Ukimtumia mtu mnayeheshimiana text meseji isiyofaa kimakosa unafanyaje?

Nilishawahi kumtumia message Shemeji yangu aliyemuoa Dada angu Mkubwa.

Message ilikua inaenda kwa mchepuko, ilikua inazungumzia Game ya jana yake ilivyokua ya Viwango, humo ndani hamna tasfida.

Kuja kugundua la haulaaaa. Nimemtumia mtu nayemweshimu sana kanizidi Umri mbali hafu ni Shemeji yangu.

Nikafikilia sekunde 3 nikasema kwanza yeye mwenyewe atakua na michepuko yake. Basi nikamtumia message ingine, nikamwambia samahani, nimekosea nilikua namtumia message mchepuko wangu.

Akanijibu kwa Emoji za kicheko then akasema Usijari.
 
Siku moja asubuhi naingia kazini boss alikuwa karudi kutoka kwenye vikao huko inaonekana alinang'wa sana kwa mambo yanayoendelea kituoni.

Hivyo saa kumi na mbili katuma ujumbe kila mtu awahi kabla ya muda wa kawaida kwa ambao hawakuwa zamu maana ana kikao cha dharura basi kwenye hiko kikao alitusema sana.

Basi kuna kademu kalikuwa ajira mpya na mimi ndiyo kamenizoea sana hivyo uwa kananiuliza vitu vingi kwa kutumia meseji tukiwa job.

Bosi alivyofura kwenye kikao kakawa hakana amani hivyo kakaanza kunichatisha punde kabla ya kumaliza kikao nikawa nakapa moyo huku namponda boss sana kuwa ni lijinga lijinga.

Asalale kutokana na uwingi wa kazi nikajikuta ile meseji ya alfajiri ya boss ndiyo nimereply na humo nimemsema boss kishenzi.

Nimekaa nataka nitoke walau nipate kifungua kinywa nasema wacha nione haka kademu kamejibuje laaa haula nakuta nilimjibu boss sio yule mrembo.

Nikakosa nguvu kwenye miguu na kichwa kikawa kizito sana , ile najikokota nitoke ofisini walau nikapate chochote kitu namuona boss anakuja uelekeo wa ofisi yangu , nikajikuta nguvu zinaniishia mara mbili nikaaa kwenye kiti huku nahemea juu.

Boss kufika nilipo kasema nina uhitaji na wewe ofisini kwangu , kiukweli sikwenda huko nilipotoka kwenda kunywa chai sikurudi kabisa.

Jioni nikatimkia mjini nikaenda zangu bar nikanywa bia zangu happ boss ashapiga simu mara kupiga , mpka kaamua amtumie yule ajira mpya kunipigia ila hakuna simu ya kima yeyote napokea.

Nilipolewa ndiyo nikamvutia waya akapokea ila akawa anauliza mbona nimekimbia nikawa sina cha kusema ila nikaamua kuomba msamaha na kumwambia japo nimemtusi sana ila mengi ni ukweli ila sisi ni wanaume anisamehe bana na pia nilifanya hivyo maana kale kadada nakataka hivyo anivumilie na kunisamehe.

Ndiyo ilikuwa mwanzo wa vita mimi na the boss mpaka wa leo.

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Rahisi sana fanya kwamba simu ilikuwa imeibiwa wakati sms inatumwa....; ikibidi weka simu yako katika sehemu hatarishi ili iibiwe kwahio chochote kilichofanyika at that time unaweza kusema (It wasn't me...)

Fanya sasa hivi sababu muda unavyozidi kwenda ndio window of opportunity inapungua / inakwisha kwahio kama wiki ishapita rudi kuomba tena ushauri nini kifanyike
 
Niliwai kosea SMS nikamtumia mama mkwe badala ya wife " nipo kwenye basi, nikifika kitu cha kwanza nakugonga vzr"

Nilipogundua, nikamsms kuwa hiyo SMS sio yake aachane nayo.
 
watu mpo makini sana 😂😂😂
 
Mpige simu mwambie ulikosea kutumia kwake,kama unaogopa labda atakuona unaandikia watu sms za hovyo mwambie ukimpa mtu simu akakosea kutuma sms kwako

Kwisha
 
Aiseee, tako laini rojorojo[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Umetisha kiongozi
 
Duuu, hahaha.
Pole mzee[emoji1787][emoji1787]
 
[emoji23][emoji23][emoji23]Mwamba, pitia K Vant 4 hapo kwa Mangi, nitakuja kulipa. Umeupiga mwingi sana mkuu
 
Acha uwoga acha ufala wewe ni wa kiume, piga simu au tuma ujumbe kuwa umekosea kwani wewe ni mwanadamu hujakamilika kukosea ni kawaida Sana kwa bahati mbaya au makusudi yote ni kukosea, usiwe mwoga kisha una mheshimu
Wewe wasema, Je kama amemtumia baba yake sms ya ajabu mfano "kalia mboo" badala ya "Kalia ndoo"
 
Tuma msg nyingine fanya kama unaomba mchango wa hela ya matibabu kwenda India next week weka crazy amount usitaje tatizo au ugonjwa.
Kama ukikutafuta usipokee wala kujibu sms after 1-2 days akikutafuta mwambie simu ulipoteza simu.
😁
 
Hapo ni kujifanya simu iliibiwa bhc hakuna kingn Ila inategemeana na mtu huyo Kama ni mwelewa ataelewa tu,na ikiwa ni baba mwambie rafiki yangu nilimwachia simu yangu akapige picha ndo akakosea kutuma sms
 
Hapo ni kujifanya simu iliibiwa bhc hakuna kingn Ila inategemeana na mtu huyo Kama ni mwelewa ataelewa tu,na ikiwa ni baba mwambie rafiki yangu nilimwachia simu yangu akapige picha ndo akakosea kutuma sms
 
Sasa ikatokea sina dakika... Nima meseji na sijui kujielezea kwa meseji nitafanya nn
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…