Ukili/ukindu/mikeka imepotea sana

Ukili/ukindu/mikeka imepotea sana

mutisya mutambu

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2010
Posts
208
Reaction score
82
Kwa sasa moja kwa moja ukitaja neno mkeka utaeleweka unazungumzia kikaratasi(receipt) baada ya kubet, lakini vijana wengi wa sasa hasa dada zetu hawajui mkeka ni nini ama ukindu ama ukili.
Wakina dada na mama zetu huko nyuma hii ndio ilikuwa kitu cha kufanya wakati wa mapumziko, ila kwa sasa wametekwa na smartphone kwenye mitandao ya kijamii, mikeka tutanunua ya dukani.

Kuna haja kubwa ya kuwafunza mabinti wa sasa, wengi hawajui huu utamaduni,unapotea polepole.
 
Siku hizo ,zilikuwa siku za furaha sana ....ukiingia chumbani kwa kijana utakuta mkeka kiwambazani ....ukiingia chumbani kwa wazazi utakuta mkeka na makawa na vipepeo vyenye ujumbe murua ......ukienda maulidini utakuta kumetandikwa majamvi.
Kuna haja ya kuuenzi utamaduni huu.ila ttzo hizi shule za akademi
 
Kwa sasa moja kwa moja ukitaja neno mkeka utaeleweka unazungumzia kikaratasi(receipt) baada ya kubet, lakini vijana wengi wa sasa hasa dada zetu hawajui mkeka ni nini ama ukindu ama ukili.
Wakina dada na mama zetu huko nyuma hii ndio ilikuwa kitu cha kufanya wakati wa mapumziko, ila kwa sasa wametekwa na smartphone kwenye mitandao ya kijamii, mikeka tutanunua ya dukani.

Kuna haja kubwa ya kuwafunza mabinti wa sasa, wengi hawajui huu utamaduni,unapotea polepole.
Msichana gani atakubali kuyasugua matako yake kwenye mkeka badala ya kutafuta location Qalii ayabinue kwa mipicha picha.!
 
Mmh. Sio rahisi kwa kweli.

Hayo yamebaki kule kwetu Tanga tena ni kwa wale watu wazima ndio utawakuta wana muda wa kushona ukili ila kwa vijana mmh. Ishashindikana hiyo.

Ndio sababu sio miswala, makawa sijui mikeka vyote vinapatikana kwa bei juu sababu wasukaji hakuna.
 
Back
Top Bottom