Ukimwezesha Mwanamke wako unajichimbia kaburi lako mwenyewe

magumbugu

Senior Member
Joined
Sep 27, 2017
Posts
143
Reaction score
266
Mapenzi kuvunjika ni sehemu ya kawaida kabisa kwa maisha ya sasa lakini kuna jambo la kuzingatia hapa.
Mapenzi huwa yanauma sana pale ambapo mwenza wako anaondoka anakuacha ghafla ukiwa mpweke kipindi kigumu sana kwako kama vile anakuacha umepauka, unanuka jasho, umefubaa, unavaa nguo zimechakaa na zimepauka,anakuacha ukiwa mgonjwa sana,anakuacha ukiwa umekonda sana,anakuacha wakati ambao jamii imekutenga,anakuacha wakati ambao hauna hata rafiki wa karibu wa kuzungumza naye.

Hapo unaweza kuwachukia wanaume au wanawake wote kwa kusema "Wanaume wote ni mbwa" au "Wanawake wote ni mbwa" lakini kosa sio la mwenza wako bali kosa umefanya wewe mwenyewe kwa mikono yako.

TUANGALIE MAISHA YA MWANAMKE WA KISASA
Binti akiwa na umri wa miaka 18-29 ,akiwa na muonekano mzuri sana,akiwa na fedha,akiwa na kazi,akiwa hajazaa,akiwa hajaanza kunywa pombe,bado hajatumia dawa za uzazi wa mpango,bado hajatoa mimba, hajalala na waume za watu, hapo huonyesha dharau, majivuno, kiburi, ujuaji, ubishi, utemi, anakuwa hashauriki, anakuwa mkali kupitiliza, anakuwa mkosoaji kupitiliza,anakuwa anaporomosha matusi ya nguoni mara kwa mara anapokwazana na watu wake wa karibu,

kila mwanaume mwenye malengo naye anamuona takataka,anamuona bwege,anamuona mshamba,anamuona amepitwa na wakati,akiwa ushauri wowote kuhusu maisha anaona hayo ni maneno ya watu wa kale yamepitwa na wakati.

wakati huo huanza kujenga urafiki na marafiki au wanaume wenye tabia za ubabe, ukali kupitiliza, kiburi, ujuaji, misimamo mikali sana,ulevi kupindukia, uvutaji bangi, utumiaji wa dawa za kulevya, wizi,wanaume waliojichora tattoo,wanaume wavaa mlegezo,wanaume wenye wenye sifa mbaya kwbeye jamii, vilevile hauna kujenga mahusiano ya kimapenzi na waume za watu kwa sababu vijana wadogo anawaona sio wa HADHI yake,

-Hapo huanza kunywa pombe,kwenda night club, atashiriki mapenzi na kila mwanaume anaekuja usoni mwake ilimradi yupo na fedha,anaanza kutumia dawa za uzazi wa mpango,au ataanza kutoa mimba mfululizo, anaweza,au anaweza kuzaa kila mtoto na baba yake kwa sababu anakuwa hana uvumilivu kwa maana ugomvi kidogo tu anasusa,anaondoka zake.

Anapofika miaka 30+ hana mwanaume yoyote wa kueleweka,hana mtoto labda kizazi hana kwa sababu ya kutoa mimba mfululizo,na kutumia dawa za uzazi wa mpango,au tayari amezaa kila mtoto na baba yake.

muda huo wa miaka 30+,waume za watu huondoka mmoja mmoja kwa sababu wengine hurudi kwenye familia zao ,wengine huanza kuchagua mabinti wadogo wenye umri wa miaka baina ya 18-29.

Hivyo hapo anajikuta ni mpweke sana ,hana mwenza isipokuwa waume za watu au vijana wadogo ambao wanamtumia kwa starehe.

akiwa amepauka, amefubaa, ananuka, anaumwa sana, ametengwa na jamii,anapigwa vita kila kona,hana kazi yoyote, wala hana biashara yoyote,hana akiba ya fedha hapo huona kwamba kimbilio lake ni kupata mwanaume mpole kupitiliza, mvumilivu, mnyenyekevu, muadilifu,mwenye hofu ya Mungu.

Akimpata mwanaume huyo hauna kumpangia sheria na kumpa masharti magumu sana ili waweze kuwa wenza.

