- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Mdau kutoka PM
Hello Jukwaa la JamiiForums na Jamii Check kwa ujumla. Mimi nina habari inanitatiza ambayo inaenea mitaani, na kila mtu anaamini hivyo,
Kwamba ukila samaki pamoja na maziwa basi unaweza kuaga Dunia, na unapaswa kula kimoja kimoja kwa wakati tofauti
Je, hii habari ina ukweli wowote?
Hello Jukwaa la JamiiForums na Jamii Check kwa ujumla. Mimi nina habari inanitatiza ambayo inaenea mitaani, na kila mtu anaamini hivyo,
Kwamba ukila samaki pamoja na maziwa basi unaweza kuaga Dunia, na unapaswa kula kimoja kimoja kwa wakati tofauti
Je, hii habari ina ukweli wowote?
- Tunachokijua
- Samaki ni chakula bora kwa sababu nyama yake ina protini nyingi inayopokewa kwa urahisi na mwili wa binadamu. Watu wengi Duniani wanategemea samaki hasa kama chanzo cha protini
Maziwa hutumika kama lishe ya watoto wachanga wa binadamu na wanyama, nje ya lishe ya watoto wachanga, maziwa ya wanyama mbalimbali kama ng'ombe, mbuzi nk hutumiwa na watu wote kama kinywaji na chakula pia kama chanzo cha protini. Maziwa hunywewa au kuungwa katika upishi wa chakula.
Kumekuwepo na imani kuwa ukila samaki na maziwa kwa wakati mmoja au kuvichanganya kwenye kupika ukila basi utapata madhara mbalimbali wapo ambao huamini huweza kusababisha hata kifo
Je, ukweli ni upi?
Jamiicheck imetafuta ukweli wa madai haya kwa Kuzungumza na Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma Dkt. Ona Machangu ambaye amekanusha madai hayo kuwa kuna madhara kwa mtu akila samaki na maziwa kwa pamoja.
Dkt. Ona Machangu Amesema:"Hapana, kula maziwa na samaki pamoja hakutasababisha kifo au madhara yoyote, kuna baadhi ya watu wanaweza kupata usumbufu mdogo wa usagaji chakula kwa baadhi ya michanganyiko fulani ya vyakula lakini si kwa maziwa na samaki.
Kwa watu wengi, ulaji wa maziwa na samaki pamoja ni salama kabisa na pia virutubisho vya protini vinapatikanika katina kula samaki au kunywa maziwa".
Pia, kupitia machapisho mbalimbali mitandaoni hoja hii ya samaki na maziwa kuwa na madhara iwapo mtu atakula kwa pamoja imekanushwa huku baadhi wakifafanua zaidi kuwa hakuna madhara kwa mtu kula samaki na maziwa kwa pamoja labda kama mtu na mzio(allegy) na kimoja kati ya hivyo au vyote na madhara atakayopata ni kutokana na mzio na sio mchanganyiko huo.
Kwa mujibu wa tovuti ya Nestle wameandika kuwa: Kisayansi, hakuna sababu kwa nini tunapaswa kuepuka kula samaki na maziwa pamoja. Kuna mapishi mengi ambayo yanajumuisha maziwa na samaki pamoja, kama samaki waliookwa na maziwa.
Hakikisha tu vyakula hivi vinaandaliwa kwa usalama kabla ya kuliwa, yaani, samaki asiwe mbichi awe ameiva vizuri, na maziwa yanatumiwa kabla ya tarehe ya mwisho wa matumizi.
Ila kwa watu ambao wana mzio wa samaki au maziwa au ambao hawana uvumilivu wa lactose vyakula hivi vitaleta shida kutokana na mzio walionao.