Ukimsikiliza Maxence Melo kwa umakini utaelewa kwanini wasanii wetu wako jinsi walivo

Ukimsikiliza Maxence Melo kwa umakini utaelewa kwanini wasanii wetu wako jinsi walivo

Agent-47

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2014
Posts
786
Reaction score
2,860
Wiki iliyopita ya mwezi huu wa September, ndugu Max Melo alitoa public lecture kwa watu wa TLS. Alielezea kwa ufasaha sana madhira aliyoyapata kwa kusimamia uhuru wa private information na JF kwa ujumla. Pamoja na kupewa kesi kama ugaidi 😆 na nyingine, his banking accounts were frozen, alizuiliwa kutoka nje ya Dar na visanga kibao.

Katika mazingira haya, ni msanii gani anaweza akapingana na mfumo na akawa salama? Akafanya show kawaida, akasafiri, akarekodi nyimbo?

Ni haki raia kuwanyooshea vidole wasanii wanapofanya mambo ya kusapoti wahuni? Nina hakika wapo wasanii hawakubaliani nayo mambo yao lakini wakidhubutu kutoa sauti nani atakuwa nyuma yao?

Siye raia kwa ujumla ndio wa kulaumiwa… Juzi, nchini Marekani, Trump aliwashinikiza Disney wamfungie Jimmy Kimmel kurusha late night show yake. Disney wakamfungia Jimmy Kimmel. Nini kilitokea baada ya hapo? Wamarekani wote kwa ujumla wao walitangaza kuisusia Disney plus(hii ni subscription kama zile za Azam). Na wengi wali cancel kabisa subscription. Eh! Mbona Jimmy Kimmel alirudishwa fasta fasta…

Tunalo tatizo la elimu ya uraia na wajibu wetu kama raia collectively.
 
Rule of the jungle,
Kufanikiwa kuwinda, hakumfanyi simba au chui kuwa na haki ya kula alichokipata, akitokea fisi anaweza akala mawindo na muwindaji akalala njaa,

Hiyo ndio Sababu simba huwinda Kwa makundi, lakini pia chui akikamata mawindo atapanda nayo juu ya mtu, Kwa bwana duma yeye atakula haraka haraka ili mpaka watakapofika awe ameshiba...

Wala hakuna uhusiano wowote, ma feeling ma feeling...
 
Uchawa uliaanzia hapa...

1759095426438.png
 
Wiki iliyopita ya mwezi huu wa September, ndugu Max Melo alitoa public lecture kwa watu wa TLS. Alielezea kwa ufasaha sana madhira aliyoyapata kwa kusimamia uhuru wa private information na JF kwa ujumla. Pamoja na kupewa kesi kama ugaidi 😆 na nyengine, his banking accounts were frozen, alizuiliwa kutoka nje ya Dar na visanga kibao…

Katika mazingira haya, ni msanii gani anaweza akapingana na mfumo na akawa salama? Akafanya show kawaida, akasafiri, akarekodi nyimbo?

Ni haki raia kuwanyooshea vidole wasanii wanapofanya mambo ya kusapoti wahuni? Nina hakika wapo wasanii hawakubaliani nayo mambo yao lakini wakidhubutu kutoa sauti nani atakuwa nyuma yao?

Siye raia kwa ujumla ndio wa kulaumiwa… Juzi, nchini Marekani, Trump aliwashinikiza Disney wamfungie Jimmy Kimmel kurusha late night show yake. Disney wakamfungia Jimmy Kimmel. Nini kilitokea baada ya hapo? Wamarekani wote kwa ujumla wao walitangaza kuisusia Disney plus(hii ni subscription kama zile za Azam). Na wengi wali cancel kabisa subscription. Eh! Mbona Jimmy Kimmel alirudishwa fasta fasta…

Tunalo tatizo la elimu ya uraia na wajibu wetu kama raia collectively.

-shemeji yenu Chivayo anawasabahi-
Wasanii wa Bongo wananunuliwa. Season ya uchaguzi inakuja na neema kubwa sana kwao kwa juhudi kidogo (more for less)!
 
Back
Top Bottom