Ukikutana naye........UTAMUULIZA?

Ukikutana naye........UTAMUULIZA?

Mungu anayajua maisha yetu sana na anajua tutaishi tu hata kama wanaotupenda hawapo!

Nikikumbuka nilikotoka huwa naogopa kumuuliza Mungu chochote kwa kuwa hapa nilipo ni miujiza ya Mungu kwangu.....

Namshukuru Mungu kwa yote wala sina cha kumuuliza
Selfish.....! We umefanikiwa na umepata miujiza yote, majirani na ndugu zako nao wamepata mafanikio na miujiza kama yako? Kwanini usimuulize Mungu mbona hawafanyii miujiza na wengine?....

Kazi ya Mungu haina makosa haihojiwi, haisahihishwi..baada ya kifo ni hukumu (hakuna maswali wala hoja) kama una maswali wakati ni sasa.. watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa (matatizo mengi tunayatengeneza/tunajitakia wenyewe eg, umaskini wa vizazi unaotengenezwa na ccm kwa ridhaa yetu wenyewe!?)..shetani siyo kisingizio tena..mpingeni naye ATAWAKIMBIA.. atatawanyika ktk njia saba sawa sawa na neno la Mungu.
Natamani nikuelewe lakini nashindwa...wakati wa kuuliza ni sasa, Mungu yuko wapi nimuulize? Nataka nimuulize uso kwa uso.... LIVE

Huyu ndugu mlevi anahoji kuhusu kufa kwa baba yake akiwa mdogo..je naye akiondoka na hiv au ajali ulevini..watoto wake nao watakuwa na hoja hii: ee Mungu mchome moto vilivyo baba yetu mr.ulabu or sharubati..
Duh! Kaaaaaazi kweli kweli!
 

Kukuwakilisha katika kuuliza maswali?
Err....wacha nikwende kuuliza....

Si atakuwa amenigea na nguvu za kufanya kazi nisihangaike kwenda kula pweza na tende
atakuw aamefanya la maana sana
NYIE VIJANA WAWILI HAPO JUU...........Mungu akiwaona hatakuwa na muda wa kuwasikiliza maswali yenu....
 
Asprin Mungu ni Roho umuendee kwa jinsi ya roho..na ana njia ya kumuendea (MIMI ndimi njia ya kweli na uzima,mtu haendi kwa BABA pasipo MIMI..) njooni tusemezane..na haja zenu nazijulikane asema Bwana!..kama watu wanavyoamini/kuendea? majini/shetani..pia wapo weengi wanaomwendea Mungu (Alfa na Omega), asprini bado unataka kumuona Mungu
 
Asprin Mungu ni Roho umuendee kwa jinsi ya roho..na ana njia ya kumuendea (MIMI ndimi njia ya kweli na uzima,mtu haendi kwa BABA pasipo MIMI..) njooni tusemezane..na haja zenu nazijulikane asema Bwana!..kama watu wanavyoamini/kuendea? majini/shetani..pia wapo weengi wanaomwendea Mungu (Alfa na Omega), asprini bado unataka kumuona Mungu
Kwa kweli napenda sana kumuona. Anitegulie hili fumbo la Imani............. Manake tunamwomba kwa imani lakini saa nyingine anajibu saa nyingine anauchuna. Nataka nimuulize kwanini saa nyingine anatuchunia wakati sie tuko serious?
 
Sharobalo wa JF aka Mr.Rocky.....kamata mwizi meeeeen.....

kweli na ubabu wangu wote huu naitwa sharobaro
may be maana ya sharobaro imebadilika na ngoja nimuulize babu Asprin na Mungu mwenyewe anipe definition ya sharobaro
 
Duh! Naona Mungu has not been given a break bado...lol... Kweli analo...
 
Wapendwa marafiki salamu,

Jana nlimpigia simu rafiki yangu. Alipokea akiwa na simanzi kubwa. Kumbe ndio alikuwa kapokea habari ya msiba wa kaka yake. Alikuwa analia na kuongea kwa shida. Nilihuzunika kwa niaba yake..........kama si nguvu ya Tusker Malt labda nami ningemwaga chozi. Mnywaji mwenzangu akashangaa kwanini nimepata simanzi ya ghafla, nikamsimulia.

Huyu mtu akaniambia neno ambalo limenifanya nitafakari kwa kina usiku kucha......... Namnukuu: "Ndugu yangu, Mwache Mungu aitwe Mungu na aendelee kukaa hukohuko aliko maana ningepata nafasi ya kukutana naye sasa hivi ningemuuliza KWANINI ULIMCHUKUA BABA YANGU nikiwa bado mdogo nikataabika namna ile?"........ Nilichoka na mpaka sasa nimechoka.....Jamaa alivyonisimulia maisha yake, jinsi mama yake alivyohangaika.......Kweli kila mtu ana swali lake.....Dah!

