Ukimlaumu sana Uhuru Kenyatta usiache pia Kumshutumu mno Raila Odinga

Ukimlaumu sana Uhuru Kenyatta usiache pia Kumshutumu mno Raila Odinga

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Ni kweli kabisa kwamba inawezekana Rais Uhuru Kenyatta na ambaye pia ni Mgombea Urais kupitia tiketi ya Jubilee tukamlaumu kwa mambo ambayo yanaendelea sasa nchini Kenya hasa katika kuelekea katika marudio ya Uchaguzi Mkuu wa nchini humo lakini pia hii haituondolei Sisi hawa hawa kuacha Kumshutumu Kiongozi wa Upinzani na aliyekuwa Mgombea Urais kwa tiketi ya NASA Mzee Raila Odinga.

Kwa upande wangu GENTAMYCINE nadhani Rais Uhuru Kenyatta alijitahidi kadri ya uwezo wake kuonyesha nini maana halisi ya Demokrasia hali ambayo ilipelekea Yeye na Wakenya wote kupongezwa duniani kwa Kitendo chake cha kuheshimu maamuzi ya Mahakama ya juu kabisa ya Kenya ( Supreme Court ) kuwa Uchaguzi ule urudiwe kwakuwa ulikuwa na dosari kadhaa za kimsingi. Hapa Uhuru Kenyatta hata leo akitoka Ikulu bado dunia itamkumbuka kwa hili na ni jambo jema na la kuigwa sana duniani kote ambako Siasa za Vyama vingi inatamalaki.

Nadhani Raila Odinga yawezekana Umri alionao unamlevya au akili zake sasa zimeanza kufika ukingoni na sasa labda anaelekea kuwa Chizi / Taahira / Mwehu / Mtambo / Dishi linayumba kutokana na Vitendo vyake vya Kipumbavu / Kipopoma kabisa ambavyo amekuwa akivifanya na vinavyotuachia Sisi ' Werevu ' maswali mengi ambayo mwishowe yanatushawishi tuzidi ' Kumdharau '.

Ni huyu huyu Odinga alipinga tarehe ya awali ya Uchaguzi na kweli ikabadilishwa, ni huyu huyu Odinga alitaka kuwe na mabadiliko fulani ya Kisera na Kikanuni ndani ya IEBC na yakafanyika, ni huyu huyu Odinga alitaka kwamba Wagombea wote walioshiriki Uchaguzi wa awali nao waweze kujumuishwa ambapo mwanzoni IEBC ilimpuuza lakini baadae ikakubaliana na alichokishauri na cha kushangaza kama siyo kusikitisha huyu huyu Odinga tena akakataa Wagombea wengine kujumuoishwa katika Uchaguzi huu wa marudio na mengine kadhaa ambayo bado yanaonyesha mapungufu makubwa ya Raila Odinga.

Katika hali tu ya kawaida na ' logically ' haingii akilini Mtu huyo huyo ( namaanisha Raila Odinga ) ambaye karibia 85% ya madai yake IEBC pamoja na Mahakama ya Juu ya Kenya imeyatekeleza halafu mara ghafla anajitoa katika Uchaguzi na hapo hapo Kesho yake tena Yeye na Binti yake wanapanda Ndege kwenda nchini Uingereza kuisema vibaya Kenya kwa ' Wazungu ' wakati zimebaki wiki mbili tu Uchaguzi wa marudio kufanyika. Huyu Odinga kama siyo ndiyo ' adui ' namba moja wa Kenya atakuwa nani?

Narudia tena kusema kwamba sikatai Rais Uhuru Kenyatta nae kwa upande wake ana makosa / mapungufu yake ila kuna uwezekano mkubwa kwamba hayo mapungufu ya Rais Uhuru Kenyatta yakawa yanasababishwa ' kimakusudi ' na matendo yasiyovumilika ya Mpinzani wake Mkuu Mzee Raila Odinga hali ambayo ' Kibinadamu ' inamfanya Rais Uhuru Kenyatta nae ahamanike / awe emotional hadi kuonekana kwamba anatumia vibaya ' Urais ' wake dhidi ya Raila Odinga.

Mtazamo wangu kama GENTAMYCINE nadhani mpaka kufikia hapa Wakenya wengi na ambao nina uhakika kabisa kwamba wana akili kubwa tu wameshajua kuwa kati ya Uhuru Kenyatta na Raila Odinga nani kweli anawafaa kwa maendeleo yao hasa ya Kiuchumi na Kijamii na hapa nisiwe mnafiki au nisifiche ni kwamba nitawashangaa na kuwadharau mno Wakenya kama wakipoteza muda wao kumpa ' Kura ' Mtu mwongo, mchochezi na mfitini Raila Odinga na kumuacha Mtu ambaye tayari ameshaonyesha dalili njema za kuwakomboa Wakenya wengi katika nyanja mbalimbali na matatizo yao Rais wa sasa Uhuru Kenyatta.

GENTAMYCINE namalizia tena kwa kusisitiza kwamba tunapomlaumu sana Uhuru Kenyatta juu ya yanayoendelea nchini Kenya basi hivyo hivyo tusiache au tusisahau pia Kumshutumu mno Raila Odinga kwa vitendo vyake vya waziwazi anavyovifanya vya kuchochea ' machafuko ' makubwa nchini Kenya ili mradi ' Kikinuka / Kikichafuka / Kikisanuka ' basi kuwe na GNU ( Government National Unity / Serikali Umoja wa Kitaifa ) ili tu na Yeye apewe ' madaraka ' ya juu kabisa na aendelee kufurahia ukubwa / uongozi ndani ya Kenya.

Nawasilisha.
 
akina Sammuel999 hawapendi kuyasikia haya....... hata mimi najiuliza kwann odinga anapenda kuwa kigeugeu kiasi hiki??

Huyo Mzee Raila Odinga nilikuwa namuheshimu sana ila sasa ni kati ya Watu ambao nimetokea si tu kuwapuuza bali hata kuwadharau vile vile. Acha Uhuru Kenyatta achukue nchi awapiganie Wakenya Kimaendeleo ya kweli.
 
akina Sammuel999 hawapendi kuyasikia haya....... hata mimi najiuliza kwann odinga anapenda kuwa kigeugeu kiasi hiki??
SammueI999hapa uezi muona,Raila mwenyewe alisema uchaguzi urudiwe,sasa anaambia watu waandamane,tarehe hiyo atajua kenya iko n kiongozi
 
Back
Top Bottom