MaxShimba
JF-Expert Member
- Apr 11, 2008
- 35,771
- 4,065
FAUDHIA WAZIRI [30] mkazi wa Magomeni Mapipa amefikishwa Mahakama ya Mwanzo ya Magomeni kwa kosa la kumwambia mwenzake ameathirika na gonjwa la ukimwi.
Kauli hiyo ya kashfa aliitoa Desemba 23, mwaka jana, huko Magomeni Makuti, alimwambia Fatuma Said kuwa ameathirika kitendo ambacho ni kinyume na maadili ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Karani Nicolaus Masakandika alidai mbele ya Hakimu Rukia Katembo kuwa, mshitakiwa aliongezea kwa kumkashifu mwenzake kuwa ana tabia ya kuchukua waume za watu.
Hata hivyo mshitakiwa alikana shitaka hilo na kuweza kuwa nje kwa dhamana kwa kutimiza masharti, na kesi hiyo kuahirishwa hadi hapo Januari 20, mwaka huu, itakapotajwa tena.