Ukimwi hauonekani kwa macho, namshukuru MUNGU wangu

Ukimwi hauonekani kwa macho, namshukuru MUNGU wangu

Makuke

New Member
Joined
Jul 19, 2015
Posts
4
Reaction score
28
( true story)

Ilikua ni siku ya Jumamosi majira ya saa sita mchana nikiwa nachezea PC nikiangalia Movie, ndipo nilipowaka tamaa ya mapenzi iliyojawa na hatari kubwa ndani yake,

Ndipo nilipoamua kuchukua simu yangu na kwa haraka kuingia katika orodha ya majina niliyoyasave kwenye simu kwa lengo la kumtafta msichana mmoja aliyefahamika kwa jina la Suzana.

kabla ya kuendelea: kwanza napenda nirudi nyuma kidogo, Suzana (Suzy) ni msichana ambae nilifahamiana nae kwa muda wa miezi isiyopungua miwili sasa, nilifahamiana nae kipindi alipokuja hospitali kumuuguza bibi yake ambae alikua mgonjwa, kwa mara ya kwanza sikuvutiwa nae kabisa msichana huyo, lakini kadri muda ulivyokuwa ukienda nilijikuta nazoeana nae sana kiasi cha kuomba namba yake ya simu kama kumjaribu kama atakubali au la!, Suzy alikubali kunipa namba yake na baada ya masaa kadhaa mgonjwa wa Suzy aliruhusiwa kuondoka kwani alikua akiendelea vizuri, suzy aliniaga na kuondoka,

Kiukweli kwakua sikuwa na hamu yoyote na Suzy bas haikuwa rahisi kumtafta kwa mda ule,. Zilipitta siku mbili tangu nionane na Suzy bila kumtafta(huenda labda nae alikata tamaa na labda alihisi sikuisave number yake ya simu aliyonipa), ilipofika majira ya saa moja jioni nilimtafta Suzy na kujitambulisha kwake, Suzy alifurahi sana kuskia ni mimi niliemtafta, baada ya hapo tulikuwa marafiki wa karibu sana na mwisho wa siku tulikuwa wapenzi, lakini jambo lisilo la kawaida ni pale ambapo kila tulipokuwa tukipanga kuonana na Suzy kwaajili ya kusex, kulikua kunajitokea dharula ambayo inakua nje ya uwezo wetu na tunaacha kukutana,

Jana ndio siku ya Jumamosi ninayoizungumzia, tuliahidiana kukutana na Suzy kwa lengo la kufanya Mapenzi Gest, safari hii hapakuwa na dharula kama siku nyingine, mimi ndio nilikuwa mtu wa kwanza kufika Gest na kumuelekeza ni wapi anikute, baada ya muda kama wa dakika 20 za kumsubili mara Suzy alifika akiwa amevaa Suruale Jeans iliyobana na yenye kushawishi kufanya nae mapenzi, lakini baada ya kufika na kupiga story mbili tatu, nilimuomba kumpima Virusi Vya Ukimwi, kwakuwa vipimo nilikuwa navyo na nilienda navyo kwa bahati nzuri baada ya kusahau kuvitoa katika suruale niliyokuwa nimevaa jana yake, baaada ya kuomba kumpima, Suzy alikataa kupima na kusema kuwa hayuko tayari kupima bila hiyari yake na kidogo alichukia,

Lakini baada ya kumsoma kuwa nae alitamani sana kushiliki na mimi, nilijifanya navaa viatu kuondoka ndipo aliponiambia nirudi ili nimpime, lakini kabla ya kumpima aliniambia anaomba aniulize maswali mawili, 1. Je ukinipima na ukanikuta Sina??, nikamjibu “hakuna shida kama utakuwa mzima”