Baada ya mwanaume mpole kupitiliza, mvumilivu sana, mnyenyekevu, muadilifu, mwaminifu,mwanaume ambaye ni mwenye malengo naye kujitoa mhanga kumfariji, kumliwaza, kumtetea kumpa mtaji, kumchukulia mkopo, kumfungulia biashara, kumtafutia kazi, kumjengea, kusaidia ndugu zake mwanamke, kuwafungulia biashara ndugu zake mwanamke,

Mwanamke huyohuyo baada ya kusimama vizuri kiuchumi,akiona ameanza kupendeza, amekuwa na afya njema,watoto zake ambao alitelekezwa nao wamesomeshwa huamua kuibua ugomvi kisha anarudi kwa Ex wake kwa madai kwamba hataki watoto zake kuchanganya damu .

mwanaume huona bora aanze kuomba msamaha, kupiga magoti, kutishia kujiua, kutuma sms mfululizo, kupiga simu mfululizo, kutuma pesa kibao ili kumshawishi warudiane, lakini Mwanamke huyohuyo huamua kumjibu kwa dharau kwa kusema "SIJAKULAZIMISHA UNIFANYIE YOTE HAYA"

KWANINI UNAPOFANYA UWEKEZAJI MKUBWA SANA KWA MWENZA WAKO UNAKUWA UMEJICHIMBIA KABURI WEWE MWENYEWE?
Angalia hapa chini
-Mwenza wako amesoma kwa fedha zako wakati huohuo wewe haujaenda shule,mwenza wako anakuwa anamiliki biashara kubwa ambayo mtaji umetoa wewe wakati huohuo wewe hauna kazi yoyote ya kueleweka.

-Mwenza wako anakuwa anang'aa kwa kuvaa nguo za gharama lakini fedha umetoa wewe wakati huohuo wewe umepauka, unanuka, umekonda,umefubaa kwa sababu ya kujitoa mhanga ili kumfurahisha na kumthibitishia kwamba ûnampenda sana kuliko mtu au kitu chochote hapa ulimwenguni

-Mwenza wako anakuwa anamiliki nyumba ambayo umemjengea kwa fedha zako wakati huohuo wewe hauna hata kiwanja
-Mwenza wako anakuwa anamiliki gari zuri wakati huohuo wewe hauna hata baiskeli

-Mwenza wako anakuwa anamiliki simu ya gharama umemnunulia kwa fedha zako wakati huohuo wewe unatumia simu ya batani/ kiswaswadu/ kitochi

Kwanini mwenza wako anaposimama vizuri kiuchumi anakuacha ghafla bila kujali jasho lako kwake ?Kumbuka binti anapokuwa na umri wa miaka 18-29 wakati huo yupo na "shape" nzuri,yupo na fedha,labda amesoma,au yupo na kazi nzuri halafu wanaume wengi wanamtongoza je huwa wanaonyesha tabia gani ?

Kwa asili Mwanamke akiwa na fedha, muonekano mzuri,kazi nzuri, elimu huwa mwenye kuonyesha dharau, kiburi, ujuaji, misimamo mikali, utemi, anakuwa hashauriki, anakuwa mkali kupitiliza, anakuwa mkosoaji kupitiliza,anakuwa haambiliki kwa sababu anajua hauwezi kumuacha wala hauwezi kuishi bila yeye au hata kama Mtaachana anajua wanaume wengi wanamtaka hivyo anakuwa na uhakika wa kuziba pengo lako.

Wapo wanawake wachache sana wenye kuonyesha huruma, kujali, kunyenyekea, uvumilivu wakati huohuo anakuwa na muonekano mzuri,anakuwa na elimu,anakuwa na kazi.

Kwa asili Mwanamke huwa anatafuta mwenza ambaye yupo na uwezo mkubwa sana wa kielimu, cheo, umaarufu,fedha,nguvu ya ushawishi, mamlaka kumzidi na vilevile Mwanamke anajiona yupo na mafanikio makubwa sana kuliko wanaume wengi huona kwamba hapo hakuna mwanaume wa ndoto zake au HADHI yake.

Kwa asili mwanaume anapotaka Mwanamke huwa anatazama Mwanamke ambaye yupo chini kwake iwe kiuchumi, kielimu, cheo, umaarufu, nguvu ya ushawishi ili kuepuka usumbufu wa kugombania mamlaka ndani ya familia.

Asili ya Mwanamke kutaka mwanaume ambaye anamzidi kila kitu haiondoki,hata kama Mwanamke atakuwa na mafanikio makubwa sana bado atahitaji kuhudumiwa.

Mwanamke hata kama atakuwa na fedha nyingi sana bado atahitaji kuhudumiwa,hiyo basi pale ambapo anamuona mwanaume wake hana kazi yoyote, hana biashara yoyote,amekonda, amepauka, amefubaa, ananuka jasho moja kwa moja huona huyo sio mwanaume wa HADHI yake.