Nami najiuliza.... Hivi ningepata nafasi ya kukutana na Mungu akanipa nafasi ya kumuuliza au kumwambia chochote ningemwambia na kumuuliza nini?.....

Kwanza ningeanza na shukrani:
Ahsante kwa kuniumba Mwanaume..... manake angeniumba mwanamke ningemuuliza kwanini ameniumba mwanamke.
Ahsante kwa kunipa mke mzuri (japo kwa ubinadamu wangu huwa natelezaga) na mabinti wawili wazuri.
Ahsante kwa kunipa wazazi wanaonipenda na kunijali sana
Ahsante kwa kunipa ndugu, marafiki, majirani tunaoheshimiana na kupendana sana.

Then lazima ningemuuliza;

Kwanini tatizo hili limetokea kwenye familia yetu?..... Kwanini kwetu?......... Ningemuuliza mbona kila siku tunakuomba kwenye maombi/sala utuondolee hili tatizo lakini huliondoi?........Lazima ningemuuliza...Niape?

Kuna mtu mwingine huku angekuwa na Swali kama angekutana na Mungu na kupewa nafasi ya kumuuliza?

Kama alivyonambia ndugu yangu, mwacheni Mungu aitwe Mungu......... Na aendelee kukaa huko aliko.
AMINA.

Leo ODM yuko kimajonzi zaidi.
Harudi kitandani wala nini. Anajiuliza tu.

Mara ngapi tunakutana nae na hatumuulizi?
Ni vile tu saa tunayokutana nae hatujui kama ndiyo yeye.
Ukipona kwenye ajali unasema 'pale ni Mungu tu'
Au hamjui kama yuko katikati yetu?
Sema naogopa kumuuliza.....
 
ningemuuliza,kwanini hataki tukaishi milele na milele
 
Babu aka Tajiri wa upeo hali yako ya leo?
Hali yangu kama yako sheikh.... Ijumaa ndo hiyo na vyungu vinakatia tu, Alhamdulillah.

kweli na ubabu wangu wote huu naitwa sharobaro
may be maana ya sharobaro imebadilika na ngoja nimuulize babu Asprin na Mungu mwenyewe anipe definition ya sharobaro
Nadhani enzi zetu tulikuwa tunawaita machekibobu.

Duh! Naona Mungu has not been given a break bado...lol... Kweli analo...
Hivi angekuwa anajipa break.....ingekuwaje mathalan ndo umevamiwa na majambazi yanataka kukubaka afu ye ndo kwanza amepumzika.......... God forbid!
 
Babu hata huko sifai
Hivi fikiria na ubabu wako mtu anakuita chekibobu au sharobaro si kitu ya ajabu kabisa
 
Hivi angekuwa anajipa break.....ingekuwaje mathalan ndo umevamiwa na majambazi yanataka kukubaka afu ye ndo kwanza amepumzika.......... God forbid!

ODM una nia njema na mimi kweli??... yaaani that is the only example you could think of?? Kweli GOD FORBID!
 
kuna vitu vingine ukijuulizaa sanaa,unaaza kuokota makopo...mungu anafanya kitu kwa sababu.maswali mengine ukijiuliza kumuuliza mungu unakufuru.polee
 
Ninapoandika haya namaanisha.....Mungu wa Yakobo,mungu wa Ibrahimu mungu wa Musa.
1.kwanza baada ya kumuona tu ningeanguka chini yake na kumuabudu kwa nguvu zangu zote.
2.pili ningemshukuru sana kwa kutenda na kuweka system ya maisha kama ilivyo.safi sana.
3.tatu ningemshukuru sana kwa kuwa na upendo mkuu na uvumilivu wa hali ya juu kwa binadamu ambao kila sekunde wanamuasi. Vinginevyo angeifutilia mbali dunia.
4.nne ningemuuliza kwanini watu wengi sana hawamwelewi na kumtumia??? Ni kazi ya shetani au kuna la ziada???
5. Tano ningemshukuru sana sana kwa kunisikiliza nimwombapo na kunipa ninachokitaka kwa spidi ya ajabu wakati fulani kabla hata sijamwomba ile kuwaza tu mambo yanajipa karibu asilimia 90 ya maombi yangu anayakubali. Kwa nini ananifanyia hivi??? Anataka hasa nimfanyie nini zaidi ya yale yaliyoandikwa kwenye vitabu vitakatifu????
6. Sita ningemwomba aendelee kunivumilia tu na kunisamehe pale ninapokosea,mimi ni wake pasipo shaka.
7.saba ningemsihi sana sana awasamehe wanadamu wote zambi zao,wote waende peponi,kwa sababu kimsingi ni shetani kawafikisha hapo dhambini. Jehenamu ibakie kuwa ni ya shetani kama alivyokuwa ameiandaa awali.
 
Back
Top Bottom