The redemeer
JF-Expert Member
- Jan 28, 2025
- 1,497
- 2,681
Tunahitaji kusema na tunahitajika kusema maneno machache na yenye maana, kwasababu ukimya una nguvu katika maneno yenye maana, Robert Greene anasema hivi kikamilifu “ watu wenye nguvu huvutia na kuogopesha kwa kusema machache” muhimu kuidhinisha wakati gani uongee na nafasi gani inayokuhitaji uongee
Usijipe leseni ya kusema chochote kila wakati, kwa wowote unaye mtaka na chochote unachotaka, si kwamba unahitaji kuonesha kuwa una nguvu ya kuzungumza lakini unahitaji kuonesha kuwa una nidhamu ya kuzungumza, nidhamu ya kuzungumza ndiyo ufunguo wako
Kuongea kila wakati hukufanya kujenga mabishano na kupasuka kihisia kwasababu hutahitaji kushindwa, upo, huhitajika kuongea sana hata iwe mtandaoni au ana kwa ana kuwa na nidhamu ya kuongea,kuna wakati jibu kwa maana ,ukiona unayemjibu bado anaonesha hali ya kutohitaji kushindwa basi upe ukimya kibali. Uma ulimi wako, udhaifu katika ukimya ni bora kuliko sauti ikosayo maana, vumilia hali ya kutoeleweka kuhitaji kueleweka ni mtego sana katikaka maneno mengi
Tunahitajika kustawisha uwezo wa kusema lakini nidhamu ni kuona namna ya kuidhinisha katika kusema, hakikisha una udhibiti mkubwa na ulimi wako, sio lazima kila wakati watu wasikie maoni yako na hasa wakati haujaombwa,kwasababu tu kuna nafasi hupaswi kujaza, jipe nidhamu ya udhibiti,tumia ukimya kwa faida, udhaifu sio kilema
Kuna wakati unahitajika kutozungumza kwa maneno hata kidogo acha kazi yako iseme badala yako, kuna wakati waoneshe watu kila neno kwako lipo kwasababu, halipo tu ili kujazia uonekane umeongea, ili hilo liweze kufahamika ni lazima ujifunze katika maana ya kukaa kimya, ni vizuri kufikiriwa kuwa unadharau kuliko kujifanya una dharau, ndiyo ni bora kutazamika kama mjinga kuliko kujifanya mjinga, tazamika kuwa mkimya kuliko kujifanya mkimya
Unapozungumza inapaswa kuwa muhimu, unachozungumza kinapaswa kuwa na maana, unapaswa kumaanisha kitu,kumbuka uhuru wa kusema ni haki si wajibu. Zeno wa Citium aliwakumbusha wanafunzi wake kuhusu masikio mawili na mdomo mmoja ili waweze kuheshimu uwiano huo ipasavyo
Acha kutamani kuzungumza zaidi,epuka hiyo tama kuwa na nidhamu katika hiyo tama, wacha wajiulize unafikiria nini, acha maneno unayo yazungumza yawe na uzito sababu ni nadra, unaweza kupuuza tusi na unaweza kukataa mualiko,hupaswi kuwa rahisi
Kubali kujipa muda wa kusilikiliza kuliko kuongea kuwa nanidhamu ya uidhinishaji ndani yako,zungumza pale ambapo una uhakika