Kwa kuhitimisha ni kwamba kama wewe ni mwanaume unapofanya uwekezaji kwa Mwanamke kuliko kwako unakuwa unampa tiketi ya kukuacha aende kwa wanaume ambao ataona ni wa HADHI yake kwa sababu sio hulka ya Mwanamke kumhudumia mwanaume.

Unapomjengea mwenza wako nyumba unakuwa unampa nguvu ya kukufukuza kwenye nyumba hiyo hata kama fedha umetoa wewe,unapomfungulia mwenza wako biashara kwa jina lake unakuwa unampa nguvu ya kukufukuza kwenye biashara hiyo pale ambapo utakuwa hauna hauna fedha.

kula vizuri, vaa vizuri, tumia manukato mazuri,tumia simu nzuri, tembelea sehemu zenye kuvutia kabla ya kumjali mwenza wako.
Mwenza wako hawezi kuthamini jasho lako kwake isipokuwa atakuwa anathamini sana jasho lake kwako na ikiwa hajafanya uwekezaji wowote kwako maana yake hana cha kupoteza endapo mtaachana.
 
Kila mtu ataumia kwa wakati wake haijalishi unawekeza au hauwekezi .. kataa ndoa wako sehemu salama zaidi .. nawasilisha.
 
Asili ya Mwanamke kutaka mwanaume ambaye anamzidi kila kitu haiondoki,hata kama Mwanamke atakuwa na mafanikio makubwa sana bado atahitaji kuhudumiwa.
Miaka ya nyuma niliwahi kufanya kazi kwenye hizi NGO za Trump, basi tulikuwa na Dada Mmoja mkali sana kutoka Nigeria, alikuwa analipwa Salary 20M za Kitanzania.

Kila siku alikuwa akiniambia anatamani apate Bwana Mwenye hela zake ataacha kazi.

Alikuwa boss wangu kwenye ngazi za kazi. Nilikuwa nawaza kumbe wanawake wote wanafanan aliyesoma na ambaye hajasoma. Wa Tanzanja uswazi na Nigeria Lagos.

🤣🤣🤣🤣
 
Naked truth, wanawake wasomi, wenye status na kazi nzuri ni ndoto ya vijana wengi wa kisasa!

Ila kuishi nao inabidi kuna muda ujizime data!
 
Maelezo marefu vya kutosha kumshambulia mwanamke aliye kosea!
Bro, kuosea kwa namna yoyote ile kwa mwanamke jua kumetanguliwa udhaifu wa mwanaume.
 
Mapenzi kuvunjika ni sehemu ya kawaida kabisa kwa maisha ya sasa lakini kuna jambo la kuzingatia hapa.
Mapenzi huwa yanauma sana pale ambapo mwenza wako anaondoka anakuacha ghafla ukiwa mpweke kipindi kigumu sana kwako kama vile anakuacha umepauka, unanuka jasho, umefubaa, unavaa nguo zimechakaa na zimepauka,anakuacha ukiwa mgonjwa sana,anakuacha ukiwa umekonda sana,anakuacha wakati ambao jamii imekutenga,anakuacha wakati ambao hauna hata rafiki wa karibu wa kuzungumza naye.

Hapo unaweza kuwachukia wanaume au wanawake wote kwa kusema "Wanaume wote ni mbwa" au "Wanawake wote ni mbwa" lakini kosa sio la mwenza wako bali kosa umefanya wewe mwenyewe kwa mikono yako.

TUANGALIE MAISHA YA MWANAMKE WA KISASA
Binti akiwa na umri wa miaka 18-29 ,akiwa na muonekano mzuri sana,akiwa na fedha,akiwa na kazi,akiwa hajazaa,akiwa hajaanza kunywa pombe,bado hajatumia dawa za uzazi wa mpango,bado hajatoa mimba, hajalala na waume za watu, hapo huonyesha dharau, majivuno, kiburi, ujuaji, ubishi, utemi, anakuwa hashauriki, anakuwa mkali kupitiliza, anakuwa mkosoaji kupitiliza,anakuwa anaporomosha matusi ya nguoni mara kwa mara anapokwazana na watu wake wa karibu,

kila mwanaume mwenye malengo naye anamuona takataka,anamuona bwege,anamuona mshamba,anamuona amepitwa na wakati,akiwa ushauri wowote kuhusu maisha anaona hayo ni maneno ya watu wa kale yamepitwa na wakati.

