Ukimpa Binti Ujauzito ni Lazima Umuoe?

Godwishes

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2011
Posts
640
Reaction score
167
Kuna madada wengi huwa wanajiimanisha kuwa,akishapewa UJAUZITO ndo tiketi ya moja kwa moja ndani Shela?Je ni lazima au unaweza lea mimba mpaka mtoto,bt anaendelea kuwa mtu wako?.
 
Kuwa mtu wako una maana gani? yaani wewe uoe mke mwingine na yeye aendelee kuwa mtu wako???
 
Sio lazima lkn kama huna mpango wa kumuoa mimba unampa yanini? Na ningekuwa mimi hata mtoto sikupi yaani unamchezea mtoto wa watu na kumdanganya ukisha mpa mimba unajataa kumuoa ili amuoe nani huku ushampotezea mda wake
 
Kabla hujauliza swali kama hili hebu jiulize dada/binti yako akifanyiwa hivyo wewe utajisiake?
Ingawa nina hakika mtu mwenye mawazo kama haya hawezi kuwa na binti
 
Ukioa unakuwa umetimiza ule msemo wa kuwa 'take responsibility of your action'
 
Siyo lazima kuoa. subiria mwanao akishaweza kula ugali amishia kwako.
MP.
 
Inategemeana, mtu anaweza akawa ana mke halafu anatoka nje ya ndoa, kisha anampachika mimba mtu mwingine je ni lazima amuoe? Ataoa wangapi?
 
ndio ni lazima umuoe....
tena kwa sherehe na matarumbeta.....
bye
 
Ukioa unakuwa umetimiza ule msemo wa kuwa 'take responsibility of your action'
Ni kweli madame, lakini kuna kuteleza katika mapenzi. Mlikuwa mnapass time na mlikuwa hamna malengo ya kuoana. ni bora kulea mtoto kuliko kukosa furaha maisha yako yote kwa kuoa mke usiempenda. to me,.. MUNGU apishe mbali aiseeee.
 
Kuna madada wengi huwa wanajiimanisha kuwa,akishapewa UJAUZITO ndo tiketi ya moja kwa moja ndani Shela?Je ni lazima au unaweza lea mimba mpaka mtoto,bt anaendelea kuwa mtu wako?.

wala haina ulazima, kwanza mkioana mnachokana haraka, ai! yani kila siku asubuhi na jioni mmegandana tu, mie ayo maisha ata siyawezi, kuna wakati huwa nataka kuishi mwenyewe .
 
hii mada wanawake wote watasema mimba ndo tiketi ya kuingia ndani ya shela wakati ni uongo.
 
Cio lazima bhana.....mie niliyempa mimba ctamuoa and she knows that!
 
Sio vizuri ku-comment story inayo kutach kwakweli.
 
sasa mpaka umempa mimba ulikuwa huna malengo nae au?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…