwa kwenye ulaji?

Aise hapa ni stress free usilete ya Jairo na Pinda na m.k.w.e.r e hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…