wakati huo huanza kujenga urafiki na marafiki au wanaume wenye tabia za ubabe, ukali kupitiliza, kiburi, ujuaji, misimamo mikali sana,ulevi kupindukia, uvutaji bangi, utumiaji wa dawa za kulevya, wizi,wanaume waliojichora tattoo,wanaume wavaa mlegezo,wanaume wenye wenye sifa mbaya kwbeye jamii, vilevile hauna kujenga mahusiano ya kimapenzi na waume za watu kwa sababu vijana wadogo anawaona sio wa HADHI yake,

-Hapo huanza kunywa pombe,kwenda night club, atashiriki mapenzi na kila mwanaume anaekuja usoni mwake ilimradi yupo na fedha,anaanza kutumia dawa za uzazi wa mpango,au ataanza kutoa mimba mfululizo, anaweza,au anaweza kuzaa kila mtoto na baba yake kwa sababu anakuwa hana uvumilivu kwa maana ugomvi kidogo tu anasusa,anaondoka zake.

Anapofika miaka 30+ hana mwanaume yoyote wa kueleweka,hana mtoto labda kizazi hana kwa sababu ya kutoa mimba mfululizo,na kutumia dawa za uzazi wa mpango,au tayari amezaa kila mtoto na baba yake.

muda huo wa miaka 30+,waume za watu huondoka mmoja mmoja kwa sababu wengine hurudi kwenye familia zao ,wengine huanza kuchagua mabinti wadogo wenye umri wa miaka baina ya 18-29.

Hivyo hapo anajikuta ni mpweke sana ,hana mwenza isipokuwa waume za watu au vijana wadogo ambao wanamtumia kwa starehe.

akiwa amepauka, amefubaa, ananuka, anaumwa sana, ametengwa na jamii,anapigwa vita kila kona,hana kazi yoyote, wala hana biashara yoyote,hana akiba ya fedha hapo huona kwamba kimbilio lake ni kupata mwanaume mpole kupitiliza, mvumilivu, mnyenyekevu, muadilifu,mwenye hofu ya Mungu.

Akimpata mwanaume huyo hauna kumpangia sheria na kumpa masharti magumu sana ili waweze kuwa wenza.

Baada ya mwanaume mpole kupitiliza, mvumilivu sana, mnyenyekevu, muadilifu, mwaminifu,mwanaume ambaye ni mwenye malengo naye kujitoa mhanga kumfariji, kumliwaza, kumtetea kumpa mtaji, kumchukulia mkopo, kumfungulia biashara, kumtafutia kazi, kumjengea, kusaidia ndugu zake mwanamke, kuwafungulia biashara ndugu zake mwanamke,

Mwanamke huyohuyo baada ya kusimama vizuri kiuchumi,akiona ameanza kupendeza, amekuwa na afya njema,watoto zake ambao alitelekezwa nao wamesomeshwa huamua kuibua ugomvi kisha anarudi kwa Ex wake kwa madai kwamba hataki watoto zake kuchanganya damu .

mwanaume huona bora aanze kuomba msamaha, kupiga magoti, kutishia kujiua, kutuma sms mfululizo, kupiga simu mfululizo, kutuma pesa kibao ili kumshawishi warudiane, lakini Mwanamke huyohuyo huamua kumjibu kwa dharau kwa kusema "SIJAKULAZIMISHA UNIFANYIE YOTE HAYA"

KWANINI UNAPOFANYA UWEKEZAJI MKUBWA SANA KWA MWENZA WAKO UNAKUWA UMEJICHIMBIA KABURI WEWE MWENYEWE?
Angalia hapa chini
-Mwenza wako amesoma kwa fedha zako wakati huohuo wewe haujaenda shule,mwenza wako anakuwa anamiliki biashara kubwa ambayo mtaji umetoa wewe wakati huohuo wewe hauna kazi yoyote ya kueleweka.

-Mwenza wako anakuwa anang'aa kwa kuvaa nguo za gharama lakini fedha umetoa wewe wakati huohuo wewe umepauka, unanuka, umekonda,umefubaa kwa sababu ya kujitoa mhanga ili kumfurahisha na kumthibitishia kwamba ûnampenda sana kuliko mtu au kitu chochote hapa ulimwenguni

-Mwenza wako anakuwa anamiliki nyumba ambayo umemjengea kwa fedha zako wakati huohuo wewe hauna hata kiwanja
-Mwenza wako anakuwa anamiliki gari zuri wakati huohuo wewe hauna hata baiskeli

-Mwenza wako anakuwa anamiliki simu ya gharama umemnunulia kwa fedha zako wakati huohuo wewe unatumia simu ya batani/ kiswaswadu/ kitochi

Kwanini mwenza wako anaposimama vizuri kiuchumi anakuacha ghafla bila kujali jasho lako kwake ?Kumbuka binti anapokuwa na umri wa miaka 18-29 wakati huo yupo na "shape" nzuri,yupo na fedha,labda amesoma,au yupo na kazi nzuri halafu wanaume wengi wanamtongoza je huwa wanaonyesha tabia gani ?

