Ukimwi wamfikisha Mahakamani!!!

MaxShimba

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2008
Posts
35,771
Reaction score
4,065

FAUDHIA WAZIRI [30] mkazi wa Magomeni Mapipa amefikishwa Mahakama ya Mwanzo ya Magomeni kwa kosa la kumwambia mwenzake ameathirika na gonjwa la ukimwi.

Kauli hiyo ya kashfa aliitoa Desemba 23, mwaka jana, huko Magomeni Makuti, alimwambia Fatuma Said kuwa ameathirika kitendo ambacho ni kinyume na maadili ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Karani Nicolaus Masakandika alidai mbele ya Hakimu Rukia Katembo kuwa, mshitakiwa aliongezea kwa kumkashifu mwenzake kuwa ana tabia ya kuchukua waume za watu.

Hata hivyo mshitakiwa alikana shitaka hilo na kuweza kuwa nje kwa dhamana kwa kutimiza masharti, na kesi hiyo kuahirishwa hadi hapo Januari 20, mwaka huu, itakapotajwa tena.



 
Hapa atashtakiwa kwa kosa gani? Naombeni msaada kwani nadhani kuna kitu cha kujifunza hapa.
 
Hapa atashtakiwa kwa kosa gani? Naombeni msaada kwani nadhani kuna kitu cha kujifunza hapa.
Kamtukana mwenzake. Ukimwi ni kama magonjwa mengine eg. ukichaa. Ukimwambia mtu ni kichaa ni sawa na umemtukana sio? Pia kumwambia achukua waume za watu ni kumchafulia mtu jina sio? Vichwa vya habari vinauza!
 

Sasa mtu mwenye ugonjwa huu, ukitaka kumwelezea kuwa ameathirika, utafanyaje?
 
Kwa ukimwi, tatizo ni jamii yetu inavyouchukuliwa huu ugonjwa, unaonekana kama mtu akiwa nao ni mzinzi, mzembe, hafai nk. Sasa kwa kuuona hivyo, kumwambia mtu ana ukimwi ni kumuonesha mabaya yote yanayoambatanishwa na ugonjwa wenyewe. Kumbe mtu anaweza kuupata bila kufanya ngono (lakini ngono ndio inachangia kwa asilimia kubwa sana). Sasa huyu itabidi akapimwe, kama anao ataambiwa alimnyanyapaa mgonjwa wa ukimwi, kama hana atashitakiwa na kosa la kumwambia ana ukimwi wakati hana, pia atashitakiwa kwa kosa la kumzushia kuwa anachukua wame za watu.
 
Opaque,
Kama kweli Fatuma kaathithirika, anachotakiwa kufanya Faudhia ni kuthibitisha huo uathirika. Ugumu unaweza kuwa kwenye kuthibitisha hilo la kuchukua waume za watu. Akishindwa kutibitisha, kosa lake litakuwa kukashfu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…