Ukimuondoa Zamalek Kombe la Shirikisho naomba, wanitajie timu ambayo ingeweza kuichalenge Yanga hii iliyotolewa Klabu Bingwa!

Makavuli

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2024
Posts
1,425
Reaction score
1,829
Ningependa mbumbumbu wanaoicheka Yanga kushindwa kufuzu hatua ya robo fainali klabu bingwa wanitajie timu ambazo zingeweza kuipa Yanga hii changamoto yoyote Ile kwenye kombe ilo walilopo la washindi wa 3 na 4!

Nimemuondoa Zamalek kwakuwa ndio timu pekee ambayo ingeweza kupambana na Yanga kupimana ubavu but timu zote zilizobaki kwenye icho kikombe cha Asante Mosepe zilizoingia hatua ya makundi akuna ata Moja ingeweza kusimama mbele ya yanga hii mnayoibeza!

Hatua ya makundi klabu bingwa ni sawa na kucheza nusu fainali ya kombe la shirikisho iyo muiweke vichwani mwenu!

Nimewapa iyo home work kwakuwa timu zote nimeziona zinazocheza shirikisho ili kuingia robo fainali mnitajie ni timu Gani ingemsimamisha Yanga!

Ndio maana nawaambia ubora wa Klabu Bingwa na shirikisho ni mbingu na ardhi ni sawa na shabiki wa timu insyoshiriki daraja la nne kujilinganisha na timu inayocheza ligi kuu inakuwa ni kufurahisha genge tu ili siku ziende!

Na wengine wakishashiba viporo vya magimbi wakavimbiwa akili uwa zinahama wanaanza kuleta reference za ajabu ajabu,,

Mwenzako anakunja bilioni 1.9 kwa kuishia makundi nafasi ya tatu wewe iyo unaipata endapo tu utafika nusu fainali ya Asante Mosepe,,na bado unavua mpaka boksa eti umeongoza kundi la wagonjwa ni maajabu ya Musa!
 
Hizo nguvu zooote unazotumia, je, hujui kuwa hilo kombe ndo limeiweka yanga kwenye ranking iliyopo? Uliona wakitoa point za shirikisho na kuziweka pembeni kuwa ni kombe la kipuuzi? Ukitaka kujua umuhimu wa hili kombe, toa point za Yanga ilizozipata kwenye shirikisho halafu uweke ranking, yanga atakuwa wa ngapi bila hizo point? Hitimisho..kutoka ni kutoka tu, hutoirudisha yanga kwenye robo fainali hata uandike nyuzi mia za kuponda kombe la shirikisho ambalo timu yako ilichukua medali.
 
Mnaferi mitihani kutokana na kukosa maarifa,,ujanijibu nilichouliza, nimewauliza nyie si mnaicheka yanga iliyotolewa klabu bingwa kwamba ni mbovu basi mnitajie timu mojawapo iliyopo uko kwenu ambayo inaweza kuifunga yanga hii,,taja ata hizo zilizoingia robo fainali
 
Simba alifuzu Club Bingwa yenye Jobe, Saido, Babacar Sar na mwamba Fredy Michael.

Nyinyi mna Pacome, Chama, Azizi Ki, Aucho, Diarra, Mzize, Musonda, Dube na bado mmetupwa kama tishu iliyotoka kufuta uchafu.

So kimsingi hamna sababu yenye mashiko inayoweza ku justify ujinga wenu au ubovu wenu au vyote kwa ujumla kuonesha kwanini hamjafuzu.
 
Hii inakusaidia vipi kupunguza maumivu ya kutolewa hatua ya makundi?

Tukishakutajia hizo timu YANGA ndio itaenda robo fainali?

Halafu YANGA kuliwa kiboga na kutolewa kwenye makundi sisi SIMBA inatuhusu nini?

Halafu wewe unatuuliza kama nani?
 
Wewe ndio unafeli na ndio maana unaandika "wanaferi"

Unaanzaje kuzitoa timu ambazo zimestahili kuwa hapo zilipo kupitia ubora wao halafu bila aibu ukajiweka wewe ili ujifanyie comparison wakati kipimo cha comparison ambacho ni mechi 6 kimekuengua?
 
Hii inakusaidia vipi kupunguza maumivu ya kutolewa hatua ya makundi?

Tukishakutajia hizo timu YANGA ndio itaenda robo fainali?

Halafu YANGA kuliwa kiboga na kutolewa kwenye makundi sisi SIMBA inatuhusu nini?

Halafu wewe unatuuliza kama nani?
Mbona zipo mbinu nyingi tu za kupunguza maumivu nimeshangaa alivyokuja na porojo za kujifariji za kipuuzi kiasi hiki
Haya kwahiyo tukimwambia hakuna timu inayomzidi yeye ndio anakuwa kavuka robo fainali?
 
Kwahiyo umeshaona klabu bingwa sio level zako tena unatamani ya Shirikisho?
Wewe uliyeshindwa kufunga hata goli moja dk 180 dhidi ya MC Alger hata ungepewa Constatine angekukalisha kirahisi tu
Mnajitoa sana ufahamu nyie watu, uwezi kuelewa maana yangu kama auna D-2,,ni kwamba usilinganishe ubora wa timu unazocheza nazo uko na ubora wa timu zilizoko klabu bingwa,,narudia Tena shirikisho ni shirikisho tu na ndio maana wanashindanishwa washindwa kwa washindwa upo hapo!
 
Wewe ndio unafeli na ndio maana unaandika "wanaferi"

Unaanzaje kuzitoa timu ambazo zimestahili kuwa hapo zilipo kupitia ubora wao halafu bila aibu ukajiweka wewe ili ujifanyie comparison wakati kipimo cha comparison ambacho ni mechi 6 kimekuengua?
Zimefika kwa ubora wao upi? Mechi 6 zimeniengua kwenye michuano ya aina Gani fafanua na ufafanue michuano uliyopo pia na ubora wa timu zilizoko uko!
 
Zimefika kwa ubora wao upi? Mechi 6 zimeniengua kwenye michuano ya aina Gani fafanua na ufafanue michuano uliyopo pia na ubora wa timu zilizoko uko!
Wewe utachekwa na watu hapa haubishani na shabiki wa Azam ambaye hajui kitu kuhusu Club Bingwa.

Mimi Club Bingwa nimefika robo fainali nikiwa na Babacar Sar, Jobe, Saido, na Fredy Michael. So kama ubovu wa timu ndio unaofanya mashindano yawe mepesi basi mimi nisingeweza kufuzu kwenda robo fainali kwa aina ya timu niliyokuwa nayo.


Sisi ndio tumewapa clue ya kujua kumbe kuna mashindano ya Club Bingwa na nyie ndio mkaanza kuweka focus.

So unavyo argue uwe unajenga hoja ukijua una argue na mtu ambaye anaelewa kila kitu kuhusu Club Bingwa.
 
Kwani kuwa klabu bingwa kuna kitu gani cha ajabu au nyie ndio mnajiona wa kwanza kuwa klabu bingwa?
Suala lilipo mezani ni nyie kuishia makundi huko klabu bingwa na wala sio suala la ugumu wa michuano maana hilo linajulikana na wewe ulienda kama bingwa wa ligi sasa inakuwaje unashindwa kuvuka hata hatua ya makundi ukafie hata hapo robo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…