Utangulizi: Kwanza sio mbu wote hueneza malaria, ni wale aina ya Anopheles tu tena hata sio wote na pia ni mbu jike pekee tena aliye na vimelea vya malaria (Plasmodium), tena vimelea hivyo viwe katika hatua ya sporozoite na tena viwe katika tezi za mate za mbu huyo!
Jibu: huwezi kupata malaria hata ukila mbu kilo mbili, kwa sababu ili upate malaria sharti mbu aliyeambukizwa vimelea vya Plasmodium akuingizie vimelea hivyo kwenye mfumo wa damu na sharti vimelea hivyo viingie kwenye ini kwanza na kubadilika (metamorphosis) na kisha kuingia tena kwenye mfumo wa damu na kubadilika tena hadi kufikia hatua ya kusababisha malaria. Ukimeza vimelea vya malaria vitameng’enywa kama chakula na makapi kutoka nje kama choo.