Akauliza tena: na je ukinikuta ninao?? Nikamjibu “hakuna tatizo pia kwani nitajua nini cha kufanya” kisha akasema kuwa yeye anataka mtu wa kumuoa na sio kumchezea na kama kupima basi iwe siku nyingine na sio siku hiyo kwani sikumtaarifu,. Wakati huu sasa sikuwa na mzaha baada ya kuona anataka kukataa tena kupima, nikaamua kuvaa na nilipokua nafunga kamba za viatu akaniuliza tena Kwani tunafanya bila Condom??, (kiukweli Condom nilikua nazo mfukoni lakini baada ya kuonyesha wasiwasi na afya yake nilimdanganya kuwa tunafanya bila Condom kwasababu sina, ili nione atasemaje baada ya hapo, ndipo aliponishika mkono kunizuia nisifunge kiatu na kusema tulale nikwambie kitu, nikamsikiliza ,

Akaanza kwa kusema “kunipima utanipima kwakuwa vipimo unavyo” lakini ukweli ni kwamba mimi NIMEATHIRIKA na nipo katika dozi,. daah!! Moyo wangu ulilipuka kwa hofu lakini nilihisi labda ananitania ili kuona nitachukua uamuzi gani baada ya yeye kusema hivyo, mimi niliamua kumuuliza kama kweli anao je ameupata lini??, akasema ni story ndefu huku akilia na chaajabu mda huu alikua mwepesi kunipa mkono wake ili nimpime huku akisema hakikisha mwenyewe kama huamini,

Mimi niliona ngoja nihakiki kama ni kweli au anatania, mara baada ya kumpima, Vipimo kweli vilionyesha ni kweli AMEATHIRIKA, daaah!!! akili yangu mda huu ilikua na wasiwasi sana nayeye na mpaka niliogopa kumshika, lakini niliwaza nikamwambia “ skia Suzy hii ni hali ya kawaida wala usiwaze sana kwani wapo watu wengu huwa na huu ugonjwa na wanaishi mpaka leo” japo moyoni nilikua na hasira huku nikiwaza kwanini alikua hataki tupime kama kweli alijua yeye ni mgonjwa, lakini nilimshukuru MUNGU kwa kuniongoza mpaka kuamua kumpima na pamoja na dharula zote Mungu alizoziweka ili tusionane siku zote tulizojuana,.

Baada ya hapo nilijifanya nina dharula na kuweka alarm kama kuna mtu ananihitaji ili niondoke kwani alianza kuniuliza ni nini hatma yetu, lakini ili kumtoa wasiwasi zaidi nilimwambia “ningekua na Condom tungefanya”(nawakati nilikua nazo), pia ili kumtoa wasiwasi zaidi nilimdanganya kuwa “ naenda ninapoitwa lakini narudi na Condom ili tufanye, lakini mda huu alisema “ wala usihangaike kununua Condom mimi sitaki kumuambukiza mtu nenda ila urudi tupige story pia akasema ila ukichelewa kurudi uniambie” ndipo nilipoondoka na baadae kumtumia meseji kuwa imeshindikana kurudi,.

HINT: mimi sio muandishi wa vitabu saa nyingine naweza kuwa sijafata taratibu za uandishi wa story lakini nia yangu si kuburudisha ni kutoa elimu kwa vijana wenzangu kuwa Ukimwi hauonekani kwa macho,

Zaidi sana namshukuru MUNGU wangu kwa ufunuo na wokovu wa ajabu juu yangu kwa siku ya Jana na Siku zote.,
 
kumbe tunatiana moyo tu mtaani,bado ukimwi unaogofya kwa mliopata hilo nijaribu mtarishinda,ambao bado take,n.b condom sio tiba ni kinga isiyo 100 percent effective
 
Nawaona wakina suzy hisa zikishuka kwa kasi ya ajabu
 
Kwakua hujasema anakaa wapi..kuanzia sasa naanza kwa Ku delete namba za kina Suzi wawili kwenye simu yangu...ctaki ujinga
 
Back
Top Bottom