Samahani mbona mnatumia Katiba pasipo husika? Ibara hiyo inaruhusu UBAGUZI?Ibara ya 20(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Ibara hiyo inasema:
"Kila mtu anastahili kuwa huru, bila ya kuathiri sheria za nchi, kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kuchanganyika na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo hadharani..."
Hii ndiyo ibara inayotambuliwa kama msingi wa kikatiba wa uhuru wa kukusanyika na kuandamana kwa amani nchini Tanzania.
Hawa ni Wabunge wa JMT lakini ajabu Viongozi wote wa juu wa SEREKALI ya Zanzibar na JMT wamekaa kimyaa kama kwamba hawasikii ama wanaunga mkono kinachoendelea.Msukuma na Waitara wameonesha kuchukizwa na matamshi ya wabunge wanzanzibar kiasi cha kumtaka rais wa Zanzibar awachukulie hatua za kinidhamu hao wabunge. Wabunge wa bara wameanza kuchachamaa dhidi ya ubaguzi wa Wazanzibar