Kwa asili Mwanamke akiwa na fedha, muonekano mzuri,kazi nzuri, elimu huwa mwenye kuonyesha dharau, kiburi, ujuaji, misimamo mikali, utemi, anakuwa hashauriki, anakuwa mkali kupitiliza, anakuwa mkosoaji kupitiliza,anakuwa haambiliki kwa sababu anajua hauwezi kumuacha wala hauwezi kuishi bila yeye au hata kama Mtaachana anajua wanaume wengi wanamtaka hivyo anakuwa na uhakika wa kuziba pengo lako.

Wapo wanawake wachache sana wenye kuonyesha huruma, kujali, kunyenyekea, uvumilivu wakati huohuo anakuwa na muonekano mzuri,anakuwa na elimu,anakuwa na kazi.

Kwa asili Mwanamke huwa anatafuta mwenza ambaye yupo na uwezo mkubwa sana wa kielimu, cheo, umaarufu,fedha,nguvu ya ushawishi, mamlaka kumzidi na vilevile Mwanamke anajiona yupo na mafanikio makubwa sana kuliko wanaume wengi huona kwamba hapo hakuna mwanaume wa ndoto zake au HADHI yake.

Kwa asili mwanaume anapotaka Mwanamke huwa anatazama Mwanamke ambaye yupo chini kwake iwe kiuchumi, kielimu, cheo, umaarufu, nguvu ya ushawishi ili kuepuka usumbufu wa kugombania mamlaka ndani ya familia.

Asili ya Mwanamke kutaka mwanaume ambaye anamzidi kila kitu haiondoki,hata kama Mwanamke atakuwa na mafanikio makubwa sana bado atahitaji kuhudumiwa.

Mwanamke hata kama atakuwa na fedha nyingi sana bado atahitaji kuhudumiwa,hiyo basi pale ambapo anamuona mwanaume wake hana kazi yoyote, hana biashara yoyote,amekonda, amepauka, amefubaa, ananuka jasho moja kwa moja huona huyo sio mwanaume wa HADHI yake.

Kwa kuhitimisha ni kwamba kama wewe ni mwanaume unapofanya uwekezaji kwa Mwanamke kuliko kwako unakuwa unampa tiketi ya kukuacha aende kwa wanaume ambao ataona ni wa HADHI yake kwa sababu sio hulka ya Mwanamke kumhudumia mwanaume.

Unapomjengea mwenza wako nyumba unakuwa unampa nguvu ya kukufukuza kwenye nyumba hiyo hata kama fedha umetoa wewe,unapomfungulia mwenza wako biashara kwa jina lake unakuwa unampa nguvu ya kukufukuza kwenye biashara hiyo pale ambapo utakuwa hauna hauna fedha.

kula vizuri, vaa vizuri, tumia manukato mazuri,tumia simu nzuri, tembelea sehemu zenye kuvutia kabla ya kumjali mwenza wako.
Mwenza wako hawezi kuthamini jasho lako kwake isipokuwa atakuwa anathamini sana jasho lake kwako na ikiwa hajafanya uwekezaji wowote kwako maana yake hana cha kupoteza endapo mtaachana.
Bro, kwanza kutendwa ni kitu cha kawaida, umuwezeshe, au, usimwezeshe, kama kuliwa ataliwa tu,
Pili,MTU ambae umeanzisha nae familia, haiwezi kuwa vibaya kumuwezesha kiuchumi, fikiria ukidondoka ghafla(wanaume hufa mapema), uzao,wako utaishi visit, kama hu kumuwezesha kiuchumi!? Princess na junior wapo feza pale, ghafla unadondoka, harafu vijana wako wanaenda kawe primary! Bro kuwa serious,
We muwezeshe tu, swala kupigwa na kitu kizito, ishi nalo tu, dunia ya Leo, ndio ilivyo,
Una mpa mke Prado VX, anaenda kuvuliwa chupi, na kijana jobless hapo kitaani,!
It's life bro, tubadirike kidogo haiwezekani mpaka Leo, bado kuna watu wanaogopa kutendwa!
 
Back
Top Bottom